Rais hashtakiwi popote akiwa Madarakani na hata akitoka, kwanini anaapishwa?

Rais hashtakiwi popote akiwa Madarakani na hata akitoka, kwanini anaapishwa?

Duuhh... Mkuu umemaliza kuchangia!!?? Sababu zaidi ya 5................. Great Thinker!!!!!!!!!
Hahaha anatuzingua tu huyo. Hakuna sababu zaidi ya show,

Mtu yuko juu ya sheria zote, yeye hazimuhusu kwa namna yoyote ile.

Hashitakiwi, haojiwi, hata haulizwi na yeyote.

Anateua Jaji mkuu, Jaji kiongozi, mwanasheria mkuu wa serikali, waziri wa sheria.

Sasa nani wa kumuhoji na kwanini anaapa au kuapishwa, haijulikani.
 
Naomba kuelewa, nini maana ya kiapo cha rais aingiapo madarakani?

Hashitakiwi akiwa madarakani na hashitakiwi akitoka madarakani.

Kwanini anaapa au anaapishwa?

Kinga aliyonayo ni kubwa sioni sababu ya kiapo cha rais.


Anaapishwa ili akivunja katiba Bunge limuwajibishe.
 
Umewahi kujiuliza wale wadhamini ni wa kazi gani? Rais akivurunda umewahi kusikia wakiwajibishwa ili wadili na mtu waliempa udhamini??
 
Naomba kuelewa, nini maana ya kiapo cha rais aingiapo madarakani?

Hashitakiwi akiwa madarakani na hashitakiwi akitoka madarakani.

Kwanini anaapa au anaapishwa?

Kinga aliyonayo ni kubwa sioni sababu ya kiapo cha rais.


Anaapishwa mbele ya Mungu kwa kushika kitabu kitakatifu ili Mungu amsaidie kutenda majukumu yake sawasawa na kama akikiuka basi Mungu amkamate barabara kwasababu kikatiba hashitakiwi, Mungu tu ndiye anayeweza kumuadhibu. Tusubiri tuone adhabu atakayopewa yule "msema kweli ni mpenzi wa Mungu".🤣
 
Hata majaji wanaomuapisha anawateua yeye, kwa msingi huohuo hata kiapo anachokula mbele ya hao majaji/jaji ni UONGO uliitakasika.
Ni UONGO uliotakasika, aliwaambia majaji alipokuwa akiwakataza kujichukulia likizo bila ruhusa yake na kwenda wanakotaka, kwamba hawana ukubwa wowote na ni yeye huwateua na aliwaambia jukumu lao kubwa ni kuitetea serikali ndiyo inawalipa na asiyetaka na aondoke ataapisha mwingine.

Sasa kwa kauli hiyo nani anaweza kumbana Rais.

Kumbuka issue ya CAG analindwa kikatiba akafumua, akasema kama haridhiki na maamuzi aliyochukua aende mahakamani.

Kuna maana gani ya kufanya atakavyo kama kuna sheria?!
 
Back
Top Bottom