Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
Dkt. John Pombe Magufuli, hongera sana kwa kutekeleza vema majukumu yako ya urais
Naomba kukukumbusha juu ya maombi ya kutengewa mkoa mpya wa Nyakanazi. Mkoa huu ilipendekezwa uundwe na wilaya za Kakonko na Kibondo (Kigoma), na Ngara na Biharamulo (Kagera). Mkoa huu uwe na jumla ya wilaya nne.
Sababu za kutenga mkoa:-
(i). Kutoka Ngara - Bukoba (300kms), Biharamulo - Bukoba (200kms), Kakonko - Kigoma (300kms), na Kibondo - Kigoma (250kms). Kwa haraka ni kuwa mzazi akihitaji kuhamisha mtoto wa shule tu gharama zinakuwa kubwa, watendaji wa Serikali wanaposafiri hutumia mafuta mengi, muda mwingi nk
Kutoka wilaya hizo kuja Nyakanazi:-
Kibondo - Nyakanazi (90kms), Kakonko - Nyakanazi (51kms), Ngara - Nyakanazi (90kms), na Biharamulo - Nyakanazi (45kms). Sifa za eneo hili kuunda mkoa zinatosha sana. Wakuu wa wilaya wanabaki hivyo hivyo, majimbo ya uchaguzi yanabaki hivyo hivyo kitakachoongezeka ni Ofisi ya Mkuu wa mkoa na mamlaka zake.
Dkt. John Pombe Magufuli (Rais), naleta kwako maombi haya mahususi nikiamini kuwa utatenda lkn niseme tulikuomba, tunakuomba na tutakuomba.
Mungu akubariki wewe na wananchi unaowaongoza,
Mungu ibariki Tanzania
Msakila M Kabende
Kigoma
13 Januari, 2021