Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar, naomba nikukosoe kwa staha; usingilie Mahakama

Natilia mkazo kweli wasipewe dhamana...hasa hao wabakaji...na nyie kueni mnaojidai rais kalewa madaraka hamjielewi. Kwan ikitokea habar mtu kabaka kitoto cha miaka 2 mnaanza toa povu hapa...hakuna kutetea ujinga waache wasipate dhamana..
Hakuna anayetetea wabakaji, wafungwe hata milele ila taratibu za kisheria zitumike, kama sheria ni dhaifu taratibu za kuzirekebisha zifuatwe ili ziwe bora.
Hatari za sheria za mdomoni na papo kwa papo ni kwamba hujui kesho sheria ipi itafuata. Ukiacha kichwa kimoja kitunge sheria kuna hatari ya kuwepo sheria isiyotekelezeka.
 
Hivi na bangi inahesabika kwenye kundi la dawa za kulevya ?🙄
 
Natilia mkazo kweli wasipewe dhamana...hasa hao wabakaji...na nyie kueni mnaojidai rais kalewa madaraka hamjielewi. Kwan ikitokea habar mtu kabaka kitoto cha miaka 2 mnaanza toa povu hapa...hakuna kutetea ujinga waache wasipate dhamana..
subiri siku mama ako asingiziwe kubaka ndio utaelewa nini maan ya matamko ya hovyo. Uwepo wa mahakama ni kuthibitisha bila shaka na kuhukumu
 
Natilia mkazo kweli wasipewe dhamana...hasa hao wabakaji...na nyie kueni mnaojidai rais kalewa madaraka hamjielewi. Kwan ikitokea habar mtu kabaka kitoto cha miaka 2 mnaanza toa povu hapa...hakuna kutetea ujinga waache wasipate dhamana..
Unaandika kama wewe hauishi kwenye hii dunia.angalia sio hadi yakukute ya walimwengu ndo ujue wenzako wanaposisitiza umuhimu wakuheshimu sheria za nchi na vyombo vyake ni muhimu.Aliye salama duniani ni marehemu peke yake.
 
Ni mwendawazimu peke yake ndiye anaweza kutegemea hawa viongozi ambao hawana kibali cha wananchi kama Mwinyi kuacha kuingilia na kuiweka mfukoni mihimili mingine.

Hata kama mimi ningekuwa Mwinyi as long as sina kibali cha wananchi katika urais wangu lazima ningevuruga mihimili mingine kwa maslahi yangu binafsi ya kuweza kutawala uma bila bugudha kutoka kwa niliowapora mamlaka.
 
Mie sikubaliani na hoja ya kuondoa dhamana, naamini kosa likiwa halina dhamana linatumika mara nyingi kinyume na malengo. Kama ulivyosema ulinzi uimarishwe na wote walio na hatia iachwe mahakama ifanye kazi yake.

Ukiondoa dhamana basi itakuwa sawa na iyo ya uhujumu uchumi na ugaidi, wanasiasa watakuwa wanabambikizia kesi mahasimu wao wanasota magereza.
 
Natilia mkazo kweli wasipewe dhamana...hasa hao wabakaji...na nyie kueni mnaojidai rais kalewa madaraka hamjielewi. Kwan ikitokea habar mtu kabaka kitoto cha miaka 2 mnaanza toa povu hapa...hakuna kutetea ujinga waache wasipate dhamana..
Halafu wanawekewa dhamana wanarudi mitaani kurejea makosa yale yale. Na hasa wabakaji watoto wanafichwa na kutetewa na ndugu wa karibu.

Kwa kweli inauma sana kuona mtoto mdogo wa miaka labda 6 au 8 amebakwa, mbakaji anatembea mtaani kwa kujitapa kabisa halafu kesi inaishia hivi hivi.
 
Rais Dk. Mwinyi yuko sahihi. Tusichezee na wauza dawa za kulevya. Hawa ni watu hatari. Wanaua nguvu kazi ya Taifa, wanazunguusha fedha haramu na mtandao wao ni hatari. Pili, udhalilishaji huacha makovu makubwa ya kisaikolojia kwa waliotendewa.

Adhabu hutolewa kutokana na aina, mazingira ya uhalifu na trend . Kama wanapewa dhamana halafu trend inaonyesha kuongezeka kwa kasi kwa matukio yeye akiwa Rais anayeongoza serikali, lazima akumbushe umuhimu wa kusimamia sheria.
 
hivi unajua maumivu ya kutuhumiwa, ukakosa dhamana miaka 2 halafu ukashinda kesi au mashtaka wakajitoa kwenye kesi???
Nadhani ame over-react kwasababu amewahurumia wanaoharibika kuwa mateja na wanaobakwa. Tuangalie nia yake zaidi.
 
Natilia mkazo kweli wasipewe dhamana...hasa hao wabakaji...na nyie kueni mnaojidai rais kalewa madaraka hamjielewi. Kwan ikitokea habar mtu kabaka kitoto cha miaka 2 mnaanza toa povu hapa...hakuna kutetea ujinga waache wasipate dhamana..
NANI SASA, UNAWAJUA WATUHUMIWA?.. MAANA YA MTUHUMIWA UNAIJUA?
 
SHERIA INARUHUSU DHAMANA KWA MTU.... AU UNAONGELEA SHERIA IP?

PUMBA HII MZEE
 
Nchi ngumu hii mnalalamika asubuhi hadi jioni hata kwa jambo jema
 
Siasa nyingi kwenye issues za madawa ya kulevya zinaangamiza taifa letu, tuendelee tu kujidanganya na eti sheria; unadhani kuna madoni wa UNGA anaweza KUFUNGWA na mahakama zetu? Kujidanganya tu. Binafsi nimeupenda msimamo wa Dr. Mwinyi
 
Nadhani ame over-react kwasababu amewahurumia wanaoharibika kuwa mateja na wanaobakwa. Tuangalie nia yake zaidi.
Inshu sio nia ya dhati, haya madaraka ndio yametuumiza sana awamu ya tano, yaani rais akitamka tu tayari inakuwa ni sheria hata kama inakinzana na katiba!!!kama amechukizwa sana basi waifanye iwe sheria tu,
 
Wauza ngada bwana hawataki kusikia mtu anapiga vita madawa ya kulevya
 
Inabidi sasa labda Mh. rais Mwinyi afanye utaratibu kama ule wa kipindi cha Nyerere, kwamba ilikuwa mtu akikamatwa amekula rushwa, tayari sheria ilikuwa inasema aina ya adhabu atakayopata na si hakimu aliyekuwa anaamua aina ya adhabu.

Sheria ilikuwa inasema kwanza anachapwa viboko 12 wakati wa kuingia, halafu tena 12 wakati wa kutoka ili akamwonyeshe mkewe..... Yaani waliweka adhabu tayari kwa mtu anayekula rushwa, na si hakimu aliyekuwa anaamua aina ya adhabu.

Mh. Rais inabidi sasa aanze kufikiri katika mkondo huu wa Nyerere, kwamba itungwe sheria inayosema kuwa watu wenye makosa ya aina hii hawatakuwa na dhamana!
 
Rais Mwinyi , KWA kweli binafsi nimeshangaa kauli yake , wenda na majirani zake wanashangaa kauli yake,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…