Rais awasamehe Makamishina walioshirikiana na Kangi Lugola uliokuwa na viashiria vya ufisadi

Watu mnajitekenya ninyi. Hawa walisimamishwa kupisha Uchunguzi. Walifunguliwa mashtaka lini? Tuhuma zao ilikuwa kusaini mkataba usio na maslahi kwa Taifa , wakisainia nje ya nchi. Mkataba umevunjwa sasa mumeibiwa nini? saini?
Hatua ya uchunguzi? Kwa hiyo kelele zote zile ilikuwa ni za nini? Amekuwa mtoto wa chekechea?
 
Ndio maana nikasema Mh rais ana penda sana maneno ya kudanganywa. Namfahamu sana Andengenye tangu akiwa askari wa kawaida Namanga kipindi cha rushwa za bia za Kenya. Hakuwa na tabia ya rushwa alikuwa mpenda haki, akaja kuwa Rpc Moro na Arusha alikuwa mwadilifu sana Hata sungusungu tume zunguka nae akiwa Rpc na alikuwa hapendi mtu kuonewa. Aje kuwa IG wa Zima moto abadilike? Hili jambo liliniumiza sana na sikipenda kuamini.
Nafurahi sasa Mh rais ameuona ukweli.
 
Na mjomba anapenda sana kuombwa ombwa msamaha,Nape alienda kuomba msamaha,Kinana nae,Boss wa zimamoto nae ameomba msamaha yaani daah.

Nape yeye alivyoenda kuomba msamaha akajibiwa Nape ameniomba msamaha na nimemsamehe lkn kusamehe kunauma.,hahah.
 
Wewe ndiyo Ande ?
 
System ilisuka njia ya kuondoa shame kwa mamlaka ya uteuzi wa kangi, kukata mauno kulikuwa kunaikera system na haikupenda kuendelea kupata aibu hiyo.

Mtu anayeongoza askari anaenda kumkatia mauno hadharani

Hivyo kangi akatafutiwa tu ka zengwe, akapangishwa kwenye jumba bovu, likamwangukia
 
Serikali inayopambana na ufisadi.

ivi mfano mimi nikafanya ufisadi nikaomba msamaha atanielewa .?
 
Alikuwa anahutubia jeshi la magereza au jeshi la zima moto...?
 
Sishangai maana Leo amesema alipokuwa jeshini alikuwa ana blasti au kushtua kwa maana nyingine alikuwa anavuta bangi.
 
Watu mnajitekenya ninyi. Hawa walisimamishwa kupisha Uchunguzi. Walifunguliwa mashtaka lini? Tuhuma zao ilikuwa kusaini mkataba usio na maslahi kwa Taifa , wakisainia nje ya nchi. Mkataba umevunjwa sasa mumeibiwa nini? saini?
Nauliza nini maana ya kuomba msamaha mala 3
 
Kama Kangi alimuacha ulitegemea awaguse hao?!

Wale TAKUKURU nao waone aibu sasa, sio kuhangaika na Chadema tu.
 
Na mjomba anapenda sana kuombwa ombwa msamaha,Nape alienda kuomba msamaha,Kinana nae,Boss wa zimamoto nae ameomba msamaha yaani daah.

Nape yeye alivyoenda kuomba msamaha akajibiwa Nape ameniomba msamaha na nimemsamehe lkn kusamehe kunauma.,hahah.
"Kutangulia kwa jengo hili ambalo mmelijenga kwa juhudi zenu ni mfano mzuri na ninajua haya mawazo ya aliyekuwa Kamishna Jenerali Andengenye,mkamfikishie salamu kwamba nimemsamehe,na hata kwasababu ameshaniomba msamaha karibu mara tatu,ni unyenyekevu wa aina yake".JPM.

#UzinduziJengolazimamoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…