Hivi kwa nini huwa mnalazimisha hoja zenu za kipuuzi ziwe za kipaumbele kitaifa.
Hao vijana watano bado mambo yao yana maswali mengi kuliko majibu.
Wametajwa kufanya biashara kariakoo.
Lakini hiyo biashara haitamkwi au kuwekwa hadharani.
Je hiyo biashara imetajwa rasmi pamoja na usajili wake?
Hawa woote ndugu zao wanaishia kusema walipigiwa simu na rafiki yao. Aliyewataarifu kuwa wamekamatwa.
Lakini kwa mujibu wa kamanda Muliro Jumanne Muliro.
Ndugu hao wameombwa kutoa namba husika woote wameshindwa kuitoa.
Saa ingine mtatuletea hoja za watu binafsi walioamua kwenda kufanya uhalifu mahali au kujiunga na makundi ya kigaidi halafu team majungu Tanzania
mnaanza kudandia hoja bila tafakuri.
Hao dada zao sijui ma shangazi wanadai waliopotea ni watoto.
Lakini wanajichanganya pale wanapomtambulisha mmoja wao kuwa mke wa waliopotea.
Kwa nchi zilizoendelea kijasusi,hao kina dada wangewekewa surveillance ya 24hrs,ikiwemo mawasiliano yao.
Hii issue ingeisha julikana mbivu na mbichi mapema tu.
Wako wapi ndugu zao wa kiume?
Kwa nini wawaachie wanawake jukumu kubwa kama hilo la kutafuta missing persons?
Wanahofia au wamesusia kujihusisha?
Kama wamesusia,je nini sababu ya wao kususia?
Tujadili bila mihemko yenye kuwa biased na upande mmoja kuichafua serikali tu.
Wakati jamii yetu nayo ikiwa chafu kwa matukio ya ajabu na ya kutisha kila uchao?
Kama unao usafiri kwa vipi mjikusanye kwenda beach party bila wenza wenu?
Ndugu Mmoja wa hao waliopotea alikaririwa akisema alimualika kusherehekea sikuu ya krismasi lakini aliomba udhuru hadi itakapofika tarehe 26/12/2021.
Ina maana walikuwa na mission yao ambayo ilikuwa ni muhimu.kuliko mambo ya mualiko wa krismasi.
Huwezi kataa mualiko kisa unaenda beach
Jambo ambalo ni utamaduni uliozoeleka zaidi kijamii ?