ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
- Thread starter
- #21
Wenye miaka 60 Wana uzoefu mzuri kabisa wa koungozi,ni upunguani kusema hakuna walichofanya.Hapa Tanzania ccm tumewapa nchi miaka 60+ hakuna cha maana walichokifanya, kila kitu ni hovyo hovyo. Acha tujaribu watu wengine. Hata mke ukioa akakushinda utaoa mwingine, hoja kwamba huyo mwingine atakua wa hovyo kuliko wa sasa haina mashiko, ni hoja ya mke wa sasa kutaka aendelee kuwepo hivyo atatafta kila maneno ya vitisho kukutishia usiongeze mke mwingine.
SSH unaemsema ndio worst case kabisa. Huyu ndio yuko tayari hata auze nchi ili mradi awe rais, hana mipango yoyote na hakua na maandalizi yoyote, hajui afanye nini na nini asifanye, yeye ni kama anapokea maelekezo kutoka kwa watu wengine. Hajawahi kukaa atuambie anatamani nchi ielekee wapi, yeye kila kitu ni mkalitazame na hilo, kina nani wakalitazame?
Samia anachukua mikopo isiyo na kichwa wala miguu huko wb ama imf lakini hatuoni hiyo mikopo inafanya nini, unakopaje kulipa mishahara na matumizi ya serikali. Katika sehemu Tanzania tuliruka mkojo na kukanyaga mavi ni kwa ssh.
Huyo unaedai ni worst case sijui anauza kila kitu nadhani wewe ndio mpumbavu au huelewi maana ya sera za ubinafsishaji.
Haya mawazo Yako ni sehemu ya uthibitisho wa kukosa akili Wala maono na kwamba mtaishia kuwa kama hao failures wengine.
Samia ndio amefanya na anafanya yafuatayo
1.Amefanya Mageuzi ya Elimu kuanzia mtaalama Hadi ugharamiaji Elimu
2.Ndio Rais wa kwanza kuweka pesa kwenye sekta ya Kilimo kw upana wake ambayo Ina Wananchi wengi
3.Ndio Rais wa kwanza kuleta Mageuzi makubwa ya miundombinu Vijijini
4.Nsio Rais wa kwanza kumtua ndio mama kichwani Kwa vitendo
5.Ndio Rais wa kwanza kufanya Mageuzi makubwa ya Afya Nchini ikiwemo bima ya Afya Kwa wote.
6.Ndio Rais wa kwanza kuanzisha sera ya Nishati safi Kwa Wananchi inayolenga kuacha matumizi ya Nishati chafu.
7.Ndio Rais wa kwanza kuwekeza kwenye miundombinu ya sekta ya Michezo na hamasa Juu.
8.Ndio Rais wa kwanza kulipa msukumo sekta ya biashara, uwekezaji nk
Kiufupi Kuna mambo mengi ya msingi aliyofanya Kwa mda mfupi kuliko wale wengine waliokuwa na maneno mengi sana ila hakuna Cha maana