Yani nchi hii!?? Kwahyo mtu awe Rais miaka 20!? Are we this stupid!??
Alafu rekebisha title address hakuna kitu kama ...'Rais Dr.'
 
Hoja zako ni za kijinga, miji lazima iwe na utaratibu maalum wa sehemu za kufanyia bishara, pia hilo la umeme ni kwamba bara tunabebeshwa mizigo ya bili za umeme za wala urojo. Ila hija yako ya hiyo kuwa Rais naounga mkono kwa sababu tofauti na hizo ulizotaja.
 
Mji msafi alafu watu wana njaa?

Machinga aliyefukuzwa atakuja lini kununua nondo moja iliyopanda mpaka elfu 30?
 
Halafu Ujinga wa hizi mada ni kwamba kila siku wanaofaa kuwa viongozi ni hao hao utadhani hakuna watanzania wengine!!
Watanzania wengine ni hao akina Mbowe ambao ni magaidi
 
Ni yupi unayempendekeza?

Sijasema mwinyi anafaa ila ni upuuzi sana kukosoa pendekezo la mtu anayefaa ukiwa huna pendekezo bora.
Mara nyingi anayefaa hapendekezwi na mtu, husukumwa na dhamira binafsi iliyojengwa kwenye karama ya uongozi. Kwa maana hiyo sina uhalali wa kupendekeza jina hapa, wakati ukifika watajitokeza tu. Kazi yetu ni kuwapima kwa historia na matendo yao.
 
Ikiwa wakati wa baba yake Loliondo ilizwa kwa waarabu kwa mkataba wa kijinga kabisa, Mzee alijimilikisha mali za umma, Ikulu ikageuzwa pango la walanguzi na wala rushwa na wakaigeuza sebule, n.k...kwa mwanae ndiyo itakuwa balaa kubwa!

Hana kabisa sifa za kuwa kiuongozi, kabebwa tu kama anavyotaka kubebwa Rizmoja!!
 
Mara nyingi anayefaa hapendekezwi na mtu, husukumwa na dhamira binafsi iliyojengwa kwenye karama ya uongozi. Kwa maana hiyo sina uhalali wa kupendekeza kina hapa, wakati ukifika watajitokeza tu. Kazi yetu ni kuwapima kwa historia na matendo yao.
Basi tusubiri.
 
Kama Mwinyi anafaa kuwa raisi basi Kingai, Jumanne na Mahita wao pia wanafaa sana, Nadhani umenielewa!!!!
 
Tayari anapaisha uchumi wa Zanzibar kwa kasi
 
Zanzibar ina wakazi wasiopinduka milioni 1 unataka ashindwe kutoa vitambulisho vya wafanyabiashara(machinga)?!!!

Usisahau Zanzibar ni nchi ya KITALII....umachinga unaingiza fedha za kigeni......
 
😍
 
Elitwege kaguswa....hajaamka TOKA AWAMU YA 5.....
 
Tayari anapaisha uchumi wa Zanzibar kwa kasi
Wakati unamlilia huyo Rais wa nchi jirani kuja kukutawala, umetoa na mawazo mbadala ya wapi kwa kumpeleka huyu Rais wako mbibi anaye kutawala sasa? Maana amesha jihakikishia mtakuwa wote tena ifikapo 2025 - 2030!
 
Anaweza kuwa rais mzuri Visiwani lakini JMT ikamshinda.

Peter’s Principle haijawahi kudanganya.
 
Wananchi walio wengi hawaridhiki na mnayoyafanya CCM,maana ushindi wa serikali zenu wote ni batili haupo kisheria upo kimapinduzi mmepindua uchaguzi mtasema na kupanga mengi lakini hakuna hata moja litakalowaletea faida.
Tume huru ya uchaguzi ndio suluhisho la maendeleo ,halafu wacheni kutisha watu eti Tumuogope Mwenyezi Mungu,wewe unaesema hayo humuogopi ? Mnatenda mema kwa msimu ,wakati wa Uchaguzi Mkuu Mungu wenu anaenda likizo mnaiba kura,mnauwa wapiga kura mnavuruga uchaguzi kwenye vituo,mnakimbia na Masanduku ya kura.
Malipo ni hapa hapa duniani ahera kunaenda hesabu tu.
 
Huo ushahidi wa kupindua uchaguzi kama unao kwa nini usiupeleke mahakamani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…