Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Kwa mema gani aliyoifanyia Tanzania ambayo ni ya kipekee (Special merits) kwamba anatakiwa kupewa ubunge wa bure tuongezea mzigo mzito walipa kodi. Amerudhishwa UN for under performance sisi tunamzawadia ubunge wa bure. Hii nchi itatuchukua miaka mingi mno kuendelea

Nimetamani kukutukana tusi la wauza miwili Yao kwa bei chee lkn nimenyuuti.
Ila silazma kupinga kila jambo huyo alikua waziri wa mambo ya nje na sasa kiongozi mwandamizi ktk ccm Hilo halitoshi kuteuliwa.
 
From 2015 , anataka command zitokee bagamoyooooo..
mazuzu tanzania hawapo....
 
CCM wana vituko!! huyu tu hajawahi kusimama akiwa mgombea mbele za wananchi!!!! anabebwabebwa tu!!
 
Nimetamani kukutukana tusi la wauza miwili Yao kwa bei chee lkn nimenyuuti.
Ila silazma kupinga kila jambo huyo alikua waziri wa mambo ya nje na sasa kiongozi mwandamizi ktk ccm Hilo halitoshi kuteuliwa.
Kuwa waziri TZ kwani tatizo?hata mwehu anaweza kupewa wizara nyeti
 
Rais Kikwete amemteua Dr Asha-rose Mtengeti Migiro kuwa mbunge wa bunge la Tanzania kuanzia jana Jumatatu.

Uteuzi umetangazwa rasmi jioni hii Ikulu ya Dar es salaam

Naona anaongeza wajumbe wa Bunge la katiba teh teh!!. Huyu lazima kuna jambo linakwenda kufanyika.
 
Hovyo hovyoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!
 
Nilishahisi tu kuna kitu katika haya mambo,2015 maandalizi yanapamba moto,ndo maana anauzwa kwa wananchi
 
Hukujua Mkuu?. Mheshimiwa Kwenye dini hafanyi kosa,nenda kw a wakuu wa wilaya,mkoa wakurugenzi,nenda hata UDOM uta shangaa kuona salamaleku zilivyo jaa

Magamba hawaoni kundure
 
Huyu mama ccm wanambeba beba tu ili aonekane anaweza lakini kiukweli hana jipya hata wanawake wenzake hawana chochote cha kujivunia ama kujifunza.

Alichokifanya huko UN ni kuiaibisha nchi yetu na kuionyesha dunia kwamba tuna baadhi ya wasomi ambao uwezo wao unaonekana kwenye makaratsi tu lakini katika utendaji ni zeeero.

Mwita minakumbuka BanK Mon alikuwahi kutoa positive comments kwa huyu mama juu ya performance yake , sasa hizi za kushindwa kazi , kuaibisha Taifa kipimo gani kilichotumika kujaji? au ndio mchezo ule ule wa Siasa kwamba ukimsifia mpinzania wako ni hatari. Pia nani nani anaweza kutupatia KPIs za mama Rose Migiro akiwa UN ?
 
Mwishoni mwa mwaka 2012 Gazeti la Serikali (HabariLeo) liliwahi chapisha habari zifuatazo:

Migiro kurudi kufundisha UDSM

ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro amesema hatajishughulisha na siasa kwa sasa na anarejea kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kuwasili nchini saa tisa alasiri jana akitoka New York, Marekani, Dk Migiro alisema maadili na masharti ya kazi aliyokuwa akifanya hayamruhusu kuwania nafasi yoyote ndani ya chama cha siasa kwa muda.

“Pamoja na kuwa nimemaliza muda wangu wa uongozi, naendelea kuongozwa na maadili ya kazi ambayo kama mtu ameshika wadhifa wa juu kama wangu, hatakiwi kujihusisha na siasa za chama chochote kwa kipindi fulani.

Aliongeza kuwa: “Lakini pia siku mbili kabla muda wangu haujaisha, Katibu Mkuu (Ban Ki-moon) amenipa heshima na kuniteua kuwa mjumbe wa Ukimwi Afrika na kazi hiyo pia itakuwa na maadili ambayo yataniongoza.”

Alipoulizwa kama ana mpango wa kutangaza kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2015, Dk Migiro alisema: “Ninachojua nchi ina Rais, lakini pia kiu yangu ni kurejea nyumbani kuwa mke, mama, shangazi, dada na mwalimu tena.”

Alisema leo anakwenda kuripoti kwa mwajiri wake Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kitivo cha Sheria alikokuwa akifanya kazi kabla ya kupewa likizo bila malipo.

“Mwajiri wangu tayari yuko hapa (uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere) anataka kuhakikisha siendi kulia wala kushoto. Narejea kwa mwajiri wangu ambaye alinipa likizo bila malipo na mkataba ulikuwa ni wa miaka mitano, hivyo narejea Kitivo cha Sheria kuwa mwalimu.”

Kuhusu Katiba, Dk Migiro alisema amefurahishwa na hatua ya Serikali kutaka kuimarisha Katiba yake, jambo ambalo linaimarisha utawala wa sheria aliokuwa akisimamia akiwa UN na kuwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kujadili mambo ya msingi yatakayoongoza nchi.

Aidha, Migiro alitaka viongozi wa nchi za Afrika kuhakikisha wanaimarisha amani ili kufanya wananchi waishi katika nchi zao na kama watataka kuondoka iwe ni kwa hiari yao.

Pamoja na kusikitishwa na raia wa Somalia waliokufa kutokana na kukosa hewa wakiwa njiani kutoroka nchini kwao, Migiro alisema UN imefanikiwa kurejesha amani katika nchi mbalimbali ikiwa ni tofauti na hali ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

Migiro ambaye wakati akiteuliwa nafasi aliyomaliza kuitumikia alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Mwakilishi Mkazi wa UN nchini Dk Alberic Kocou na aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela. Pia familia yake, ndugu na jamaa ambao waliimba wimbo wa kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa jana, Dk Migiro ambaye ni mwanasheria, alizaliwa Julai 9, 1956 Songea mkoani Ruvuma

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom