Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

JK ATEUA MAKATIBU WAKUU WANNE NA MANAIBU KATIBU WAKUU WATANO WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa mujibu wa uteuzi huo,

Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.


madaraka matamu..mjomba tuachie nchi yetu. kapumzike kwa salama.
 
Yaani huwa nalaumu sana walompgia kura huyu jamaa,hii ni zaidi ya kero, cjui hata ni wa kuweka kundi gani
kwa kweli hata mimi nilishiriki kumweka huyu "dhaifu" madarakani 2005. Nilimwomba Mungu anisamehe na akanisamehe; makosa jinsi ile sirudii tena!
 
Maswi tena!

Mliomchagua Kikwete mmetuponza sana watanzania.

Nakiri kumtopenda huyu raisi kwa kiwango cha juu sana.

Hatunywi sumu hatunyongi............ccm mbele kwa mbele !
Na mvimbe mpasuke .......mtajijua wenyewe ! Salary Slip
 
Last edited by a moderator:
Wana JF,

What is the meaning of all these nonsense?
Hivi huyu Rais anayeondoka baada ya masaa 24 NEC itakapotangazwa Rais mteule ana maana ani kuendelea kuteua Watumishi katika cadre mbalimbali? Alikuwaga wapi siku zote za miaka 10 kuwateua hao maswahiba wake??

Hivi Rais Kiwete anafikiri huyo Rais anayekuja hataweza kuteua wasaidizi wake???Hii definetely ni MATUMIZI MABAYA, MABOVU sana kwa ofisi ya Rai!!!!K wa kifupi huu ni UFISADI WA AINA NYINGINE!!

Watanzania hatuoni mantiki ya Rais aliyebakiza masaa kuendelea kufanya uteuzi wa kipuuzi kana kwamba ni swala la dharura...........!!!!!! Rais dhaifu peke yake ndiye anaweza kufanya upuuzi kama huu.
 
Maswi tena!

Mliomchagua Kikwete mmetuponza sana watanzania.

Nakiri kumtopenda huyu raisi kwa kiwango cha juu sana.

Hatunywi sumu hatunyongi............ccm mbele kwa mbele !
Na mvimbe mpasuke .......mtajijua wenyewe ! Salary Slip
 
Last edited by a moderator:
Maswi tena!

Mliomchagua Kikwete mmetuponza sana watanzania.

Nakiri kumtopenda huyu raisi kwa kiwango cha juu sana.

Hatunywi sumu hatunyongi............ccm mbele kwa mbele !
Na mvimbe mpasuke .......mtajijua wenyewe ! Salary Slip
 
Last edited by a moderator:
Naanza kuamini Kauli ya Lowassa kwamba hawajakutana na JK barabarani......Hapa anaingamiza CCM mazima.Hii ni kete ya Ushindi kwa Lowassa na Ukawa kama watatumia kete hii majukwaani Leo hii.....Hiki ni kifo cha Mende..Chaliiiiii

Sasa mnalia lia nini !?.......kwani mmejipangaje !?? made
 
Last edited by a moderator:
Yaani huwa nalaumu sana walompgia kura huyu jamaa,hii ni zaidi ya kero, cjui hata ni wa kuweka kundi gani

Walimpigia JK kwa style hii hii ya Lowasa. Mihemko ilitawala hivihivi na mainjinia wa mihemko hiyo walikuwa ni Rostam na Lowasa. Baada ya JK kuchukua nchi wakasuka dili la RICHMOND/DOWANS kurudisha gharama walizotumia kutengeneza mihemko. Na kwa kuwa serikali ilikuwa mikononi mwao wakatengeneza mazingira ya serikali kushindwa kesi na Rostam akalipwa Bil 120 na ndizo sasa wamezitumia kuwanunua akina Mbowe na kutengeneza mihemko mitaani. Ikiwa lowasa ataingia madarakani hizo gharama lazima zirudi. Rostam hajawahi fanya kazi za hasara. Unakumbuka KAGODA, na DEEPGREEN aliyechota Bil 40 kaunta za CRDB alikuwa nani?
 
Aaaaah wewe unadhani anawakomoa wapinzani...NO hili ni janga la kitaifa including you and your family
 
Sheria inaendana na busara. Dibagula, alipofungwa kule Morogoro, sheria ilifuatwa. Akahukumiwa; lakini mazingira ya uvunjifu wa amani uliifanya Mahakama ya juu ione busara ya kufuta kabisa ile hukumu kwa mkosaji. Unachoona hapo ni kwamba pamoja na sheria kuwa ilitumika vizuri, bado busara ilitawala na ikaifanya nchi ikatulia.
Kwa hili la JK kuendelea na uteuzi hadi dakika za majeruhi ni kweli Kikatiba yuko sahihi, lakini busara inagoma kabisa! Huwezi kuwa unajindaa kuondoka madarakani wiki moja ijayo halafu ukaunda safu unazotaka wewe. Hii ni gharama. Kumbuka, huyo anayekuja anaweza kupangua wote hao, na wakalipwa mafao! Mzigo ni kwa mwananchi maskini. Yeye atakuwa anakula maisha yake ya ustaafu kama kawaida. Fikiria, mtu dhaifu kabisa kama Kipande anampa madaraka baada ya kuvuruga Bandari! Huyu Rais ni wa pekee, si kwa Afrika Mashariki na Kati pekee, bali ulimwengu mzima. Tulipomuunga mkono mwaka 2005 hatukujua tunaunga mkono aina hii ya kiongozi! Mungu atusamehe. Watanzania watusamehe, na zaidi ya wote; Dk. Salim Ahmed Salim atusamehe!!

....Je; unaweza kuripoti hivi hivi kwenye gazeti lako la Raia Tanzania la kesho?!
 
Ebu Sasa Tuambieni Wana CCM; Tuseme Kwa Bahati Mbaya Magaufuli Akabahatika Kuupata Urais wa JMT, Je Walioteuliwa Jana na JK

Atarecall uteuzi Huo.Hii Sasa Ni Too Much, Nadhani JK Anajaribu Kucheza na Psychology/Bongo za Wapiga Kura. Wapiga Kura Ebu Jitokezeni

Tuwaonyeshe CCM ya Kwamba Rais Uchaguliwa na Wananchi na Sio Kuteuliwa na Viongozi wa CCM.Kesho Pigeni Kura za hasira

Tujinasue Na Minyororo Hii ya Kujiona Wanyonge kwenye Nchi yetu.


Ninawasiwasi Na Uchaguzi Huu..Tutaweza Kumaliza Vibaya Kwani Kuna Kila Dalili za Wagombea Kutofika salama.../ Uchaguzi Huu Ni

Mkali na Upepo Unavuma Kulekea Upande wa Lowassa/Ukawa. Je Itakuwaje Mh. Lowassa Akishinda, na je atakubali wateule wa jana Waendelee na Nafasi zao.

Kesho sio Mbali Tutajua Mbivu na mbichi...


Jimbo la jf lina wapiga kura wachache sana.peleka stress zako utasikika na wengi
 
Yaani tena Maswi, Kipande na Chambo? Wapiga dili wakubwa. Ama kweli Kikwete kaamua!!
 
....Je; unaweza kuripoti hivi hivi kwenye gazeti lako la Raia Tanzania la kesho?!

Kimtokacho mtu ndo kimeujaza moyo wake! Manyerere eti na wewe leo unamsema JK Kweli ndo maana umetubu! na kesho andika haya haya kwenye Jamhuri yako au kule kwingine kwenye colum zako!
 
Back
Top Bottom