Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Hata sijui anawaonaje WaTZ? Huyu jamaa amewadharau sana wananchi. Safari zake watu wamesemaaaaaa lakini aliendelea tu hadi juzi.
Imagine nchi zenye demokrasia ya kweli, ambapo mwananchi akitoa malalamiko tu, kiongozi huenda na maji.....Tutafika lini huko?

mbali na hivyo mimi nasema hivi endapo kama huyu jamaa angekuwa anaongoza taifa la watu wanaojielewa yaani wanaofahamu haki zao kutoka serikalini ni nini, huyu mkware asingemaliza muda wake
 
Raisi wangu dah!!!!!!!!!!!!!

Hata kama sheria/katiba inaruhusu lakini sio kihivyo jamani.
 
Najaribu kuwaza kwa sauti.
Teuzi za mabalozi, wakuu wa wilaya, mikoa, makatibu wakuu, wabunge na watumishi wengine waliopo serikalini na ambao walifaidika na fadhila za ccm miaka ya nyuma na familia zao na hata ukoo wao unaofaidika na teuzi hizi, ina maana ccm wanaanza kesho na idadi ya watu/kura 3milioni.

Tutashinda kweli?

umewaza kitu cha msingi sana kaka, hapa tushirikiane na Askofu Gwajima tusali sana hata hao wanufaika na utawala huu dhalimu wapeleke kula zao mahala panapo stahili
 
Mwaka huu tusipofanya mabadiliko Mungu atatushushia laana ambayo itatutesa sana,
Wale wazee Wa kutetea kila kitu kwa ushabiki maandazi endeleeni tu
Mi kesho naenda kufutilia mbali hii CCM

Kabisa mkuu. Yaani tusipoindoa ccm mwaka huu tutakuwa sawa na yule jamaa wa kwenye biblia aliyefukia talanta yake chini badala ya kuifanyia biashara izalishe kama walivyofanya wenzie.
 
eeh haya....
JK ATEUA MAKATIBU WAKUU WANNE NA MANAIBU KATIBU WAKUU WATANO WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa mujibu wa uteuzi huo,

Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.
 

Kama UKAWA Watatumia Kete Hii Majukwaani Leo, Hili Litawageuza Wengi Ambao Kesho Walipanga Kuipigia Kura CCM, Magfuli Anaubiri Ufisadi Huku Mzee Mrisho, Anawateua Hao Hao Kuwa Wasaidizi WAKE? Akiya Mungu CCM Ni Wasanii Wa Kupindukia.

Naanza kuamini Kauli ya Lowassa kwamba hawajakutana na JK barabarani......Hapa anaingamiza CCM mazima.Hii ni kete ya Ushindi kwa Lowassa na Ukawa kama watatumia kete hii majukwaani Leo hii.....Hiki ni kifo cha Mende..Chaliiiiii
 
Kwa nini? Jk bado raisi anaendelea na majukumu yake kama kawaida, au amevunja sheria yoyote na huu uteuzi?

Ateue nafasi mbili za Mawaziri waliofariki basi maana nazo ziko wazi. Nafasi ya Kigoda na Kombani.
 
Back
Top Bottom