Wtu mnajadili masuala muhimu yaliyobeba mustakabali wa dunia, kama vile mnajadili habari za simba na Yanga!
Unadhani Putin akiwa anafanya ziara zake Marekani huwa hawajui? Nini huwa kinawafanya wasijipenyeze na kumshambulia Putin?
Hii dunia iko very complex kuliko ushabiki wenu. Warusi wanajua, kumgusa rais wa marekani ni kuanzisha vita ya dunia. Upande wa pili, Marekani pia wanajua kumgusa Putin ni kutangaza vita ya nyuklia. Wote wawili hawako tayari kufanya hivyo!
Ndio maana wanataarifiana.
NB: viongozi wengi tu wa ulaya wameshuka hapo Kiev na kuondoka salama. Wakubwa wanajua wanachokifanya!