Rais Dkt. Magufuli tuko katika Majonzi makubwa, lakini Kocha wa Yanga ametutukana Watanzania wote. Akamatwe upesi

Rais Dkt. Magufuli tuko katika Majonzi makubwa, lakini Kocha wa Yanga ametutukana Watanzania wote. Akamatwe upesi

Ukweli ni mchungu.. mimi mwanayanga ila najua uongozi wa yanga umejaza wajinga.

Yanga miaka yote ni shamba la bibi la wapigaji
 
Sasa wenyewe YANGA mnajiita UTOPOLO, yeye akiwaita Nyani MNALIA LIA! utopolo mnazingua acheni kulia lia
 
Tungekuwa na elimu,tungekuwa na akili unadhani ccm ingetutawala for 60 good years? Hata hivyo viwanja vya kufugia mbwa ccm walijimilikisha na still wameshindwa kuvitunza? Kwa ujumla if I can summary yote aliyosema ni kuwa.Watu wenye akili hawawezi kutawaliwa na CCM,watu wenye akili hawawezi wakaambiwa na mwanasiasa tena akiwa amejifungia kijijini kwake kuwa Covid_19 imeisha wanakubali kirahisi,kumuamini na Kisha kujiachia Kama wanavyofanya watanzania.
Unatakiwa ukamatwe ukatoswe baharini
 
6edf1a86-7fc5-4909-a3fc-bbdadae2fada.jpg
 
Hii haivumiliki na GENTAMYCINE nasema tena kuwa hii haivumiliki na namuomba Waziri wa Michezo aamuru Jeshi la Polisi nchini Tanzania chini yake IGP upesi sana wamsake ( wamtafute ) popote pale alipo Kocha wa Yanga SC Raia Ubelgiji Luc Eymael kwa ‘ Matamshi ‘ ya Kuidhalilisha Tanzania na hadi Sisi Watanzania.

Muda si mrefu Kituo cha Redio cha Wasafi FM katika Kipindi chao ‘ Maarufu ‘ cha Michezo Kiitwacho ‘ Sports Court ‘ kimetoka Kucheza ‘ Sauti ‘ ya Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga SC ambayo kiukweli aliyoyasema huko ‘ hayavumiliki ‘ na naenda kuweka hapa baadhi ya ‘ Kashfa ‘ zake Kwetu Watanzania…


  1. Tanzania ni nchi ya Kipuuzi sana
  2. Viongozi wa Tanzania ni Wahuni
  3. Mashabiki wa Yanga SC hawajui Mpira ni kama Nyani au Sokwe ( a.k.a mpya ya Yanga SC sasa ni Sokwe Nyani SC badala ya Utopolo SC )
  4. Shirikisho la Mpira nchini Tanzania lina Watu Wajinga mno na Wanaipendelea mno Simba SC
  5. Watanzania wengi ni Watu ambao hawana Elimu na wapo wapo tu
  6. Uongozi wa Yanga SC ni wa Watu Wapumbavu na Waongo nitashangaa Klabu ikipata Maendeleo chini yao
  7. Viwanja vingi vya Soka vya Tanzania ni vya Kufugia Mbwa na hata huu mnaousifia nao ni Mbovu tu
Na kutokana na ‘ Maadili ‘ kuna maneno yake mengine ya ‘ Matusi ‘ makubwa makubwa Kocha huyu ‘ Katutukana ‘ Sisi Watanzania. Japo ‘ Hasira ‘ zake nyingi zilikuwa ni kwa ‘ Mashabiki ‘ wa Yanga SC na Uongozi wake lakini pia ‘ ametutukana ‘ sana Watanzania na Rais wetu JPM nae ni Mtanzania vile vile.

Kwa wale ambao mtapenda Kusikia ‘ Kashfa ‘ hizi nzito za Kocha wa Yanga SC Mbelgiji Luc Eymael kwa Watanzania na Klabu ya Yanga SC Kesho Saa 2 na Nusu hadi Saa 5 Kamili asubuhi tegea Sikio Wasafi FM hasa katika Kipindi chao cha Michezo cha ‘ Sports Arena ‘ ambapo wameahidi Kuirudia hiyo ‘ Sauti ‘ huku wakisema kuwa Kesho ni Siku ya Kocha wa Yanga SC Luc Eymael.

Kwa ‘ Udhalilishaji ‘ aliousema Kocha wa Yanga SC Luc Eymael nitashangaa kama kuanzia Usiku huu hadi Kesho kama ‘ hajakamatwa ‘ na Mamlaka husika. Na kwa msiojua hii ni mara ya Pili Kocha huyu ‘ Mpumbavu ‘ anaichokonoa Tanzania kwani alipokuja alishawahi ‘ Kuhitilafiana ‘ na Shirikisho la Soka nchini na ‘ Kutishia ‘ kuwaambia Wazungu huko Ulaya kuwa wasije Kutalii nchini Tanzania.

Kwa wale mliopo katika Makundi ya WhatsApp ya Wanahabari za Michezo nadhani hivi sasa mnaisikia hiyo ' Clip ' ya huyu Kocha. Ni balaa tupu!!!!
Kama kawatukana yanga na mashabiki wake ni sawa. Tena ametumia sauti ndogo sana. Namshauri aongeze sauti.
 
Ni kweli katukana ila ukiangalia na mfumo wa mpira tanzania ulivo na mambo yalivo sioni pa kumlaumu kwa matusi yake ila kasema ukweli mtupu hvo tupunguze jazba half turekebishe tunapokosea
Over
 
kwani huyo jamaa kawatukana WATANZANIA au kawatukana utopolo fc
 
Bila sababu wala aibu ametukana nchi na taasisi zote za michezo mbwa nyani wajinga. Kwa kweli kwa uhuni alioonyesha alistahili kupigwa palepale na kuwekwa ndani mara moja .
Kwa kosa gani hebu acha kubweka bweka
 
Mashabiki wa utopolo mnadhalauliwa hadi na kibarua wenu(coach, morison) mnashindwa kumtimua morison mnatimua kocha ambae anadai stahiki za kimkataba wake na mkataba umeisha,

Angeweza kuomba msamaha kocha wenu maana ubaguzi hauwez kuisha duniani kati ya ngozi nyeupe na mtu mweusi
 
Back
Top Bottom