Rais Kagame ataka M23 watambuliwe na Serikali ya DR Congo

Rais Kagame ataka M23 watambuliwe na Serikali ya DR Congo

hiki kikao cha leo ndo kimewahalisha wanyamurenge kuwa sasa nao ni wananchi halali kabisa wa drc maana hadi wametajwa kabisa kwenye makubaliano ya kikao na tshisekedi kaagizwa akae nao na awasikilize.

drc kwishnei. na hiki ndo alichokuwa anakitafuta PK sikuzote hizi. kikao cha leo ni pigo kubwa sana kwa tshisekedi na jamaa zake wa drc. haya maazimio ya leo hayatekelezi kwa tshisekedi. ni back to square one vita itaendelea.
DRC walishawatambua kitambo ila wachache wao walikaidi kwa kurud msituni , kamsikilize Kikwete ameleezea vzr tu , ttzo ni Kagame anataka mgogoro huu upambe moto ili aendelee kuiba
 
Kagame ameleta msimamo wa M 23 kuwa watambulike na congo DR, sijui ni kivipi serikali ya Congo haiwatambui Wanyamulenge?

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amesema nchi yake haiwezi kukaa kimya wakati usalama wake unahatarishwa na DRC na kubainisha kuwa Rwanda imejaribu mara nyingi kuzungumza na Congo bila mafanikio huku akisisitiza kuwa suluhisho la kudumu linahitajika badala ya lawama zinazoelekezwa kwa Rwanda kila tatizo linapotokea DRC.

"Congo hawawezi kutuambia tukae kimya wakati wanasababisha matatizo makubwa ya kiusalama dhidi yetu, hakuna wa kutuambia tukae kimya, tumeongea na Congo mara nyingi tumewaita tukae tuongee hawataki, Mimi naomba tusiwe na vikao vingi sana kama ambavyo tayari tumeshakuwa navyo.” — amesema Kagame akizungumza kwenye mkutano wa EAC-SADC.

“Hatuwezi kila siku kukaa kujadili matatizo maana kinachoendelea pale ni vita ya Kikabila ni suala la kutambuana, kujadiliana na kuwapa haki yao, tutumie kikao hiki kupata suluhu ya kudumu na sio matatizo yatokee Congo kisha ubaya anapewa Rwanda" — amesema Kagame.
Na tatizo la FdLR na Mkataba wa Amani wa Arusha vipi nao tukae Kimyaa wakati , ukabila pia upo Rwanda
 
DRC walishawatambua kitambo ila wachache wao walikaidi kwa kurud msituni , kamsikilize Kikwete ameleezea vzr tu , ttzo ni Kagame anataka mgogoro huu upambe moto ili aendelee kuiba
Link ya Kikwete kuhusu Banyamulenge
 
Serikali ya DRC itawezaje kuwatambua Banyamulenge wakati wako na silaha mkononi, huku wakipigana kutaka kuipindua serikali halali ya DRC?
Hallo...M23 Ukikaa nao na kuwasikiliza matakwa Yao, hawana Jambo la msingi..wanataka watambuliwe na wawekwe Kama viongozi katika serikali ya DRC... Hili Jambo likishafanyika inakuwa Kama mazoea kwa makundi mengine ya kwamba Kuna shortcut ya kuingia serikalini..hivyo vitazaliwa VI M23 VINGI SANA
 
Tatizo lenyewe sasa ni yeye Kagame. Suluhishio ni SADC-EAC kuwapa kipigo M23 kisha kutengeneza Buffer Zone katika mpaka wa Rwanda.
Au wawafurushe hadi Rwanda ndani kabisa ili Rwanda wapate joto la vita
Ishu ni kwamba majamaa Hawa Wana silaha nzito nzito sana...afu wanajificha kwa raia...na DRC walizuiwa kubunua silaha kutoka kwa mabeberu miaka flani hapo nyuma but now sijajua kwa mda huu
 
Back
Top Bottom