Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Rais Jakaya Kikwete amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa mbunge

Nilishahisi tu kuna kitu katika haya mambo,2015 maandalizi yanapamba moto,ndo maana anauzwa kwa wananchi

mbona mtu wenyewe hauziki.siasa hawezi anabebwabebwa lakini bado hatoshi arudi tu akafundishe tena wakimpa uwaziri ndio wataharibu kabisa, udhaifu wake sasa watu wataufuatilia kuliko wakati wowote
 
Hana tofauti na Zakia Meghji

Katiba mpya itoe haya madudu!Viti maalum au sijui vya upendeleo unaenda mtetea nani?

Huyu Dr Asha Mtengeti hajawahi jieleza na kuomba apigiwe kura ktk uchaguzi wowote ule duniani yy kuteuliwa tuuuuuuu!!

2015 MBUNGE iwe lzm apatikane kwa kupigiwa kura!
 
Sasa Lowasa na Sita kazi kweni, 2015 ccm inapitisha sheria mpya kwa mgombea uraisi kwa tiketi ya ccm sharti awe na jinsia ya kike, qualifications zingine zitafuata baada ya.
 
Katiba mpya itoe haya madudu!Viti maalum au sijui vya upendeleo unaenda mtetea nani?

Huyu Dr Asha Mtengeti hajawahi jieleza na kuomba apigiwe kura ktk uchaguzi wowote ule duniani yy kuteuliwa tuuuuuuu!!

2015 MBUNGE iwe lzm apatikane kwa kupigiwa kura!

Mkuu, una ugomvi na James Mbatia?
 
Hii inatisha hasa kwa kuzingatia kuwa kuna waziri mmoja inasemekana yupo "mahututi" katika hospitali moja huko Afrika Kusini.
 
Sasa Lowasa na Sita kazi kweni, 2015 ccm inapitisha sheria mpya kwa mgombea uraisi kwa tiketi ya ccm sharti awe na jinsia ya kike, qualifications zingine zitafuata baada ya.
hii haiwahusu hao uliowataja bali inakuhusu na wewe, kama kweli aliunderperform UN basi huenda akiwekwa Magogoni basi itakuwa hivyo hivyo na matokeo yake tutayabeba sote kama taifa. Tz bado sana.

 
Watu wale wale,mambo yale yale...kanyaga twende
Mie naona anaenda kuongeza kura za ndiyo maana kwa vyovyote vile hawezi kuipinga serikali hata kama inavurunda same as CCM.
Tuonee labda patakuwepo na mabadiliko.......
 
Huu ndiyo ukweli Ban Ki-moon alivyomuona Dr. Asha Rose Migiro na wala siyo porojo za mabloger
According to Ban Ki-moon, "She is a highly respected leader who has championed the cause of developing countries over the years..." He also said that "Through her distinguished service in diverse areas, she has displayed outstanding management skills with wide experience and expertise in socio-economic affairs and development issues."
[SUP][11][/SUP] According to The New York Times
 
una ushahidi au ndio ule wivu wa kipuuzi. Wewe jobless unampondea mtu kama migiro ni kichekesho.
Jobless ni wewe unaeshinda lumumba kusubiri buku Saba kwa kila thread unayochangia. Kama ail perform better kwa nini baraza la usalama UN hawakumwongezea mkataba? Ni kwa sbb ni kilaza kazoo a kufanya mambo kimagambamagamba wakati we zako pale alikuwa wanakwenda kwa supersonic speed. Gamba we.
 
Huyu mama WAZUNGU walimuona KILAZA. Sisi tunamuona anafaa!!!!! UN kulimshinda. Hiyo ndo tofauti ya sisi na wazungu. Heri angemuteua Shonza kuliko Migiro. HELA ZA UN NAONA KAMALIZA.

Wewe acha kuwa mtumwa wa fikra.
Kwa hiyo wazungu ndio wamekuwa miungu yako? wakiona kitu hakifai basi na kwako hakifai? kwa hiyo wewe ubongo wako uko controlled na wazungu??
 
Centre for Political Intelligence
Why Dr. Migiro lost her UN job

Posted on July 11, 2012 by VoxMedia

Barely a week after the immediate former Deputy Secretary-General, Dr. Asha Rose Migiro returned to Tanzania after serving a five-year term at the helm of the world body, sources within the UN have hinted that poor performance and failure to fit “in the diverse and complicated body” were some of the reasons she was refused a contract renewal.
“The position of the Deputy Secretary-General is complicated and demanding; it requires somebody who is experienced to efficiently run the Secretariat. Her biggest challenge was not understanding the politics at the world body and creating alliances,” the source told Vox Media in a telephone conversation.
Dr. Migiro is understood to have approached the African Group, comprising 28 percent of all UN members, to ask for help in lobbying for her re-appointment, but her quest was rejected.
“She wasn’t popular amongst diplomats; so nobody listened to her. You should also recall that her appointment was widely criticized.”
In Dar es Salaam, a former senior ruling party secretariat member who worked closely with her in the same team before she assumed the UN post said her appointment was influenced by her personal relationship with President Jakaya Kikwete.
It is understood that President Kikwete and UN Secretary-General Ban Ki-moon cultivated a close relationship when serving as foreign ministers for their respective governments.
When it came for Ban Ki-moon to canvass for votes toward his UN bid, Tanzania’s vote was predominant; Dr. Migiro was apparently battered with Kikwete’s vote.
But when Ban Ki-Moon recently decided to review his entire team in a bid to control growing criticism of his team, Dr. Migiro had to go for “poor performance and lack of experience required of staff with the top UN mandate.”

This entry was posted in Analysis. Bookmark the permalink.

According to The New York Times, this was a fulfillment of his promise to pick a woman from the developing world for the post of Deputy Secretary-General.[SUP][9][/SUP] The UN News Centre noted that Migiro and Ban had worked together while they were foreign ministers of their respective countries.[SUP][6][/SUP]
Huu ndiyo ukweli wenyewe siyo porojo za Vox media blog ya kibongo.
 
Hahaha....

Na kama atamteua kwenye cabinet reshuffle ni lazima aonyeshe ana utaalamu exceptional ambao hauwezi kupatikana ndani ya wabunge wa CCM.

Next time atampa Kinana Ubunge kuelekea general Election


Kesho Headline utaskia, Migiro Aula....

Nawashangaa watu wanaolaumu JK kumteua mtu aliye-underperfom UN kuwa mbunge wakati alimteua mtu aliye-underperfom UNHABITAT kuwa Minister

kwakua nafas 10 za rais kuteua wabunge kikatiba hazijaisha,basi atakuteua na ww uliye over perfom kule UN!!!!!
 
Ficha upumbavu wako, mbona Ban Kimoon bado yupo?

Asha ame-under perfom UN na wala si vinginevyo, ni sawa na Lowasa kuitwa Waziri mkuu mstaafu na waliopigwa chini ubunge kuitwa wabunge wastaafu.

Acha uzuzu wako wewe zezeta,
Kwa hiyo kipimo chako ni kwamba kwa Ban Kimun bado yupo UN ndio ameperform na kwa vile Dr. Migiro hayupo UN ndio ame-under perform. Performance ya mtu haipimwi hivyo mkuu, unajiaibisha.
The good way ya kupima performance ya Migiro: tuambieni ni kipi alitakiwa kukifanya na hakukifanya, ni kipi hakutakiwa kukifanya akakifanya na wapi ambapo amekosea, mabaya yake ni yapi? wapi alikiuka miiko na maadili ya kazi au taaluma yake? tupeni hizo data ndio mtuaminishe kuwa mama Migiro alifeli pale UN, otherwise hayo myasemayo yatakuwa ni majungu na fitina.
 
Jobless ni wewe unaeshinda lumumba kusubiri buku Saba kwa kila thread unayochangia. Kama ail perform better kwa nini baraza la usalama UN hawakumwongezea mkataba? Ni kwa sbb ni kilaza kazoo a kufanya mambo kimagambamagamba wakati we zako pale alikuwa wanakwenda kwa supersonic speed. Gamba we.

Vijana wa lumumba wana jitihada kubwa kuhalalisha malipo.yao
 
Kweli, but Akiwa Rais, nahama nchi

Shida yetu kubwa ni kuchukulia mambo juu juu kishabiki na kutofanya uchambuzi wa ndani.

ukifanya utafiti, toka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa ianzishwe, haijawahi kutokea mtu aliyeshika nafasi hiyo kwa mihula miwili. Mara zote imekuwa nafasi ya muhula mmoja ili kuwezesha mabara yote kupata nafasi kuongoza katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa UN.

Ndio maana mtu wa kwanza kuishika alikuwa Mcanada, akafuatiwa na mtu wa Latin America, akafuatia mtu kutoka Ulaya, akafuatia kutoka Afrika.

Mtu wa mwisho kabla ya Dk Migiro aliyeishika nafasi ile alikuwa anatoka Uingereza, jina lake lilikuwa Mark Maloch Brown. Mtu huyu alishirikia nafasi hiyo kwa mwaka mmmoja tu akaondoka. Na msijekudhani kukaa kwake kipindi kifupi hivyo alikuwa na uwezo mdogo, la hasha. Huyu bwana ndio alkuwa UNDP Administrator (Mkuu wa UNDP duniani) aliyepata mafanikio makubwa sana. Si hivyo tu, hata baada ya kumaliza UN, aliporudi Uingereza aiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na akapewa hadhi ya kuingia kwenye Cabinet ya Uingereza. Na nchi yake ilimpa heshima ya kuwa Lord...desipite the fact kwamba amekaa UN as Deputy SG kwa kipindi kifupi kuliko mtu yoyote.

Dr.Migiro ame aliza full term ya u DSG, na tofauti na wenzie wote waliomtangulia kwenye nafasi ile yeye ndio mtu pekee aliyepewa meno ya kuongoza menejimenti ya taasisi ile. Kwa wale waliokutana naye kikazi (sio makundi na mashabiki wa 2015 wa hapa nyumbani, wanamkubali kwamba alikuwa mtu very firm, very thorough na alikuwa mfuatiliaji makini sana). Sifa hiyo ilimjengea imani kubwa Bw.Ban Ki Moon, lakini ilimjengea uadui na watu ambao walikuwa na maslahi yao binafsi na ya nchi zao ndani ya shirika.

Hata kwenye siasa za ndani ya mabara kwenye umoja wa Mataifa, mama huyu alijijengea maadui kwasababu ya msimamo wake wa kusimamia haki bila upendeleo. Hata kundi Bara la Afrika ambalo lilikuwa linategemea uwepo wake pale juu lingepata faida ya ziada lilikuwa disappointed kwasababu Mama yule alisimamia maslahi ya taasisi zaidi kuliko makundi. Hurka yake hiyo ya kutokuwa na upendeleo wa wazi wazi, ilijionyesha hata katika kuteua wasaidizi wake, badala ya kujaza watu wa nchi yake tu, alifanya usaili makini ha kupata wasaidizi kutoka mabara yote ikiwemo Afrika, Ulaya nk. Ni wazi kabisa kwa siasa za UN zinazoelemea kwenye maslahi ya makundi, nchi, mabara, style ya uongozi ya mama huyu haikuwafurahisha wengi. Watu wengi wanamlaumu Mama huyu juu ya kushindwa kumtetea Prof.Anna Tibaijuka pale alipoungia kwenye mgogoro na Warusi ambao walikuwa wanaitaka nafasi yake na wakatumia uwepo wao kwenye Baraza la Usalama kama mjumbe mwenye turufu kumshinikiza KM wa Umoja wa Mataifa amtose. Mambo ya ndani hayasemwi, lakini ukweli ni kwamba Mama yule alifanya kazi kubwa ya kumshawishi KM wa Umoja wa Mataifa afanye maamuzi kwa misingi ya taratibu na sheria bila kumuonea mtu au bila kujal maslahi ya makundi au mabara. Kwa bahati mbaya KM bwana Ban alishafanya uamuzi......na alikuwa na haki ya kuchuk uamuzi aliochukua kwasababu mwisho wa siku wakubwa wale ndio wangemchagua tena kushika nafasi yake kwa kipindi cha pili (KM wa UM anachaguliwa na Baraza la Usalama na kuidhinishwa na Baraza Kuu) ili kulinda mkate wake akakubali kumtosa Mama Tibaijuka ambaye alikuwa na msimamo mkali wa kudhibiti ubadhilifu uliokuwa ukifanywa na raia wa urusi ambao walikuwa kwenye UN Office pale Nairobi. Mwisho wa yote, historia itamhukumu Dr Migiro kwa kazi aliyofanya pale UM.

Utamaduni wa mataifa yote ulimwenguni kujivunia pale raia wake anapomaliza kazi nzuri katika nyanja za kimataifa. Utamaduni huo umekuwepo hata hapa nchini huko nyuma akina Salim A Salim, akina Getrude Mongera walipomaliza walipongezwa na kuonekana mashujaa waliopeperusha jina la nchi yetu. Lakini kwa Dk Asharose kwasababu ya siasa zetu uchwara ambazo zimegubikwa na uchu wa urais 2015, Mama huyu amerudi nyumbani na kupokewa na maneno ya uwongo na uzushi kutoka kwa waathirika wa utawala wake kule UN kwamba ameshindwa kazi, mkataba haujaongezwa. By the way, Bw.Ban Ki moon kabadilisha timu yoooote, hakuna aliyebaki katika ngazi ya juu kasoro yeye mwenyewe.....unataka kusema wale wooooote ni vilaza? Fanyeni utafiti mdogo mtagundua baadhi ya wale walioondoka, ni watu walio accomplish mambo makubwa sana kwenye medani za kimataifa na kwenye nchi zao.

watanzania wote bila kujali itikadi zetu, tulitakuwa kufurahia mafanikio yake badala ya kuyaponda. Hakuna mtanzania amewahi kufikia ngazi aliyofikia, ha pengine hatatokea katika miaka mingi ijayo, hivyo tusiharibu sifa hii nzuri ya mwenzetu ambayo tulitakiwa kuipigia kelele ili kuwa motivate watoto wa kike wa tanzania kwamba wanaweza, yupo mtanzania mwanamke aliyeweza.

Mwisho nitoe changamoto kwa critics wake, zaidi ya kumchambua historia yake katika UMoja wa Mataifa, nendeni deep zaidi mchambue nafasi nyingine alizowahi kushika nchini- Serikalini, na nje ya Serikali. Tafuteni watu wanaomfahamu kwa karibu wawaeleze Asharose ni mtu wa aina gani, ana uwezo gani, anasimamia nini? Mimi binafsi ninamfahamu- ni mtu mwadilifu, ni mchapa kazi hodari, hapendi ubabaishaji- siku zote wababaishaji wamekuwa matatani wanaposhughulika na mama huyu, ni mtu anayefuatia mambo in details- na akianzisha jambo hulisimamia mpaka lifike mwisho wake....sio mtu wa matukio, sio mtu wa kutafuta umaarufu. Anazo sifa zote za kuwa kiongozi bora kuliko watu wengi ambao wanaongozwa na matukio na umaarufu wa bandia kwa kutumia ushawishi wa fedha.

 
Back
Top Bottom