Rais Erdogan wa Uturuki aiambia Israel sitisha vita. El Sisi wa Misri aiambia ifungue mpaka

Rais Erdogan wa Uturuki aiambia Israel sitisha vita. El Sisi wa Misri aiambia ifungue mpaka

Hali ndani ya Gaza imeelezwa kuwa ni balaa na machafuko huku majeshi ya Israel yakiwa yameingia kikamilifu eneo hilo na askari wa IDF wakipigana na watu mpaka kwenye kambi za wakimbizi.

Katika hali ya machafuko kiasi hicho raisi wa Uturuki ameiambia Israel isitishe vita mara moja. Raisi wa Misri kwa upande wake ameliambia taifa hilo lifungue mpaka wa Rafah misaada ipitie bila vizuizi.

Machafuko hayo yanatokea huku huduma zote muhimu jimboni humo zikiwa zimekatwa kwa zaidi ya wiki sasa.

Upande wa kaskazini mpakani na Lebanon urushaji wa makombora kutoka wanamgambo wa HizbuLah nao unaongezeka kila muda unavyosonga.
Kichapo ndio kimeanza rasmi. Si mlikuwa mnasema ameogopa kuingia. Sasa kwanza kakata mawasiliano na nje mpaka waombe po
 
Nimeona.Hamas wanaendelea kupambana pamoja na kuporomoshewa mabomu ya balaa.Nimeona pahala vifaru kadhaa vya Israel vimerudishwa nyumbani au vimesukumwa nyuma.
Angalia sasa na al arabia tv.
Uone kinachowakumba wanamgambo wa hamas ndani ya kaskazin mwa gaza
 
Siangalii hawa wapuuzi ,, nina shida ya maji , umeme , na sandano za chanjo za watoto wangu nije kuangaika na haya majitu walimuua Yesu wangu
Yesu alikua myahudi mwenzao,,,wewe anakuhusu nn???
Afu yesu aliuliwa na waitaliano sio wayahudi.
Wao wayahudi walimshitaki tu kwa warumi.
 
Yesu alikua myahudi mwenzao,,,wewe anakuhusu nn???
Afu yesu aliuliwa na waitaliano sio wayahudi.
Wao wayahudi walimshitaki tu kwa warumi.
Alishatakiwa na ma puppet wa warumi walioamini kaja kuchukua utawala wao ni kama Leo TU watu wanavyochongeana kwa mabosi wakiona nafasi zao zinatishiwa usalama
 
Wanaropoka ropoka hovyo tu na hakuna linalofanyika mpaka US aongee, hao UN wenyewe na kelele zao zote wame bounce. Nacheki Al jazeera hapa jana usiku israel huko Gaza katia kufuru ya kufa mtu unaambiwa haijawahi tokea tangu vita ianze.
Netanyahu alieleza wazi kuwa, mpaka hii vita iishe, Gaza itakuwa tofauti kabisa. Kwa kipigo alichojipanga kukitoa, ilibidi aombe usaidizi wa US na Uingereza wasogeze vyombo vita na silaha ili kuzuia mataifa jirani kujiunga moja kwa moja kwenye vita. Hii imempa Israel nafasi nzuri ya kumshughulikia Hamas. Hamas wamewaingiza raia wema katika hali ambayo hawakuwahi kuiona toka wazaliwe.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Wanaropoka ropoka hovyo tu na hakuna linalofanyika mpaka US aongee, hao UN wenyewe na kelele zao zote wame bounce. Nacheki Al jazeera hapa jana usiku israel huko Gaza katia kufuru ya kufa mtu unaambiwa haijawahi tokea tangu vita ianze.
Acha utani mkuu, napenda sikia habari kama hizi, ilikuaje jana?
 
Back
Top Bottom