Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Habari zimezagaa jijini Kinshasa kuwa Kabila atakuwa waziri mkuu nchini Congo huku Emmanuel Shadari akiwa Rais. Nafuatilia habari hizi kwa kina.
Tetesi hizi zinajiri huku chama chake cha PPRD kikiwa kimehakikisha Kabila atakuwa mwenyekiti wa kudumu wa chama hicho. Pia atakuwa mwenyekiti na mratibu mkuu wa muungano wa vyama vya siasa vinavyounga chama chake maarufu kama Common Front for Congo (CFC).
Mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama cha PPRD na muungano wake pacha wa CFC uliwekwa chini ya mikono ya Rais Kabila bila kujua ni kwanini watu wote hao walikubali hali hii.
Wagombea 26 wameshachukua Fomu za kuwania urais Congo na kila moja akilipa dola laki moja. Hizi ni hela nyingi ktk nchi masikini huku mtu akiwa na ari ya kugombea ili awatumikie wananchi wenzie.
Hivyo kwa unyonyaji huu tume ya uchaguzi CENI imeingiza dola za Marekani 2600,000. Hata hivyo wachambuzi wa mambo wameendelea kuwashangaa wakongomani kwa wengi kujitokeza kuchukua Fomu licha ya gharama za fomu kuwa juu.
UPDATES: Wakati wa kipindi cha Maoni cha radio DW kiswahili ya ujerumani jumamosi tarehe 11/08/2018 saa saba mchana kwa saa za Africa Masahariki na saa sita mchana kwa saa za Congo DRC limeibuka jambo. Mbunge wa PPRD Franswaa Nzekuye kakiri wazi Kabila anaweza kuwa waziri mkuu na baada ya miaka mitano kama wananchi wamemchoka Emmanuel Shadari, Kabila anaweza kugombea urais tena bila kizuizi chochote. Kipindi hicho cha maoni kilizungumzia siasa za Congo DRC na walioshiriki ni Wakongomani tupu.