Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Rose mna hati miliki nalo? si Waridi hilo? Mbona Waislaam wengi sana wanaitwa Warda = Rose.

Hivi bila kuleta viroja hamuoni uroda?


Mambo ya hati miliki unajua wewe mdini. yeye mwenyewe hanashida anajiita Asha-Rose. Kwanza hata jina Asha linatumiwa na wakristo na wasiokuwa na dini. Nazani hata jina lenyewe ni la kihindi au dini ya hindu kabisa
 
Kwa mema gani aliyoifanyia Tanzania ambayo ni ya kipekee (Special merits) kwamba anatakiwa kupewa ubunge wa bure tuongezea mzigo mzito walipa kodi. Amerudhishwa UN for under performance sisi tunamzawadia ubunge wa bure. Hii nchi itatuchukua miaka mingi mno kuendelea


Anapiga ngoma na makofi ya nguvu huko vijijini na kina Nape, Kinana, kwenye misafara ya kinafki isiyokuwa na tija na taifa bali chama cha wizi. Sasa iliyobaki ni kusinzia tu bungeni maanake alichoka sana kutembea na kujifanya kuwa anawapenda watanzania wachovu kumbe ni danganya toto tu. Tutamuona anavyolala bungeni.
 
Kashindwa UN, linakwenda Idodomie, tuone kama 2015 atapata ulaji wowote?
 
Maisha wa tz yanapanda tena!! Ili kufiti mushara wa mgiro tutaisha jamani huyu KIWETE Ngoja niombe maombi SEA atoke Jera
 
Katiba inampa rais uwezo wa kuteua wabunge wangapi? na mpaka sasa Kikwete akiwa 65% ya kipindi chake keshatetua wabunge wangapi? Hivi ni kweli kuwa serikali ya Tanzania inanundwa na mihimili mitatu ya mahakama, bunge na ofisi ya rais?
 
Nilitegemea kitu kama iki...kifuatacho utasikia Mgombea wa urais CCM lazima awe mwanamama!!
 
Mambo ya hati miliki unajua wewe mdini. yeye mwenyewe hanashida anajiita Asha-Rose. Kwanza hata jina Asha linatumiwa na wakristo na wasiokuwa na dini. Nazani hata jina lenyewe ni la kihindi au dini ya hindu kabisa

Umemaliza? kama tayari, sasa nenda kawaulize niliowajibu kwanini walileta hiyo point ya jina, ukipata jibu, njoo ulete hoja yako. Umedandia treni kwa mbele
 
CCM kuwa kurundikiana vyeo hamjambo!! -
 
ndo gear ya kuwaenguwa wagombea urais wanamme wote wa magamba. matumbo moto
 
mbona vijana wapo wengi? halafu utasikia ooho. magamba tunajali vijana, yaani wanarundikiana mavyeo tu
 
Hata chadema kwa kuwarundikia vyeo hamjambo kweli kweli mwangalie John Mnyika a.k.a Mzee wa Evening Class!

Ana vyeo Tisa yaani 9 ndani ya chadema! Kila mtu analijua Hilo na alishawahi kulalamika kwa kuzidiwa na vyeo! Vingine vilikuwa vinapwaya!
 
Hii mara ya pili anapata ubunge bure bure kwa saab sidhani kama alivyokuwa waziri mara ya kwanza alikuwa ame earn ubunge.
 
Maandalizi ya URAISI-2015 kwa hoja ileile kuwa safari hii "tumpe mwanamke" kama ilivyokuwa kwa spika wa Bunge.
Swali ni je,Watanzani wako tayari kuongozwa na Raisi mwanamke kwa kigezo hicho hicho cha "safari hii tumpe mwanamke"....???

Eee Mungu wa Mbingu na Nchi tuwezeshe tupate Katiba inayotokana na sisi Wanaichi na si itokanayo na utashi wa vyama vya siasa,maana bila hivyo kiongozi wa Nchi atakuwa anafanya vyovyote vile anavyotaka na haya ni majanga kwa Taifa la Tanzania.................!!!!!!!!

Mwanamke awe Rais!! Mungu anakataa kabisaaaa!
 
Hivi nchi hii haina watu wenye fikra mpya za kuitoa kwenye hili lindi la umaskini zaidi ya haya MAKAPI?

Mbona kuna watu wengi tu wazuri wanaoweza kutuongozea nchi yetu?Au mnahofia hawatalinda maovu mliokwisha fanya?

Watu kibao wanamaliza vyuo kila kukicha halafu mnarudisha yaleyale masalia!!!?

AMKA WATANZANIA MNAIBIWA MCHANA KWEUPE!
 
Kuna dot.........fulani na mizunguko yake ya Chama, haya tuone kamati kuu itaamua mgombea awe mwanamke kama walivyo fanya kwa spika wa bunge. Tusubiri tuone

itakua njia rahisi kabisa kwa CDM.
 
Back
Top Bottom