Rais Kamuzu Banda alizitaka Mbeya, Njombe na Songea kuwa sehemu ya Malawi

Kiongozi ya ndani kwetu ni magumu, kutokana na katiba yetu; mengine kuyaongelea sio salama.

Iła mipaka ya Tanzania sio swala la mzaha kabisa, hilo ndio eneo kama nchi JWTZ aicheki.
Kwenye swala la mipaka ndio utajua JWTZ ni kina nani , ila nimeshangaa sana kuona hili ziwa nyasa google walisha badilisha muda mrefu sana sijui serikali yetu ilikiwa wapi
 
Nakumbuka miaka ile ya 70 wakati tunaimba nyimbo za kumkejeli Banda
Banda wa Malawi, atuvalia ngozi ya simba, kututishia watanzania hatujali hatujali
Mwalimu kwa propaganda alkua mkali sana...Banda asingemweza...idd amini aliitwa nduli...hivi nini MAANA ya nduli? Kwenye swala la mipaka hakuwa na mchezo
 
Hili linanikumbusha pia kisiawa cha ''Latham'' kati ya Tanganyika na Zanzibar
Kwa muda mrefu kimekuwa Tanganyika hadi Samia alipokirudisha Zanzibar alipokuwa Rais wa JMT
Hili wamemruhusu vipi huyu mama kulitekeleza? Mbona ajabu hii na viongozi wa Tanganyika wamekaa tuu?
 
Kwenye swala la mipaka ndio utajua JWTZ ni kina nani , ila nimeshangaa sana kuona hili ziwa nyasa google walisha badilisha muda mrefu sana sijui serikali yetu ilikiwa wapi
Uwezi lazimisha kuamua wengine wanavyotaka kuku-label; JWTZ inajua mipaka halisi ya Tanzania sio Google.

Kungekuwa na mgogoro halisi huko ungeona wameanza mazoezi, kama wanavyofanya kwenye mipaka mingine korofi.

Unadhani wanaenda tu kufanya mazoezi mipakani, kama awajaona huyu jirani ni mkorofi.

Malawi akiwa shida wataenda huko.
 
Mbeya kuwa Malawi! 🤔🤔😲 Labda huko mpakani Kasumulu, lakini kujumuisha Mbeya yote kuchukuliwa na Malawi hiyo Ni impossible. Yaani mie wa Kambikatoto Chunya mara paap nimekuwa Mmalawi. Lol!
Sio mmalawi, utaitwa mnyassa
 
Mwalimu kwa propaganda alkua mkali sana...Banda asingemweza...idd amini aliitwa nduli...hivi nini MAANA ya nduli? Kwenye swala la mipaka hakuwa na mchezo
Aliipenda sana nchi yake
Naona nduli lilikuwa kama tusi la kumuita Idd Amin kama mnyama au jitu katili
Tuliimbishwa haswa ila baada ya vita tulisota sana na kufunga mikanda
 
Dah akomae malawi.........asee kuna nchi ni tishio ila sio malawi aisee,,,,,,labda kama watasogeza mipaka na hao waganga wao wa style za waganga wa wakinga
 
Na sisi tuakikishe tunadai nchi yetu ya Rwanda na Burundi
 
Niko upande wako 100%
 
Sisi ambao tuko mipakani karibu na Malawi ikitokea tukapiga kura ya kuwa sehemu ya Malawi hatukatai.Malawi kunamifumo mizuri ya kielimu,kiuchumi , kibiashara na,kijamii kuliko Tanzania.
Kama mambo ni mazuri hivyo basi huku mjini wasingejazana watu wao wakifanya kazi za ndani
 
Mtu ashatangulia mbele ya haki huyo


Udongo ushakula tayari
 
Sasa Tanganyika ingebaki nini, kama na nduli Iddi Amini alikuwa anaitaka Kagera
 
Nimewahi kusoma hilo chapisho. Kesi ya Ziwa Nyasa kwa asilimia kubwa haipo upande wetu. Na kumbe mwanzoni Nyerere alitambua kwamba hatuna sehemu ya ziwa!! Alitegemea Wamalawi watakuwa reasonable na watamaliza suala mezani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…