Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

It is not huyu jamaa, it is Katiba mbovu ndio matokeo yake haya.
 
Duuuuh....!!! Haya bwana kikwete. KILA la kheri na mipango yako
 
Last edited by a moderator:
Izo ni mbinu za kiintelejensia. Ameshaona kuna viongozi ni tim fulani watapenyeza siri ivyo anajaribu kuaribu sistim
 
Lowasa hadi sasa mshindi ndio maana tumeona watu wameteuliwa siku 5 kabla ya muda wa raisi kuisha
 
wataendelea kuwepo,,,unafikiri rais mpya anaanza kuondoa wafanyakazi kazini,,,itachukua kama miaka 2,kabla rais mpya hajaweka watu anaowataka yeye,,sio jambo la kuapishwa leo na kuanza kuondoa makatibu tawala,,etc

Hivi ukiwa CCM ubongo unatindia?
 
Mnakumbuka wakati ule wa EPA baadhi ya watu wakiunguza Range Rover zilizojaa document za muhimu?
Sasa ukiona hivyo watu wana preposition wafuasi wao kwenye maeneo muhimu.
 
Ni haki yake kisheria, lakini kibusara ninashaka.

busara ipi iliyokiukwa hapo?,,,,tatizo la bavicha bana ni ushabiki uliopitiliza,,,sasa hapa jk amekiuka busara ipi hasa?hebu tufafanulie....



tatizo lingine la bavicha ni wivu wa kike,,,,,
 
Raisi wa Jamhuri ya Muungano amemtea Eliakimu Maswi kuwa katibu Tawala wa mkoa wa MAnyara na Aliekuwa kaimu Mkurugenzi Bandari nchini ameteuliwa kuwa katibu Tawala wa mkoa Katavi
 
JK ATEUA MAKATIBU WAKUU WANNE NA MANAIBU KATIBU WAKUU WATANO WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa mujibu wa uteuzi huo,

Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.
From Bandari to KATAVI,wataisoma namba
 
Katiba inamruhusu. Sasa hivi ni piga tu,hakuna busara yoyote inayohitajika. Usishangae akaanza kuwateua wabunge na kubadilisha baraza la mawaziri (ingawa muda wa bunge umeisha.)
 
rais anayo mamlaka hayo mwehu wewe.... Hata kesho anaweza kufanya chochote.
 
Rais ana mamlaka kikatiba kuteua yyt amtakaye ili amradi akidhi vigezo mpk ukomo wake wa uongozi unapoisha,wazee wa viroba tulieni mnyolewe na sindano ziwaingie,huyo ndo jk,born in town,raised,schooled,graduated and employed in town,the (saigon boy),amesoma alama za nyakati
 
Huyu jamaa anazidi kumwaribia tu Magufuli......

Ninaomba sheria ya wagombea iboreshwe. Wawe wanapimwa akili kwanza kabla hawajapewa form. Ni hayo tu.

haa haa ulaji. na maghufuli atafanya hivohivo tena kwa kasi ya ajabu. dawa ni kesho kuchagua lowasa...

Maswi tena!

Mliomchagua Kikwete mmetuponza sana watanzania.

Nakiri kumtopenda huyu raisi kwa kiwango cha juu sana.

Jamani nishasema humu jamvini msije shangaa J'tatu watu tunasubiri matokeo jamaa anateua watu.

Ebu Sasa Tuambieni Wana CCM; Tuseme Kwa Bahati Mbaya Magaufuli Akabahatika Kuupata Urais wa JMT, Je Walioteuliwa Jana na JK

Atarecall uteuzi Huo.Hii Sasa Ni Too Much, Nadhani JK Anajaribu Kucheza na Psychology/Bongo za Wapiga Kura. Wapiga Kura Ebu Jitokezeni

Tuwaonyeshe CCM ya Kwamba Rais Uchaguliwa na Wananchi na Sio Kuteuliwa na Viongozi wa CCM.Kesho Pigeni Kura za hasira

Tujinasue Na Minyororo Hii ya Kujiona Wanyonge kwenye Nchi yetu.


Ninawasiwasi Na Uchaguzi Huu..Tutaweza Kumaliza Vibaya Kwani Kuna Kila Dalili za Wagombea Kutofika salama.../ Uchaguzi Huu Ni

Mkali na Upepo Unavuma Kulekea Upande wa Lowassa/Ukawa. Je Itakuwaje Mh. Lowassa Akishinda, na je atakubali wateule wa jana Waendelee na Nafasi zao.

Kesho sio Mbali Tutajua Mbivu na mbichi...

huyu jamaa ahamini kama kesho anafungasha viragoo//////// hapa makomeo anaenda kuwa bawaba tu ila mlango ni jk

Yaani huwa nalaumu sana walompgia kura huyu jamaa,hii ni zaidi ya kero, cjui hata ni wa kuweka kundi gani

maswi karudi tena? nimeamini huyu jamaa sio mzima kichwani na hakitakii mema chama chake!

nilishasema mtavimba mpaka mtapasuka bure,,,,na mkiindeleza kilomolomo atateua hadi tarehe 30,,,,just to prove a point...

Omar chambo ni mpiga dili mkuu alikuwa wizara ya uchukuzi akashindwana na mwakyembe Leo kapelekwa kwenye gesi

He can't be serious!

wataendelea kuwepo,,,unafikiri rais mpya anaanza kuondoa wafanyakazi kazini,,,itachukua kama miaka 2,kabla rais mpya hajaweka watu anaowataka yeye,,sio jambo la kuapishwa leo na kuanza kuondoa makatibu tawala,,etc

Umetuonyesha dhahiri jinsi ambavyo CCM hamna Nia nzuri na watanzania.

Hii tutapiga chini kesho kutwa,

Sheria bila busara wala mazoea ni mchezo mchafu

It is not huyu jamaa, it is Katiba mbovu ndio matokeo yake haya.

Ukistajabu ya musa utayaona ya jk😎😎😎😎😎

Wonders shall never end

Katiba inamruhusu. Sasa hivi ni piga tu,hakuna busara yoyote inayohitajika. Usishangae akaanza kuwateua wabunge na kubadilisha baraza la mawaziri (ingawa muda wa bunge umeisha.)

Ccm oyeeeeee.......
Ccm mmeipenda wenyewe,
Ccm kazi tu,
Ccm ileile,


#mabadiliko
#ccmout
#maajabuyakikwete
 
Back
Top Bottom