ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 9,091
- 21,087
Kagame ameleta msimamo wa M 23 kuwa watambulike na congo DR, sijui ni kivipi serikali ya Congo haiwatambui Wanyamulenge?
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amesema nchi yake haiwezi kukaa kimya wakati usalama wake unahatarishwa na DRC na kubainisha kuwa Rwanda imejaribu mara nyingi kuzungumza na Congo bila mafanikio huku akisisitiza kuwa suluhisho la kudumu linahitajika badala ya lawama zinazoelekezwa kwa Rwanda kila tatizo linapotokea DRC.
"Congo hawawezi kutuambia tukae kimya wakati wanasababisha matatizo makubwa ya kiusalama dhidi yetu, hakuna wa kutuambia tukae kimya, tumeongea na Congo mara nyingi tumewaita tukae tuongee hawataki, Mimi naomba tusiwe na vikao vingi sana kama ambavyo tayari tumeshakuwa navyo.” — amesema Kagame akizungumza kwenye mkutano wa EAC-SADC.
“Hatuwezi kila siku kukaa kujadili matatizo maana kinachoendelea pale ni vita ya Kikabila ni suala la kutambuana, kujadiliana na kuwapa haki yao, tutumie kikao hiki kupata suluhu ya kudumu na sio matatizo yatokee Congo kisha ubaya anapewa Rwanda" — amesema Kagame.