Rais Faye wa Senegal aanza visingizio baada ya kushindwa kutimiza ahadi alizotoa baada ya kuapa kuwa Rais. Awashutumu wapinzani kumkwamisha Bungeni

Rais Faye wa Senegal aanza visingizio baada ya kushindwa kutimiza ahadi alizotoa baada ya kuapa kuwa Rais. Awashutumu wapinzani kumkwamisha Bungeni

Hapa Tanzania ccm tumewapa nchi miaka 60+ hakuna cha maana walichokifanya, kila kitu ni hovyo hovyo. Acha tujaribu watu wengine. Hata mke ukioa akakushinda utaoa mwingine, hoja kwamba huyo mwingine atakua wa hovyo kuliko wa sasa haina mashiko, ni hoja ya mke wa sasa kutaka aendelee kuwepo hivyo atatafta kila maneno ya vitisho kukutishia usiongeze mke mwingine.

SSH unaemsema ndio worst case kabisa. Huyu ndio yuko tayari hata auze nchi ili mradi awe rais, hana mipango yoyote na hakua na maandalizi yoyote, hajui afanye nini na nini asifanye, yeye ni kama anapokea maelekezo kutoka kwa watu wengine. Hajawahi kukaa atuambie anatamani nchi ielekee wapi, yeye kila kitu ni mkalitazame na hilo, kina nani wakalitazame?

Samia anachukua mikopo isiyo na kichwa wala miguu huko wb ama imf lakini hatuoni hiyo mikopo inafanya nini, unakopaje kulipa mishahara na matumizi ya serikali. Katika sehemu Tanzania tuliruka mkojo na kukanyaga mavi ni kwa ssh.
Wenye miaka 60 Wana uzoefu mzuri kabisa wa koungozi,ni upunguani kusema hakuna walichofanya.

Huyo unaedai ni worst case sijui anauza kila kitu nadhani wewe ndio mpumbavu au huelewi maana ya sera za ubinafsishaji.

Haya mawazo Yako ni sehemu ya uthibitisho wa kukosa akili Wala maono na kwamba mtaishia kuwa kama hao failures wengine.

Samia ndio amefanya na anafanya yafuatayo
1.Amefanya Mageuzi ya Elimu kuanzia mtaalama Hadi ugharamiaji Elimu

2.Ndio Rais wa kwanza kuweka pesa kwenye sekta ya Kilimo kw upana wake ambayo Ina Wananchi wengi

3.Ndio Rais wa kwanza kuleta Mageuzi makubwa ya miundombinu Vijijini

4.Nsio Rais wa kwanza kumtua ndio mama kichwani Kwa vitendo

5.Ndio Rais wa kwanza kufanya Mageuzi makubwa ya Afya Nchini ikiwemo bima ya Afya Kwa wote.

6.Ndio Rais wa kwanza kuanzisha sera ya Nishati safi Kwa Wananchi inayolenga kuacha matumizi ya Nishati chafu.

7.Ndio Rais wa kwanza kuwekeza kwenye miundombinu ya sekta ya Michezo na hamasa Juu.

8.Ndio Rais wa kwanza kulipa msukumo sekta ya biashara, uwekezaji nk

Kiufupi Kuna mambo mengi ya msingi aliyofanya Kwa mda mfupi kuliko wale wengine waliokuwa na maneno mengi sana ila hakuna Cha maana
 
Give him time.
Kuna vyama viko madarakani miaka 63 Sasa wanafunzi bado wanakaa kwenye vumbi chini, mradi mdogo tu wa mwendokasi umeeashinda kuendesha. Sehemu kubwa ya Dar haina maji ya bomba. Ndani ya miezi 6 Senegal Wana mabasi ya mwendokasi ya umeme.
Ni kawaida MTU mfupi anaona Raha Sana kuona MTU mfupi kuliko yeye.
Huwezi kumpima kiongozi kwa miezi sita jamani, give him time.
Exaggeration politics.Kapo kengine kule Burkinafaso
 
Hayo malalamiko wanatoa kina nani?

Wa senegal wenyewe bado wana imani naye kubwa sana.

Bunge linamkwamisha bado wana hasira. Ila mwezi Dec si mbali atavunja bunge. Maana kwa sasa hawezi kuvunja mpaka bunge litimize miaka miwili tangu wachaguliwe.
Kwa Sasa hicho ndio Kisingizio ila nakuhakikishia hakuna kipya atafanya Kwa sababu Nchi sio Mali ya Rais
 
Miezi 6 baada ya Rais wa Senegal Basirou Diomaye wa Senegal na Waziri wake Mkuu Ousmane Sonko wameanza kuleta visingizio Kwa Kushindwa Kutimiza Baadhi ya ahadi zao walizodai watazitatua ndani ya siku 100.

Serikali ya bwana Faye inasingia Bunge Kumkwamisha ambalo lina Wabunge wengi wa Upinzani(zamani chama Tawala).👇👇

My Take: Naendelea kuwakumbusha watu kwamba ni mjinga tuu ndio ataamini kwamba Wapinzani ndio watawatatulia shida zao.

Nawaambiaga mara nyingi kwamba Wanasiasa wote ni matapeli na siasa ni kazi kama kazi zingine so unapotumia Rasilimali zako hadi.kuandamana kulala risasi uwe unapima kama unachopigania utanufaika

Kwa taarifa yenu tuu Wapinzani hata Hawa wa hapa Tanzania Wana maneno meengi yasiyo na msingi na Wala hawana njia za kutatua Changamoto zenu sana sana wanachotafuta ni madaraka tu.

Imetokea Ghana, Malawi, Kenya, Senegal,Zambia na nk, and won't be different Kwa Tanzania.

Kumbuka ukiitiwa fursa jua wewe ndio fursa. SSH Anatosha na chenji inabaki.

==========

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, anaonekana kupata ugumu kutumiza baadhi ya ahadi zake wakati wa Kampeni, miezi sita baada ya kuchaguliwa kuongoza taifa hilo la Afrika magharibi.

Serikali ya Faye ikiongozwa na waziri wake mkuu, Ousamne Sonko imeendelea kutuhumu bunge la taifa kwa kuwa kizingiti kwa sera za serikali yao, kwani idadi kubwa ya wabunge ni wa upinzani, Sonko akikataa kuwasilisha sera za serikali bungeni kwa misingi kwamba bunge hilo halitambui cheo chake.

Rais Faye amekuwa mstari wa mbele kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa washirika, akiwa mpatanishi kati ya muungano wa Ecowas na matifa ya Mali, Niger na Burkina Faso ambayo yalitangaza kuijiondoa katika muungano huo.

Hata hivyo wakosowaji wake wanadai ni hiyo mbinu ya kuepuka majukumu yake nyumbani katika hilo ambalo linashuhudia uhaba wa juu wa ukosefu wa ajira kwa vijana na deni la taifa.

Serikali ya Faye pia inatuhumiwa kwa kukosa kuizngatia usawa wa kijinsia katika teuzi mbalimbali za serikali.

Raia wengi wa Senegal aidha wanadai taifa lao halijasonga mbele tangu kufanyika kwa uchaguzi, wakati huu waziri mkuu Osmane Sonko akidai huenda bunge likavunjwa na rais Faye ili kutoa nafasi ya uchaguzi mpya wa wabunge.

Pia soma:Ushauri: Rais Mteule wa Senegal BD Faye Asikubali kuwa Kivuli na Kuendeshwa na Sonko.Kuna Watu Lazima Waishie Kuwa Ngazi
Umeanza,aidha ujinga au kuwehuka.Unajisahaulisha Magufuli alisemaje?Kwamba wakinzani wanachelewesha maendeleo.Nini tofauti na akina Sonko?Hata TANU/CCM walikuwa ni wakinzani wa wakoloni.Hawakuzukia hewani tu.Usijitoe ufahamu.
 
Wenye miaka 60 Wana uzoefu mzuri kabisa wa koungozi,ni upunguani kusema hakuna walichofanya.

Huyo unaedai ni worst case sijui anauza kila kitu nadhani wewe ndio mpumbavu au huelewi maana ya sera za ubinafsishaji.

Haya mawazo Yako ni sehemu ya uthibitisho wa kukosa akili Wala maono na kwamba mtaishia kuwa kama hao failures wengine.

Samia ndio amefanya na anafanya yafuatayo
1.Amefanya Mageuzi ya Elimu kuanzia mtaalama Hadi ugharamiaji Elimu

2.Ndio Rais wa kwanza kuweka pesa kwenye sekta ya Kilimo kw upana wake ambayo Ina Wananchi wengi

3.Ndio Rais wa kwanza kuleta Mageuzi makubwa ya miundombinu Vijijini

4.Nsio Rais wa kwanza kumtua ndio mama kichwani Kwa vitendo

5.Ndio Rais wa kwanza kufanya Mageuzi makubwa ya Afya Nchini ikiwemo bima ya Afya Kwa wote.

6.Ndio Rais wa kwanza kuanzisha sera ya Nishati safi Kwa Wananchi inayolenga kuacha matumizi ya Nishati chafu.

7.Ndio Rais wa kwanza kuwekeza kwenye miundombinu ya sekta ya Michezo na hamasa Juu.

8.Ndio Rais wa kwanza kulipa msukumo sekta ya biashara, uwekezaji nk

Kiufupi Kuna mambo mengi ya msingi aliyofanya Kwa mda mfupi kuliko wale wengine waliokuwa na maneno mengi sana ila hakuna Cha maana
Mbona amekuwa wa kwanza kufanya kila kitu! wengine walikuwa wanafanya nini?! Au ndio kusema walikuwa kama mapazia tu! Inasikitisha sana.
 
Mbona amekuwa wa kwanza kufanya kila kitu! wengine walikuwa wanafanya nini?! Au ndio kusema walikuwa kama mapazia tu! Inasikitisha sana.
Kila kitu kama kipi hicho ambacho wengine hawakufanya?
 
Back
Top Bottom