Rais Dr. Samia, Tanzania Inaweza Kuzalisha Petroli, Dizeli, Jet Fuel, Methanol, Amonia na Urea Kutoka Kwenye Gesi – Tutauza Haraka Sana

Viongozi wa Tanzania wako kama wa Nigeria ambako vituo vya mafuta vimekauka huku viongozi ni mabilionia.
 
Viwanda huwa vipo kwa ukubwa fulani, na vinatofautiana kwa uwezo basi yatupasa tupate medium sized factory.,kuendana na soko! The later tunaweza Ku expand.
 
Unadhani hawajui hili,we unadhani wasomi wote na washauri wote wa rais hawalijui hili??!

Tatizo la nchi hii ni utashi wa kisiasa, political willing, labda atokee tena kiongozi mzalendo mwenye nia ya kujenga nchi kwadhati bila kuogopa masharti ya mabeberu na wazungu wa magharibi, world bank, imf na mabepari wa nje! Aje kiongozi asiyetumiwa kuwafurahisha mafisadi na wapigaji. Angalau Jpm alijitahidi na dunia iliona hilo licha ya mapungufu yake kwenye democrasia! Lakini hawa waliopo sasa utasubiri sana! Wao bora liende, nchi ina amani na utulivu, chama kinashinda kwa kishindo, wanatawala vizuri hiyo imetosha! Hayo mengine hayawahusu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…