Rais Biden awataka raia wa Marekani kuondoka Ukraine. Vita vikianza hatatuma vikosi kuwaokoa

Rais Biden awataka raia wa Marekani kuondoka Ukraine. Vita vikianza hatatuma vikosi kuwaokoa


Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa raia wote wa Marekani waliosalia nchini Ukraine kuondoka nchini humo mara moja kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya kuchukuliwa hatua za kijeshi za Urusi.

Bw Biden alisema hatatuma wanajeshi kuwaokoa Wamarekani ikiwa Moscow itavamia Ukraine.

Alionya kwamba "mambo yanaweza kutokea haraka" katika eneo hilo.

Urusi imekanusha mara kwa mara mpango wowote wa kuivamia Ukraine licha ya kuwa na wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka.

Lakini ndiyo kwanza imeanza mazoezi makubwa ya kijeshi na nchi jirani ya Belarus, na Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuizuia kuingia baharini.

Kremlin inasema inataka kutekeleza "mistari nyekundu" ili kuhakikisha kuwa jirani yake wa zamani wa Soviet haingii NATO.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema Alhamisi kwamba Ulaya inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa usalama katika miongo kadhaa huku kukiwa na mvutano.

Source BBC NEWS

Je ni kweli Russia haitanii kuivamia Ukraine pamoja na vitisho vya wababe wa dunia NATO, EU....?
View attachment 2115599
Aiseee [emoji13]
 
Ukraine anatakiwa aelewe kwamba msaada atakaopewa na NATO ni silaha tuu ila front wajiandae kuingia wenyewe..

Screenshot_20220211-183411.png
 
NATO inatamani sana kupata washirika wa iliyokuwa USSR ili wapate kushare utaalam wa silaha za iliyokuwa Shirikisho la Urusi...
 
Porojo za kuzuia dili ya Bomba la Gas liliounganishwa kutoka Urusi mpaka Ujerumani lisianze au lisitishwe , ili auze Gas yake Ulaya. Ndio maana wenye akili wanamchora tu Mmarekani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sure mkuu.....coz anaona Kama .....Russia atafaidi Sana na ile Nord stream project
 
Hii kauli ina makusudi ya kutengeneza 'necessary panic' kwa raia wa Marekani nchini Ukraine ili kuondoka nchini humo kwa haraka zaidi. Sidhani kama ina mahusiano yoyote na Marekani kupeleka jeshi ama la. Maana juzi tu, White House ime-approve mpango wa Pentagon wa kupeleka kikosi cha uokozi karibu kabisa na Ukraine.

Hata hivyo, kabla hata ya kauli hii kutolewa, tayari kuna vikosi kadhaa vya jeshi la Marekani vimekwisha pelekwa nchi kadhaa za Ulaya Mashariki na zinazopakana na Ukraine kwaajili ya jukumu maalumu la kujihami.
Daaaaah......kimeumana......kwenye hili suala nilimkubali tu mu Iran ....

Alitiishia kuwa yeyote atakaye kubali majesh ya marekan kuweka kambi pale middle East........atakufa Nae[emoji23][emoji23]
 
Rais Joe Biden amewataka wamerekani waliopo Ukraine kuondoka mara moja baada ya kuona kuna kina dalili ya Russia kuinyakua Ukraine muda wowote kabla ya michezo ya Olimpiki kumaliza ama baada.. na amesisitiza hatatuma wanajeshi kwenda Ukraine kuwakomboa raia hao watakao kaidi..swali la kujiuliza Marekani na mikwara yote leo wanaishia kusema hawatatuma wanajeshi kwenda kuwaokoa raia wao watakao kaidi kutoroka mapema kabla Ukraine haijaanza kushushiwa kipigo cha mbwa mwizi...vyanzo vinasema Russia anazidi kupeleka wanajeshi pamoja na zana nzito wakati huo Luteka kubwa ya kijeshi ikiendelea Nchini Belarus...Rais wa Ukraine ameingiwa hofu baada kuona Nchi yake itaingia kwenye mikono ya wanyang'anyi mda wowote..
Raisi wa Ukraine....Alisema ... wananchi wake wapo tayari kwa mapigano
 
Putin anaamua kuichukua Ukraine wakati huu maana keshagundua Marekani chini ya Biden haiwezi kumfanya lolote uzuri NATO mwendawazimu Trump aliidhoofisha sana
Ukicheki kwa makini .....ni Kama kweli Trump .....alikuwa anatumwa......coz Kuna muda alitaka kuivunja NATO[emoji23][emoji23]
 
Hamna Nchi ya Ulaya ipo tayari kuona miji yake ikibaki magofu wamejitaidi sana kwenda Moscow lakini Russia wametoa masharti yao na wanajifanya wanagoma ngoja Ukraine inyakuliwe iwe chini Kremlin ndio NATO watafarakana
Yule jamaa.....ukicheki kwa makin ni Kama muoga flan
 
Raisi wa Ukraine....Alisema ... wananchi wake wapo tayari kwa mapigano
Shida baadhi ya wananchi wa ukraine wana asili ya urusi.......kuna vita ya chinichini hadi kwenye kanisa lao la orthodox.........kuna makanisa yamekubali kua chini ya kiongozi wa russia ....huku wengine wakitaka kanisa la Ukraine lijitenge............mrusi anaweza akaichukua hii nchi kama karata zake atacheza vizuri
 
sio utani Russia ameshafunga bahari ya nyeusi na sea of azov Ukraine amebaki kulia yupo anapiga mazoezi ya kijeshi usa na nato wameshatambua jamaa hatanii licha ya mikwara mbuzi
Boris Jonson ....kakubali kuwa umoja wa ulaya unapitia TENSION kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa
 
Back
Top Bottom