Rais Joe Biden azuru Kyiv, Ukraine Februari 20, 2023

Rais Joe Biden azuru Kyiv, Ukraine Februari 20, 2023

Nipo salama kabisa Kaka,kupotea ni majukumu wakati mwingine yanatufanya tuwe tunachungulia tu na ku comment hapa na pale mara chache.

Najiandaa kumsikiliza Putin nimeona Sky News watafanya coverage ya hiyo hotuba.Wacha tumsikilize anakuja na yapi mapya leo.
Yuko live mkuu ngoja numuite mzee wa mbutu bloku a yeriko

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini Marekani anamuwekea vikwazo Urusi? Yeye kama nani?
Kwanini Urusi asimuwekee vikwazo Marekani?
Kama nchi ikikuwekea vikwazo na vikatiki basi hauna uwezo wa kumpiga huo ndiyo ukweli.
Kuna nchi ilishawahi kumuwekea vikwazo Marekani?
Kama Russia ameshindwa kuichukua Ukraine mpk sasa hivi, hana ubavu wa kupigana na Marekani. Hata China analijua hilo ndiyo maana wanawekewa vikwazo

Someni historia kwanza kabla ya kutoa comments kuhusu masuala ya punitive sanctions - kumbuka Umoja wa mataifa ndio walikuwa na manlaka ya ku slap sanctions kwa Taifa lolote linalo fanya mambo ya ndio siyo - hakuna article yoyote kwenye sheria za Umoja wa Mataifa ambazo zinaiipa Merikani mamlaka ya ku slap punitive sanction yeyote kwa Taifa lolote hasa mataifa ambayo Merikani wana yachukulia ni washindani wao kijeshi na kiuchumi, wanalazimisha zitengwe tu wakati kiukweli Merikani haina mamlaka yoyote kupoka mamlaka ya UN for political gain.

Sasa cha kujiuliza hapa - Marekani walipata wapi ujasiri na ujeuri wa kupoka mamlaka ya Umoja wa Mataifa? Jibu ni dogo: Merikani walianza kivimba kichwa na ujeuri baada kisitishwa kwa vita baridi baina ya US na USSR kwa maelewano baina yao lakini vyombo vya magharibi ueneza propaganda kwamba USA ndio ilishinda vita baridi - ulagai utupu!! Tangu wakati huo ndio USA ikaanzisha mbinu zake za chini chini za kutaka wajenge Unipolar World na wendawazimu wao wa so called NWO - mawazo yao hayo ya ajabu ndiyo yakawafanya wajione wanazewa kufanya lolote muda wowote bila ya kuhojiwana mtu - miaka hiyo walijuwa kwamba Urusi haipo kama zamani kijeshi na kiuchumi - Ujinga wa Rais mlevi Yeltsin akawaruhusu jeshi la Merikani kuja ku-dismantle ndege hatarishi za Urusi, Submarines, Submarine hunting choppers some of Russian fighter bombers were brand new, ICBMs etc - lengo la USA walitaka kuwarudisha nyuma Urusi kijeshi na kiuchumi ie USA wasiwe na mshindani mkubwa kwa nyanja zote. Come Putin ka-reverse kila kitu hasa kijeshi Taifa la Urusi likaanza kuheshimika sana kimataifa - what Putin did to RF ni mihujiza kabisa hata mataifa ya magharibi hawamini macho yao. Mataifa ya magharibi hasa USA hawampendi kabisa Putin kutokana na ujasiri wake wa ku-dismantle Unipolar World na NWO akishirikiana na BRICS alliance kitu hii inawatia wasi wasi sana Uncle SAM ndio maana anapalililia vita Ukraine na soon Taiwan lengo lake nihilo hilo wavuruge alliance ya BRICS and other economically independent Nations ambazo hazikubali kupelekwa putana mataifa ya magharibi - nawakumbusheni kwa mara nyingine tena kwamba vita vita na vurugu zinazo endelea kila pembe ya Dunia muhusika mkuu na huyo huyo Merikani - hawataki kuzidiwa kete na Urusi/China nk - wabnafsi kama nini.
 
Ndiyo mmeamua kujifichia hapo,sasa alivyotaarifiwa si ndiyo sasa angeonyesha makeke yake.Kumbe kataarifiwa na akaufyata kimya kama hayupo vile.
Watu wamekasirika.

Wanataka iteka Ukraine, wameshindwa lipua Ikulu ya Kyiv
 
Wadau habarini!

Tunaomba mwenye hutuba ya Rais wa Marekani Biden jana akiwa katika viwanja vya Kyiv., ambapo tunaambiwa alifunga safari ya muda mrefu kwa treni kuelekea vitani (Ukraine) kutembelea maeneo mchana kweupe.

Natanguliza shukuran
 
Ndiyo mmeamua kujifichia hapo,sasa alivyotaarifiwa si ndiyo sasa angeonyesha makeke yake.Kumbe kataarifiwa na akaufyata kimya kama hayupo vile.
Hujui kingereza au unajitoa ufahamu brother?
 
Ndiyo mmeamua kujifichia hapo,sasa alivyotaarifiwa si ndiyo sasa angeonyesha makeke yake.Kumbe kataarifiwa na akaufyata kimya kama hayupo vile.
The term "Deconfliction" maana yake U.S.A aliiomba Russia kupunguza mashambulizi eneo la tukio ili rais wao aweze kuwa salama.
 
Biden kaingia kwa siri kubwa sana huko Ukraine hata maafisa wa white house wengi wao walikuwa hawajui kama kuna safari ya rais Kenda Ukraine...US nao wamekuwa waoga sasahivi ..wamedhihilisha wazi kuwa wanamuogopa Urusi
Maswala kama haya ni nyeti na usiri ni kitu cha muhimu, wangeweza kutangaza hiyo safari ingekua na tension kubwa sana lakini wamejiandaa kiusalama na kujiridhisha kwamba wanaweza kuingia Ukraine bila dhara lolote, ndio maana imekua ghafla kwetu sisi lakini kijasusi ni mpango wa muda mrefu.
Marekani hawamwogopi Mrusi ila wameprove kwamba tunaweza kuandaa mpango wowote na kuingia Ukraine bila Moscow ambao ndio wanadai wameikamata Ukraine kufanya kitu chochote.
 
Ulitaka RUSSIA afanye nini ili kuionesha DUNIA kua hajaribiwi

Kwanini US asingeenda pale bila taarifa kwa MOSCOW ili kuionesha DUNIA kua yeye hatishiki na wala hatishwiii !!!??
Wewe unaitafsiri tofauti. Hivi kama wewe unarushiana mawe na jirani yako halafu mbabe mmoja awape taarifa kwamba niko napita njia hiyo kwahiyo acheni kurusha mawe yenu nipite kwanza halafu nikitoka ndio muendelee kurushiana mawe yenu. Hivi hapo Nani kaufyata? Aliyesitisha kurusha mawe ili mbabe apite au aliyetoa taarifa kwamba napita njia hiyo kwahiyo acha kurusha mawe?.
 
Aliheshimu sheria za UN zakutoshambulia wanadiplomasia

Kama alivyowaheshimu kina stoltenberg na wengineo woote

Kwanini WH ilitoa taarifa MOSCOW wakat anaenda UKRAINE

Yaani uende kenya halaf utoe taarifa Uganda

Us kaonesha udhaifu haswaaa
Acha uongo wewe. Umesahau mlivyovurumisha makombora kule Kiev wakati katibu mkuu WA UN Antonio Guteresh yupo Kiev mpaka kulazimika kuingia kwenye SHELTERS? Rusheni makombora Sasa ili na Biden akimbilie kwenye SHELTERS tuone. Yaani adui yako amtembelee mnayepigana naye vita na wewe utii ziara yake?
 
Watch: Biden promises to support Ukraine for 'as long as it takes' during Kyiv visit
[emoji1541][emoji1541]

[emoji837]


Pia unaweza kusikiliza hapa kupitia DW Swahili alichoongea Biden alipokuwa Ukraine
[emoji1541][emoji1541]
[emoji837]
Daah jamaa anazidi kuonesha vita haviishi leo wala kesho.
 
Back
Top Bottom