Ukiamua kujitoa kupambania course fulani hutakiwi kuwa na excuses, unapambana huku ukiijua vizuri jamii yako ikoje. Siyo unapambana halafu usipofanikiwa unaanza kulaumu wananchi ni ujnga. Maana kwanza ulipoanza kutangaza sera za chama chako kwa wananchi, ulianza wewe kama wewe kuwafuata wananchi na kuwaaminisha kuwa wewe ndiye wa kuwatoa point moja kwenda ya pili iliyobora zaidi, siyo wananchi waliokufuata na kukwambia kuwa njoo utupiganie, yalikuwa ni maono yako binafsi. Sasa upo katikati ya struggle na huku tukiwa tunaenda vizuri isipokuwa inahitajika kuweka vitu fulani sawasawa unaanza kukata tamaa na kulaumu wananchi, kufanya hivyo ni kusaliti course yako mwenyewe!
Wananchi wameshawaamini wapinzani na ndiyo maana wanawapa kura nyingi tu ila wale majambazi wa kisiasa wanapora!
Sasa hapa Wapinzani wenye akili wanapaswa wajipongeze kuwa kwenye uwanja wa kisiasa tumeshaeleweka kwa wananchi, sasa tufanye nini twende hatua ya pili. Huo ndo uongozi!
Na mapambano siyo lazima ushinde pambano leo au mwakani au baada ya miaka 10 inaweza kuchukua hata miaka 50 lakini sharti ni. lazima usimamie misimamo ya msingi bila kuyumba na kwa kuvumilia tabu, na mateso.
Civil rights movement hawakupata mafanikio kwa struggle ya miaka 10 tu, waliendelea kupambana na kupambana mpaka wakapata nafuu kubwa. ANC haikumuangusha Kaburu kwa miaka 20, iliwachukua zaidi ya miaka 80 ya kupambana na kupambana. Wewe unafikiri ndani ya South Africa hakuna watu waliokuwa wakila bata kwa kushirikana na serikali ya Kikaburu, mfano ni Chief Mongustu Buthelezi wa chama cha Inkatha, lakini hii haikuwazuia akina Oliver Tambo kuendelea kupambana wakiwa in exile.
Kwa hiyo ukiona kingozi wa kisiasa eti anawakatia tamaa wananchi ambao kimsubgi waeshaonyesha kumuunga mkono kwenye sanduku la kura basi huy siyo kiongozi ni. mchumia tumbo!
Ukiwa kiongozi kweli utawaonyesha wananchi njia A, B, C za kuresist na uwe na subira wakati wakijiadapt kuzifuata hizo njia, usiwalazimishe maana vitu vingine vinakuwa ni vigeni kwao!
Kiongozi wa kweli hawezi kulaumu wananchi, wakati at the end of the day hata mshahara wake, au ruzuku ya chama chake, au uhalali wa uwepo wa chama chake msingi wake ni wananchi!