Rais Dkt. John Pombe Magufuli, tunaendelea kukuomba Mkoa mpya wa Nyakanazi

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, tunaendelea kukuomba Mkoa mpya wa Nyakanazi

Dkt. John Pombe Magufuli, hongera sana kwa kutekeleza vema majukumu yako ya urais

Naomba kukukumbusha juu ya maombi ya kutengewa mkoa mpya wa Nyakanazi. Mkoa huu ilipendekezwa uundwe na wilaya za Kakonko na Kibondo (Kigoma), na Ngara na Biharamulo (Kagera). Mkoa huu uwe na jumla ya wilaya nne.

Sababu za kutenga mkoa:-

(i). Kutoka Ngara - Bukoba (300kms), Biharamulo - Bukoba (200kms), Kakonko - Kigoma (300kms), na Kibondo - Kigoma (250kms). Kwa haraka ni kuwa mzazi akihitaji kuhamisha mtoto wa shule tu gharama zinakuwa kubwa, watendaji wa Serikali wanaposafiri hutumia mafuta mengi, muda mwingi nk

Kutoka wilaya hizo kuja Nyakanazi:-
Kibondo - Nyakanazi (90kms), Kakonko - Nyakanazi (51kms), Ngara - Nyakanazi (90kms), na Biharamulo - Nyakanazi (45kms). Sifa za eneo hili kuunda mkoa zinatosha sana. Wakuu wa wilaya wanabaki hivyo hivyo, majimbo ya uchaguzi yanabaki hivyo hivyo kitakachoongezeka ni Ofisi ya Mkuu wa mkoa na mamlaka zake.

Dkt. John Pombe Magufuli (Rais), naleta kwako maombi haya mahususi nikiamini kuwa utatenda lkn niseme tulikuomba, tunakuomba na tutakuomba.

Mungu akubariki wewe na wananchi unaowaongoza,
Mungu ibariki Tanzania

Msakila M Kabende
Kigoma
13 Januari, 2021
Bangi hizi,hivi ukianzisha mkoa mwingine,ndio unapata hospitali nzuri,shule nzuri,viwanda,hapo ni kuongeza gharama za serikali,tunachotakiwa ni kupunguza idadi ya mikoa,iwe 15,futa vyeo vya wakuu wa mikoa,futa vyeo vya wakurugenzi wa halmashauri,
Hizo pesa zitumike kutengeneza viwanda,hakuna uhusiano na kikundi Cha watu kuwa na Mkuu wa wilaya,Mkuu wa mkoa,Mbunge,na maendeleo yao,Kwanza wabunge wengi wakishachaguliwa,uhamia Dar,Kama waziri wa elimu,DED,DAS,RAC,wanajua matatizo ya sehemu flani,sasa mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa wanakazi gani zaidi ya kuvunja Sheria tu,hawana kazi maalum
 
Si wajibu wangu kujua yumo au hayumo humu - hili ni jukwaa huru la kisiasa. Jenga tabia ya kuskip hoja unapokuwa huna cha kuchangia.
Wewe una hoja gani zaidi ya kuonyesha upuuzi wako hapa! kwa akili yako ndogo unaona umeandika point kubwa sn? acha kujaza takataka server za watu
 
Bangi hizi,hivi ukianzisha mkoa mwingine,ndio unapata hospitali nzuri,shule nzuri,viwanda,hapo ni kuongeza gharama za serikali,tunachotakiwa ni kupunguza idadi ya mikoa,iwe 15,futa vyeo vya wakuu wa mikoa,futa vyeo vya wakurugenzi wa halmashauri,
Hizo pesa zitumike kutengeneza viwanda,hakuna uhusiano na kikundi Cha watu kuwa na Mkuu wa wilaya,Mkuu wa mkoa,Mbunge,na maendeleo yao,Kwanza wabunge wengi wakishachaguliwa,uhamia Dar,Kama waziri wa elimu,DED,DAS,RAC,wanajua matatizo ya sehemu flani,sasa mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa wanakazi gani zaidi ya kuvunja Sheria tu,hawana kazi maalum
Point tupu mkuu umeandika kuliko huyu mpuuzi aliyeleta takataka hapa, inatakiwa mikoa ibaki hata mitano inatosha.
 
Inaonekana wew jamaa ni mtumishi hapo Nyakanazi na unajua ikipanda hadhi kuwa mkoa basi na wewe umeula!
 
Bangi hizi,hivi ukianzisha mkoa mwingine,ndio unapata hospitali nzuri,shule nzuri,viwanda,hapo ni kuongeza gharama za serikali,tunachotakiwa ni kupunguza idadi ya mikoa,iwe 15,futa vyeo vya wakuu wa mikoa,futa vyeo vya wakurugenzi wa halmashauri,
Hizo pesa zitumike kutengeneza viwanda,hakuna uhusiano na kikundi Cha watu kuwa na Mkuu wa wilaya,Mkuu wa mkoa,Mbunge,na maendeleo yao,Kwanza wabunge wengi wakishachaguliwa,uhamia Dar,Kama waziri wa elimu,DED,DAS,RAC,wanajua matatizo ya sehemu flani,sasa mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa wanakazi gani zaidi ya kuvunja Sheria tu,hawana kazi maalum
Hii ni ilani yenu na Lissu - CCM tunaamini uanzishwaji maeneo ya kiutawala ni moja ya huduma (wananchi wanapata vijiji, kata, wilaya, na mikoa); wananchi wanapata huduma karibu
 
Hii ni ilani yenu na Lissu - CCM tunaamini uanzishwaji maeneo ya kiutawala ni moja ya huduma (wananchi wanapata vijiji, kata, wilaya, na mikoa); wananchi wanapata huduma karibu
Mara ya mwisho umesikia USA,UK,au japan inaongeza mkoa,state,ni lini?
Hizi nchi ni tajiri,lakini haziongezi maeneo ya kiutawala,zinaongeza viwanda,sie maskini,tupo bize na uteuzi,na kuongeza watawala tu,hatuna madarasa ya kutosha,mikopo ya Elimu ya juu,hairipiki,harafu magenius wetu wanaona kuongeza mikoa ndio suluhisho,
 
Kwamba majiji yao hayakuanza yakiwa Kijiji, mji, jiji, na sasa Metropole? Yamefikaje hapo

Hata hivyo sisi hatuigi kila kitu toka kwao
 
Nilishatoa ufafanuzi kabla, nirudie tena kukujuza kuwa hakuna halmashauri nchini isiyokuwa na vyanzo vya mapato ingawa haimanishi kwamba vyanzo hivyo hulingana (mfano ktk mkoa wa Kagera halmashauri ya Bukoba hailingani na Karagwe)

Suala la pili ni kuwa mfumo wa kodi zetu hukusanya kodi na kuziweka Serikali kuu, kisha fedha hizo hutekeleza majukumu kadhaa (mishahara = salaries, miradi ya maendeleo = development projects, na matumizi mengineyo = other charges) ktk mikoa kulingana na vipaumbele.

Kwa ufupi ni kuwa hakuna mkoa unaoendeshwa kwa makusanyo yake yenyewe.
Sawa ikitokea nsinisahau katika teuzi
 
Mtoa mada anahoja za msingi sana, ushauri wangu wabunge na wadau eneo husika wapaze sauti.
Fikra za mkoa wa Rubondo hazina mashiko ukilinganisha na uhitaji halisia.
Hujui kuwa Rubondo ndiyo kitovu cha utalii kwetu kanda maalum?
 
Ungesema nimesotaje!
Na hili linahusiana vipi na mada yangu jmn? Mada inahusu kuwa na mkoa mpya wa Nyakanazi, mambo ya vyeo yafungulie mada nyingine inayojitegemea
Hivi kwenye thread yako umekumbuka kuweka kabisa na nambari ya rununu?
 
Watanzania wengi bado tuna akili zilizopitwa na wakati kabisa (obsolete)!
Katika zama hizi za TEHAMA (Advanced ICT) bado mtu anajadili ukubwa wa Mkoa na vitu vingine myopic!

Tunatakiwa kupunguza gharama za uendeshaji wa Nchi hii ili rasilimali zitumike kusomesha Watoto wa Tanzania ili waje wapambane katika Dunia na Sayari ya Mars za Elon Musk!

Tunakokwenda mambo yote yanakwenda kuendeshwa kwa "AI" ( Artificial Intelligence).

Gharama za kuwa na Wakuu wa Wilaya, Ma DAS , Wabunge 394 kwa Nchi maskini kama Tanzania lazima ziangaliwe upya.

Kwa maendeleo ya TEHAMA hakuna hata sababu ya kuwa na Bunge linalokutana Dodoma kila wakati na vitu kama miezi 3 ya Bunge la Budget!

Kila Mbunge akae jimboni kwake, ofisi zao ziunganishwe na vifaa vya TEHAMA na Bunge liendeshwe kwa Teleconferencing na tutaokoa mabilioni mengi katika matumizi yasiyo na msingi na fedha zote hizo zipelekwe kwenye kuboresha elimu yetu!

Wakati Mwl.Julius K.Nyerere anafikiria kuweka Makao Makuu ya Nchi Dodoma, aliona kuwa pale ni katikati ya Nchi na hivyo aliangalia zaidi suala la umbali kutoka kila upande wa Nchi.

Leo katika mapinduzi ya TEHAMA kama unafikiri sawasawa hata suala la kuweka Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi kwa kigezo cha umbali na kuwa ni katikati unaweza kuona ni IRRELEVANT!
 
Back
Top Bottom