Kwa hiyo anaapa au kuapishwa kutii miiko ya kazi yake ambayo kimsingi akivurunda haojiwi na wala hashitakiwi?!
Sioni sababu ya kumuapisha aliye juu ya sheria
Niliandika na ninaandika tena, Malaika kumuapisha Mungu ni kuchezea muda, hawana mamlaka kumuwajibisha kwanini wamuapishe?!
Akivurunda kivipi?!
Ngoja tuchukue mfano wa kawaida, wa shule!!
Mwalimu anayeshindwa kufundisha na kupelekea wanafunzi kufanya vibaya, huyo anavurunda lakini pia huwezi kumshitaki kwa sababu kuvurunda kwake ni sehemu ya kazi yake kama incompetent teacher! Unachoweza kufanya ni kumtimua kazi!!
Kinyume chake, mwalimu huyo huyo akiwa anaiba mali za shule, anafanya mapenzi na wanafunzi, hayo si sehemu ya kazi yake kwahiyo unaweza kumtupa korokoroni!!
Tuje kwa Rais sasa!!
Rais ame-perform vibaya... uchumi umeanguka, ajira zimeshuka, huduma za jamii zipo hoe hae n.k! Hapo amevurunda kwahiyo huwezi kumshitaki!
Lakini Rais huyo akifanya jambo linaloenda kinyume na maadili ya viongozi wa umma, hapo anashitakika vizuri tu!! Nilikuwa na docs, sijui nimeitupia wapi! Ile doc inahorodhesha maadili y akiongozi wa umma!!
Kama bado yupo madarakani, and assuming bunge lipo huru and wabunge can react, kitakachofanyika ni rais kuwa impeached kwa sababu huwezi kumshitaki wakati yupo madarakani, na akishakuwa impeached, anafikishwa mahakamani kama kawaida!!
Unachotakiwa kufahamu ni kimoja tu: Je, tuhuma husika unadhani inatokana na moja ya majukumu yake au hapana!!! Kama ni moja ya majukumu yake ndipo hapo huwezi kumshitaki lakini kama alichofanya sio moja ya majukumu yake kama rais, na kwamba amevunja maadili ya umma, basi unamshitaki hata "wakati yupo madarakani"
Hii dhana kwamba huwezi kumshitaki wakati yupo madarakani haina maana hata akivunja sheria kama ilivyotajwa kwenye katiba basi ni LAZIMA asubiriwe amalize muda wake, la hasha! Tafsiri yake ni kwamba huwezi kumsimamisha mahakamani wakati akiwa bado rais... na logic hapo ipo wazi kwa sababu majaji wote kateua yeye!!
Ni kutokana na hilo ndo maana anakuwa impeached kwanza ndipo anafikishwa mahakmani!