Rais Biden awataka raia wa Marekani kuondoka Ukraine. Vita vikianza hatatuma vikosi kuwaokoa

Rais Biden awataka raia wa Marekani kuondoka Ukraine. Vita vikianza hatatuma vikosi kuwaokoa

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
1644565455883.png

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa raia wote wa Marekani waliosalia nchini Ukraine kuondoka nchini humo mara moja kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya kuchukuliwa hatua za kijeshi za Urusi.

Bw Biden alisema hatatuma wanajeshi kuwaokoa Wamarekani ikiwa Moscow itavamia Ukraine.

Alionya kwamba "mambo yanaweza kutokea haraka" katika eneo hilo.

Urusi imekanusha mara kwa mara mpango wowote wa kuivamia Ukraine licha ya kuwa na wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka.

Lakini ndiyo kwanza imeanza mazoezi makubwa ya kijeshi na nchi jirani ya Belarus, na Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuizuia kuingia baharini.

Kremlin inasema inataka kutekeleza "mistari nyekundu" ili kuhakikisha kuwa jirani yake wa zamani wa Soviet haingii NATO.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema Alhamisi kwamba Ulaya inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa usalama katika miongo kadhaa huku kukiwa na mvutano.

Source BBC NEWS

Je, ni kweli Russia haitanii kuivamia Ukraine pamoja na vitisho vya wababe wa dunia NATO, EU?
Russia-exercising-amphibious-assault.jpg
 
Kwa maana hiyo ni kwamba Marekani anaufyata kwa Urusi?

"Hatutapeleka wanajeshi wetu" hii tafsiri yake ni kwamba hatuna uwezo wa kuwazuia hawa jamaa wakianza jambo lao

na hatuna vifaa vya kupambana nao..hii kauli ya Biden ni ya kuitafakari haswaa kwa hao wamarekani waishio Ukraine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani Marekani yuko obssessed sana na mzozo wa Ukraina na Urusi kuliko nchi majirani wanaozunguka Ukraine. Sijajua ana maslahi gani pale mahali
 
Yaani Marekani yuko obssessed sana na mzozo wa Ukraina na Urusi kuliko nchi majirani wanaozunguka Ukraine. Sijajua ana maslahi gani pale mahali
Porojo za kuzuia dili ya Bomba la Gas liliounganishwa kutoka Urusi mpaka Ujerumani lisianze au lisitishwe , ili auze Gas yake Ulaya. Ndio maana wenye akili wanamchora tu Mmarekani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hii kauli ina makusudi ya kutengeneza 'necessary panic' kwa raia wa Marekani nchini Ukraine ili kuondoka nchini humo kwa haraka zaidi. Sidhani kama ina mahusiano yoyote na Marekani kupeleka jeshi ama la. Maana juzi tu, White House ime-approve mpango wa Pentagon wa kupeleka kikosi cha uokozi karibu kabisa na Ukraine.

Hata hivyo, kabla hata ya kauli hii kutolewa, tayari kuna vikosi kadhaa vya jeshi la Marekani vimekwisha pelekwa nchi kadhaa za Ulaya Mashariki na zinazopakana na Ukraine kwaajili ya jukumu maalumu la kujihami.
 
Rais Joe Biden amewataka wamerekani waliopo Ukraine kuondoka mara moja baada ya kuona kuna kina dalili ya Russia kuinyakua Ukraine muda wowote kabla ya michezo ya Olimpiki kumaliza ama baada.. na amesisitiza hatatuma wanajeshi kwenda Ukraine kuwakomboa raia hao watakao kaidi..swali la kujiuliza Marekani na mikwara yote leo wanaishia kusema hawatatuma wanajeshi kwenda kuwaokoa raia wao watakao kaidi kutoroka mapema kabla Ukraine haijaanza kushushiwa kipigo cha mbwa mwizi...vyanzo vinasema Russia anazidi kupeleka wanajeshi pamoja na zana nzito wakati huo Luteka kubwa ya kijeshi ikiendelea Nchini Belarus...Rais wa Ukraine ameingiwa hofu baada kuona Nchi yake itaingia kwenye mikono ya wanyang'anyi mda wowote..
 
Putin anaamua kuichukua Ukraine wakati huu maana keshagundua Marekani chini ya Biden haiwezi kumfanya lolote uzuri NATO mwendawazimu Trump aliidhoofisha sana
Hamna Nchi ya Ulaya ipo tayari kuona miji yake ikibaki magofu wamejitaidi sana kwenda Moscow lakini Russia wametoa masharti yao na wanajifanya wanagoma ngoja Ukraine inyakuliwe iwe chini Kremlin ndio NATO watafarakana
 
Hii kauli ina makusudi ya kutengeneza 'necessary panic' kwa raia wa Marekani nchini Ukraine ili kuondoka nchini humo kwa haraka zaidi. Sidhani kama ina mahusiano yoyote na Marekani kupeleka jeshi ama la. Maana juzi tu, White House ime-approve mpango wa Pentagon wa kupeleka kikosi cha uokozi karibu kabisa na Ukraine.

Hata hivyo, kabla hata ya kauli hii kutolewa, tayari kuna vikosi kadhaa vya jeshi la Marekani vimekwisha pelekwa nchi kadhaa za Ulaya Mashariki na zinazopakana na Ukraine kwaajili ya jukumu maalumu la kujihami.
sio utani Russia ameshafunga bahari ya nyeusi na sea of azov Ukraine amebaki kulia yupo anapiga mazoezi ya kijeshi usa na nato wameshatambua jamaa hatanii licha ya mikwara mbuzi
 
Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa raia wote wa Marekani waliosalia nchini Ukraine kuondoka nchini humo mara moja kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya kuchukuliwa hatua za kijeshi za Urusi.

Bw Biden alisema hatatuma wanajeshi kuwaokoa Wamarekani ikiwa Moscow itavamia Ukraine.

Alionya kwamba "mambo yanaweza kutokea haraka" katika eneo hilo.

Urusi imekanusha mara kwa mara mpango wowote wa kuivamia Ukraine licha ya kuwa na wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka.

Lakini ndiyo kwanza imeanza mazoezi makubwa ya kijeshi na nchi jirani ya Belarus, na Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuizuia kuingia baharini.

Kremlin inasema inataka kutekeleza "mistari nyekundu" ili kuhakikisha kuwa jirani yake wa zamani wa Soviet haingii NATO.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema Alhamisi kwamba Ulaya inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa usalama katika miongo kadhaa huku kukiwa na mvutano.

Source BBC NEWS

Je ni kweli Russia haitanii kuivamia Ukraine pamoja na vitisho vya wababe wa dunia NATO, EU....?
View attachment 2115599

Hakutakuwa na vita! Marekani wanabwaka hovyo hovyo tu na kuwatishia watu bure.
 
Ukiangalia geographically, Putin roho inamuuma sana na yupo tayari kupigana kwa namna yoyote ile ilimradi amzuie Us kusogelea mpaka wake Ukraine kupitia Nato.

Kidume kimetoa oda kwamba marufuku Ukraine kujiunga nato, ngoja tuone.
 
Back
Top Bottom