Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Mkakati Kuelekea Bunge la katiba Maana Kura ya Mbatia washaikosa.
 
Nimekubali baraza la mawaziri litavunjwa na huyu mama namtabiria kukwaa uwaziri muhimu hasa wa Elimu. Na pia namtabilia cheo kikubwa 2015.
 
Dalili ya mvua ni mawingu na mwenye macho haambiwi tazama.

Kwa kuzingatia hiyo misemo miwili,kuna kila dalili ya kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na baraza jipya kutangazwa hivi karibuni.e Ninachokiano ni kuwa waziri mkuu wa sasa atawekwa kando na nafasi yake yake kuchukuliwa na huyu mama X.Pamoja na sababu zingine ni kumuandaa huyu mama kuwa mgombea uraisi kupitia chama tawala.Huyu mama inaonekana ni kipenzi cha Raisi wetu na huu uteuzi wake si bure.

Hata hivyo,huenda katiba hairuhusu mbunge wa kuteuliwa kuwa waziri mkuu lakini anaweza kupewa wizara nyeti kwa sababu hiyo tu.

Ikumbukwe hata waziri mkuu wa sasa ameonekana kupwaya na hivyo ataondoka sambamba na mawaziri wengine a.k.a mawaziri mizigo.

Tusubiri tuone.
 
sidhani kama jk anampango wa kumpiga chini pinda
 
Kama unamzungumzia Migiro haiwezekani kwa sababu siyo mbunge wa kutoka kwenye jimbo na hajapigiwa kura na wananchi katiba hairuhusu.
 
Waziri mkuu huteuliwa miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa na wananchi si wakuteuliwa na raisi!
 
umekosea kutabiri mkuu,utabiri wangu ni kuwa mh Daktari Asha Rose Migiro anaenda kumpokonya daktari Kawa mbwa ubosi wa wizara ya elimù! just wait and see
 
Kuteuliwa na Mh. Rais ni heshima kubwa sana kwa yeyote yule.

Tuache mizaa na kebehi,hakika hili ni jambo jema si tu kwa wanachama

wa chama tawala bali ni ishara njema ya mabadiliko ya juu serikalini.

Hongera Mama Migiro na sote tumtakie kila la kheli katika kutekeleza

jukumu hilo.
 
Rais Kikwete amemteua Dr Asha-rose Mtengeti Migiro kuwa mbunge wa bunge la Tanzania kuanzia jana Jumatatu.

Uteuzi umetangazwa rasmi jioni hii Ikulu ya Dar es salaam
Anataka kutoa mzigo mdogo na kuweka mzigo mkubwa zaidi.Yaani huo utakuwa mzigo wakulemea
 
Back
Top Bottom