minyoo
JF-Expert Member
- May 25, 2013
- 23,510
- 22,529
Kiapo kile ni magumashi tu kwani hafuati katiba.Ni UONGO uliotakasika, aliwaambia majaji alipokuwa akiwakataza kujichukulia likizo bila ruhusa yake na kwenda wanakotaka, kwamba hawana ukubwa wowote na ni yeye huwateua na aliwaambia jukumu lao kubwa ni kuitetea serikali ndiyo inawalipa na asiyetaka na aondoke ataapisha mwingine.
Sasa kwa kauli hiyo nani anaweza kumbana Rais.
Kumbuka issue ya CAG analindwa kikatiba akafumua, akasema kama haridhiki na maamuzi aliyochukua aende mahakamani.
Kuna maana gani ya kufanya atakavyo kama kuna sheria?!