Kuna kitu hukijui kwa faida ya wengine elewa yafuatayo:-
(i). Mwaka 2014 agenda ya kugawa maeneo ya kiutawala kwa kutenga mkoa wa Nyakanazi ilijadiliwa na kupitishwa na RCC Kigoma (kikao kilikubali wilaya ya Kakonko na Kibondo ziunde mkoa mpya wa Nyakanazi)
Mwaka huo huo mkoani Kagera chini ya RC Kanali Fabian Massawe alielekeza kikao cha RCC kiwe na agenda ya kuichukuwa Biharamulo na Ngara ili ziunde mkoa wa Nyakanazi. Kikao kikiwa kwenye hatua za mwisho kufanyika ndipo yalifanyika mabadiriko ya kiuongozi ambapo Kanali Fabian Massawe alitenguliwa na nafasi hiyo kuwekwa RC wa sasa wa Mwanza Mongella. Siku ya kikao agenda hii iliwasilishwa kisha akaagiza kwa kuwa ni mgeni iahirishwe itajadiliwa baadae.
So, muda ulienda ndipo 2015 tuliingia ktk uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi alihamishiwa Mwanza. Lkn pia kama unakumbuka baada ya Rais kuchaguliwa aliagiza kuwa ktk kipindi hicho maeneo mapya ya kiutawala si kipaumbele kwake. Ndiyo maana niliandika "tulikuomba, tunakuomba, na tutamwomba"
Kama hujaelewa niambie nikupe zaidi