Rais Hussein Mwinyi amkaribisha Mamadou Sakho Ikulu. Ni nyota wa Crystal Palace na timu ya Taifa Ufaransa

Rais Hussein Mwinyi amkaribisha Mamadou Sakho Ikulu. Ni nyota wa Crystal Palace na timu ya Taifa Ufaransa

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Nyota huyo na familia yake yupo Zanzibar kwa mapumziko na familia yake.

Inasadikiwa ataanzisha kituo cha michezo cha watoto na kuendeleza soka la Zanzibar.

IMG_20210531_153137.jpg

"Nimefurahi kwa uwepo wako hapa Zanzibar na tutashirikiana katika kuendeleza soka la watoto"
IMG_20210531_155126.jpg
 
Huyu jamaa inaonekana Tanzania iko moyoni mwake tofauti na masupastaa wengine wa Afrika.
Kama sikosei hii ni mara yake ya pili inayotambulika kuja tanzania hata kama ni kwa mapumziko tu.
Au kaona fursa?
Sio fursa. Mimi tokea nimfahamu Sakho tokea akiwa PSG kabla ya kuhamia Liverpool 2013 yeye na mkewe Madja wamekuwa ni watu wanaojitolea sana katika jamii hasa Africa.

Hii ni kutokana na yeye mwenyewe kuwahi kusema kuwa hakupata privilege ya kuishi maisha mazuri akiwa mtoto hivyo kwakuwa Mungu amemjalia basi kile kidogo alichonacho anakitumia kuwainua watoto walio katika mazingira magumu.

Jamaa amefanya charity work nyingi sana Africa asee ni moja ya mastaa wa soka wanaojitoa sana namkubali sana kwa hilo. Yeye na Mane wanajitoa sana japo Mane ame base zaidi kwao Senegal ila Sakho amefanya sehemu nyingi sana.
 
Sio fursa. Mimi tokea nimfahamu Sakho tokea akiwa PSG kabla ya kuhamia Liverpool 2013 yeye na mkewe Madja wamekuwa ni watu wanaojitolea sana katika jamii hasa Africa.

Hii ni kutokana na yeye mwenyewe kuwahi kusema kuwa hakupata privilege ya kuishi maisha mazuri akiwa mtoto hivyo kwakuwa Mungu amamjalia basi kile kidogo alichonacho anakitumia kuwainua watoto walio katika mazingira magumu.

Jamaa amefanya charity work nyingi sana Africa asee ni moja ya mastaa wa soka wanaojitoa sana namkubali sana kwa hilo. Yeye na Mane wanajitoa sana japo Mane ame base zaidi kwao Senegal ila Sakho amafanya sehemu nyingi sana.
Nimekupata Kop.
Jamaa ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wa kiafrika katika kuinuana Waafrika.
Asante
 
Nimekupata Kop.
Jamaa ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wa kiafrika katika kuinuana Waafrika.
Asante
Yes ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wa Kiafrika japo yeye sio Mwafrika ni Mfaransa mwenye asili ya Afrika.
 
Huyu jamaa inaonekana Tanzania iko moyoni mwake tofauti na masupastaa wengine wa Afrika.
Kama sikosei hii ni mara yake ya pili inayotambulika kuja tanzania hata kama ni kwa mapumziko tu.
Au kaona fursa?
Wa West Africa wanaipenda sana Zanzibar, wengi wao ni Waislam na wanaamini Zanzibar ni sehemu safi ya wacha Mungu.
 
Habari kubwa hii mbali ya soka pia suala la utalii kuitangaza Zanzibar na Tanzania, serikali ya Zanzibar imefanya jambo la kuhakikisha msukumo wa utalii wa kila aina kupitia soka, fukwe safi za bahari n.k fursa zake zinaifikia dunia.
 
Back
Top Bottom