Rais Dkt. Samia atangaza ofa ya kuiona Taifa Stars bure dhidi ya Guinea

Rais Dkt. Samia atangaza ofa ya kuiona Taifa Stars bure dhidi ya Guinea

Mbona Watanzania tupo kama Ngiri tuna National Disaster inaendelea hapo Kariakoo hadi sasa watu bado wapo chini ya kifusi bado Serikali inatoa funds kulipia watu kuingia viwanjani wakati zinahitajika kwenye uwokozi? Ina maana hatujali wenzetu? Kwa ubinafsi huu tukivamiwa tutaweza kujilinda? Hapana kwa kweli.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza ofa ya kipekee kwa watanzania kuiona mechi ya timu ya taifa, Taifa Stars, bila malipo. Ofa hii inalenga kuongeza hamasa kwa wapenzi wa soka nchini katika kipindi hiki kigumu baada ya tukio la kusikitisha la kuporomoka kwa jengo katika eneo la Kariakoo.

Soma: Mwana FA: Ushindi wa Taifa Stars ni maalum kwa Rais Dkt. Samia Suluhu

Kwa upande wake, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeungana na Rais kutoa pole kwa waathirika wa tukio hilo pamoja na familia za waliopoteza maisha. Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Habari wa TFF, Cliford Marion Dimbo, akibainisha kuwa Shirikisho limeguswa sana na tukio hilo na linaendelea kusimama pamoja na watanzania wote wakati huu wa majonzi.

Wakati taifa likiendelea kuomboleza, hatua hizi zimeonekana kuwa faraja kwa wapenzi wa soka na wananchi kwa ujumla.

Hakuna kwenda Morocco!
 
Taifa Stars inaenda kutolewa mbele ya watu wengi
 
Back
Top Bottom