Rais Dr. Samia, Tanzania Inaweza Kuzalisha Petroli, Dizeli, Jet Fuel, Methanol, Amonia na Urea Kutoka Kwenye Gesi – Tutauza Haraka Sana

Tunaweza pia kununua kutoka kwa majirani wetu
 
Sasa wakizalisha wenyewe"automatic"miradi itakua ni ya serikali, wao kampuni zao za kuagiza zitapataje faida?
Kama ilivyo kwenye Migogoro ya Ardhi
Wasababishi na kuhodhi Ardhi za watu kiujanja ujanja ni wao
Unategemea tatizo litakwisha!!!
CCM ni janga
 
Hiyo LNG ya Msumbiji ni eneo lililokaribiana kwa karibu kabisa na iliyovumbuliwa upande wa Tz. Yawezekana ni mkondo mmoja. Sasa Tzi tuendelee kukodoa macho wenzetu Msumbiji wakiendelea kumaliza gas.
 
Tutakupa ukuu wa wilaya kwa mawazi haya mazuri
Mtampa ukuu wa Wilaya ili akakimbizane na wanaolangua korosho ki maghendo badala ya kumpeleka kwenye eneo lake husika?
 
Baada ya kusoma kuwa kuna wawekezaji wanafanya huo mchakato, we naye umeruka na andiko
 
Hiyo LNG ya Msumbiji ni eneo lililokaribiana kwa karibu kabisa na iliyovumbuliwa upande wa Tz. Yawezekana ni mkondo mmoja. Sasa Tzi tuendelee kukodoa macho wenzetu Msumbiji wakiendelea kumaliza gas.

Ndiyo, ni kweli mkuu gesi ya Msumbiji inatoka katika eneo lililo karibu sana na gesi iliyogunduliwa upande wa Tanzania. Mafuta na gesi mara nyingi hupatikana katika mikusanyiko ya miamba ya hifadhi (reservoirs) ambayo inaweza kuvuka mipaka ya kisiasa, na kuna uwezekano mkubwa gesi ya Msumbiji na Tanzania zinashiriki mkondo mmoja wa kijiolojia katika Bonde la Ruvuma na maeneo ya kina kirefu cha bahari.

Uhusiano wa Gesi ya Tanzania na Msumbiji

(i) Gesi ya Msumbiji inapatikana katika Bonde la Ruvuma, ambalo linaenea kutoka kusini mwa Tanzania hadi Msumbiji.
(ii) Eneo la gesi la Tanzania (Block 1, 2, na 4) lipo karibu kabisa na vitalu vya gesi vya Msumbiji, kama Rovuma Basin ambako ExxonMobil, Eni, na TotalEnergies wamewekeza katika LNG.
(iii) Kama muundo wa kijiolojia wa gesi unafanana, kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na chanzo kimoja cha gesi kilichoenea kati ya nchi hizi mbili.

Mradi wa LNG wa Msumbuji umeshaanza uzalishaji, huku gesi ikiwa inasafirishwa kwenda Ulaya na Asia.

Wamefanikiwa kuvutia wawekezaji wakubwa kama TotalEnergies, ExxonMobil, na Eni, na tayari wameanza kuuza gesi yao kimataifa.

Wamewekeza katika miundombinu ya LNG kwa haraka, licha ya changamoto za kiusalama zilizokuwepo Kaskazini mwa nchi yao.


Kwa upande wa Tanzania Mradi wa LNG Lindi bado upo kwenye hatua za mazungumzo, na bado hatujafikia Final Investment Decision (FID).

Sera za uwekezaji zimechukua muda mrefu kujadiliwa, ikiwemo makubaliano na makampuni ya gesi kama Shell na Equinor.

Msumbiji inauza gesi huku Tanzania tukisubiri LNG ianze – na kama gesi ni ya mkondo mmoja, kuna hatari ya Msumbiji kuitumia zaidi kabla Tanzania haijaanza.

Hapa inabidi serikali ifanye jambo tuanze Uzalishaji wa hiyo Gesi Sasa!

Ndio maana nimeshauri badala ya kusubiri LNG, Tanzania inaweza kuwekeza haraka kwenye miradi ya kuzalisha mafuta ya GTL, Methanol, na Mbolea (Amonia & Urea) kutoka gesi yetu. Hii itatusaidia kufaidika na gesi yetu kabla hatujachelewa.
 
Ni sawa na kusema huko serikalini hakuna wataalamu wa ‘oil and gas’ wanaotambua byproducts za crude hydrocarbons baada refinery processes.

Wakati huko shule wamefundishwa value chain nzima ya industry, commercial exploitation, large consumption markets, competition structure ya dunia na investments requirement kuanzia kwenye; upstream business, mid stream business and downstream business.

Na uwekezaji wenyewe ukikuta kampuni inashiriki katika value chain nzima ujue ni very big player na anasoko lenye demand kubwa ya bidhaa, vinginevyo washiriki wadogo lakini mitaji mikubwa utawakituta sehemu moja tu ya value. Hata hao big players hapa tunazungumzia the likes Chevron, Shell, BP, Total and the likes ambao japo private firms wana-market cap kubwa kushinda GDP ya Tanzania na wenyewe sio kila nchi wanayochimba hydrocarbon wanashiriki kwenye entire value chain.

Watu wanakuja kuwekeza kwa sababu zao wewe unakuja na hadithi zako wafanye nini cha ziada; halafu mnadhani hizo negotiations ni rahisi kweli. Au Shell, Equinor na Exxon Mobil; makampuni ambayo yapo kwenye top 10 ya industry hawajui kuhusu unitasation ya visima vya gas, waachie Msumbiji ibebe gas yote ya visima vyao vilivyo Tanzania.

Watanzania uwa tunapenda kutoa vitu kichwani na kudhani, that’s how things work in practice. Na hili ni tatizo kubwa mno Tanzania yaani unakuta mtu anaongea tu wengine wana nafasi serikalini kutwa kujiongelea tu vitu kutoka kichwani.
 
Hapa tunakumbushia na kuvutia wawekezaji katika taifa letu. Pengine makablasha yanaweza kufunguliwa sasa hii miradi ikatekelezwa.
 
of CNG is significantly lower.
Other advantages:
CNG vehicles are environmentally friendly.
CNG vehicles reduce the probability of a hazardous fire in case of a gas leak.
CNG vehicles are a versatile bi-fuel option, allowing owners to operate them on either CNG or petrol.
 
Nina mashaka jinsi msumbiji wanavyoishambulia pia uwezekano ni gas ya mkondo mmoja, na hatuna valve ya kufunga kwa chini, itakwisha sisi tukitoa tu macho! 😀😀, labda yule bibi wa mtwara atusaidie, Kuna hadithi aliwahi kuifunga gas kwa special valve!, kama ni kweli hadithi hii, basi Kuna watu wanavipawa!
 
Hapa tunakumbushia na kuvutia wawekezaji katika taifa letu. Pengine makablasha yanaweza kufunguliwa sasa hii miradi ikatekelezwa.
Huko Qatar kwenye reserve kubwa ya Gas sidhani kama magari yao mengi ni gas; hata hiyo petrochemical plant yao wamezindua kama miaka 10 nyuma na wameanza kuuzia dunia gas toka 1950’s.

Saudi Aramco na mtaji wake wote petrochemicals plants zake ni joint ventures, kwanini shida sio mtaji soko. Kuna watu huko unapotaka peleka tayari wameshaji establish sokoni, ku-penetrate unataka mtu ambae tayari ana market position.

Bado umeme wa kuendesha viwanda, kama umeme wa wananchi na viwanda vya kuzalishia juisi tu tabu; seuse umeme wa kiwanda cha petrochemical byproducts.

Unadhani kwanini Dangote ana mini power plant yake ya umeme. Uwa unajiandikiaga tu vitu with confidence.
 
Nchii hii sijui wajukuu zangu na vitukuu vya Mzee Wasira watakuta nini
 
Kwenye GTL plant tupata petroli, dizeli na Jet Fuel tunauza Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Kwenye Amonia plant tunapata mbolea tunauzia wakulima wote wa Afrika Mashariki.

Kwenye Methanol Plant Tunapata pia petroli tunauza Afrika Mashariki.

Mafuta yote niliyo yataja tutauzia kwenye vituo vya mafuta vipo tayari.

CNG inahitaji vituo vya kujaza gesi kila mkoa. Kituo kimoja ni huge investment.

LNG bado wawekezaji hawajafikia mwafaka wa kuanza utekelezaji.
 
Usipende kutoa kichwani kwako soma kwanza maelezo ya uwekezaji wenyewe na condition ya mwekezaji.

Watu awaendi nchi za watu kabla ya kufanya marketing research yao, hela yao itarudi vipi. Hiyo plant inauwezo wa kuzalisha 2500 barrel per day, matumizi ya Tanzania kwa siku ni kama 72000 barrel per day. Uwezo wa kiwanda kuzalisha mafuta kwa mahitaji ya Tanzania tu ni drop in the ocean, sasa hayo ya kuuza nchi jirani utatoa wapi.

By product nyingine wana mpango wa ku-export nje ya nchi, ndio maana unaelezwa watu wana masoko yao tayari. Wewe unakuja na story zako za kutoka kichwani.

👋
 
Ngoja tusubiri serikali inasemaje.
 
Achana na hizi ndoto Aisee! Hizi ni sawa na zile za kudai "tuchimbe madini mbugani kwani wanyama hawali madini"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…