Rais hashtakiwi popote akiwa Madarakani na hata akitoka, kwanini anaapishwa?

Duh!!
 
Naomba kuelewa, nini maana ya kiapo cha Rais aingiapo madarakani?

Hashitakiwi akiwa madarakani na hashitakiwi akitoka madarakani.

Kwanini anaapa au anaapishwa?

Kinga aliyonayo ni kubwa sioni sababu ya kiapo cha Rais.
Sidhani kama kile kiapo kinahusiana na mashtaka.

Huku mtaani tunashtakiwa kila uchwao lakini hakuna aliyewahi kuapa mimi Abdallah Twaibu sitakaa niuze bangi, Mungu nisaidie.

Na hakuna hakimu anasema Abdallah Twaibu nakufunga kwa kukiuka kiapo chako kwamba hutakaa uuze bangi milele.

Tusioapa tungekuwa hatufungwi.
 
Siku katiba ikibadilishwa atashitakiwa kama kawaida, mbona Omary Bashir kashitakiwa na wakati naye alikuwa MUNGU mtu?
 
Upo sahihi
 
Rais hashitakiwi kwa makosa yatakayojitokeza wakati akitimiza majukumu yake ya uraisi na si vinginevyo. Ikitokea akatoa maamuzi yaliyo kinyume cha sheria, akistaafu anaweza kushitakiwa. Sasa hapo itategemea serikali mpya iliyoko madarakani kama itaamua kumshughulikia kisheria
 
Wenyewe huapishana huko juu, na utudanganya kwamba kiapo ni kusema na kutenda kweli na haki chini ya kiapo, yani ni kiapo cha miiko ya uongozi.
Hata mahakamani zipo kesi watu huapishwa na zipo zetu hizi za kuhukumiana bila kujali na wakisisitiza ukate rufaa.

Wanasema huruhusiwi kusema uongo chini ya kiapo, huruhusiwi kutenda kosa chini ya kiapo lakini sijawahi kusikia mtu kashitakiwa kwa kuvunja miiko ya kiapo.

Formalities tu wanafanya kutupumbaza sisi, wakimaliza wanatucheka tunavyokuwa tumetoa macho kuangalia mtu kaapishwa.
 
Ipo haja ya wagombea urais wapimwe akili. Maana inawezekana wengine wana mafaili mirembe.
 
Naomba kuelewa, nini maana ya kiapo cha Rais aingiapo madarakani?

Hashitakiwi akiwa madarakani na hashitakiwi akitoka madarakani.

Kwanini anaapa au anaapishwa?

Kinga aliyonayo ni kubwa sioni sababu ya kiapo cha Rais.
Asante kwa swali fikirishi Nanye Go !!Sijawahi kujiuliza hivyo, kweli wewe ni Great Thinker
 
Naomba kuelewa, nini maana ya kiapo cha Rais aingiapo madarakani?

Hashitakiwi akiwa madarakani na hashitakiwi akitoka madarakani.

Kwanini anaapa au anaapishwa?

Kinga aliyonayo ni kubwa sioni sababu ya kiapo cha Rais.
Naamini kiapo hakina haja ndiyo maana huyu Rais wa sasa amaana navunja Katiba kama anavyojisikia.
 
Ukweli tunahitaji katiba mpya ili tuweke OPTION ya kumshtaki rais iwapo atavunja katiba! Rais anaapa kuilinda na kuifuata katiba katika utendaji wake, lakini katiba yetu haisemi achukuliwe hatua gani iwapo atatenda kinyume na kiapo chake na hapa ndipo dhana nzima ya kumuapisha rais wetu inakuwa ni useless!
 
Usanii tu! Hakuna haja ya kiapo! Mtu anakula kiapo halafu hatimizi kiapo na hakuna wa kumfanya chochote!

Siasa za bongo usanii mtupu!
Hio ni mojawapo ya mapungufu ya katiba yetu. Hali kadhli matokeo yanayompeleka raisi madarakani hayahojiwi popote kwa katiba tuliyonayo, ndio sababu wanafanya wanayotaka hawa watu.
 
Formality lazima aape...



Cc: mahondaw
Kwanini aape?!

Kesha kuwa Rais hata kabla ya kiapo, ukipewa cheti cha ushindi na NEC tayari wewe rais sasa nini sababu ya kuapa au kuapishwa?!

Kuapa au kuapishwa kuna formalize nini?
 
Siku katiba ikibadilishwa atashitakiwa kama kawaida, mbona Omary Bashir kashitakiwa na wakati naye alikuwa MUNGU mtu?
Okay, hiyo siku unaiona karibu au bado ni imani?!
 
Naomba kuelewa, nini maana ya kiapo cha Rais aingiapo madarakani?

Hashitakiwi akiwa madarakani na hashitakiwi akitoka madarakani.

Kwanini anaapa au anaapishwa?

Kinga aliyonayo ni kubwa sioni sababu ya kiapo cha Rais.
Mfano kiapo cha kutenda HAKI kuilinda Katiba vyote huwa havitimizi, mfano kuwabambikia kesi kesi uonevu unyanyasaji mateso kwa wapinzani sidhani kama vipo kwenye kiapo chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…