sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,182
- 8,948
Nafuatilia Hotuba ya Mh Rais Magufuli akiwa anahutubia Askari Magereza katika sherehe ya uzinduzi wa jengo la ofisi za Magereza, sasa hivi kupitia TBC1 amekiri kuwasamehe wale viongozi wote walioshiriki kusaini mkataba uliokuwa na viashria vya rushwa akiwemo aliyekuwa Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaj ndugu Andengenye na wenzake wanne.
Sambamba na msahama huo ameaidi kumpangia kazi nyingine ndugu Andengenye.
Sambamba na msamaha huo hajaweka wazi kama na yule mzee wetu aliyekuwa mjeda na baadae akawa mbeba sime ya Spika na baadae Waziri mzuri mkata mauno kama nae atamsamehe au la!?
Pia amewatakaMkuu Wilaya ya Dodoma na mkurugenzi wa Jiji la Dodoma wapunguze KUOKOTA sasa WAOE.
Pia soma > Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai
Over.