safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Kauli yenyewe hii hapa chini 👇👇👇Kwa kauli hii
Hii kauli imesema "YEYOTE ATAKAYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA.."yoyote atakae kamatwa kwa kosa la madawa ya kulevya
mkuu hii kauli maana yake atakayekamatwa kwa madaya ya kulevya eidha
Awe anatumia yeye katika mkoa huo
anasambaza yeye katika mkoa huo
Kwa hiyo kauli ya mh raisi imemgusa kila annaehusika na madawa na wala hakusema "yeyote atakayekamatwa akitumia madawa" angelisema hivi ulikuwa na haki ya kulalamika lakini hakusema hivyo.
Kauli ya Raisi ni kauli ya jumla wewe umeifanya ni kauli mahususi na umeuweka umahususi huo ili umkosoe sio sawa.
Itakiwa useme kwa nini hajasema au hajatoa tamko la kuongeza nguvu ili kubaini mtandao.Kwanini asiongeze nguvu kwenye vyombo vya ulinzi wakabaini mtandao nakuufyeka?
Kwa sababu huna uhakika kwamba hajaongeza nguvu isipokuwa uhakika wako ni kuwa hajasema kama ameongeza nguvu.
Na sio kila anachofanya raisi eti akiseme ili wewe ujue kwamba kaongeza nguvu,ikitokea atasema kama haikutokea sababu hatosema.
Lakini pia Vyombo vya ulinzi vinafanya operesheni zake kama kawaida ili kupambana na mambo hayo wewe huwezi kujua wanatumia njia gani kuomgeza nguvu.
Pengine njia wanazotumia kuongeza nguvu ni njia ambazo hazitakiwi kutangazwa yaani zisijulikane.
Hivi majuzi pale airpot yikamatwa madawa ya kulevya na walinzi.Hapo bado unajiuliza madawa yanaingiaje?
Hakukamata raisi,alafu unauliza yanaingiaje wakati kazi inafanyika na wenye dhamana kwa kadri ya uwezo wao.