Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa naona ukosefu wa elimu ya lugha ya mawasiliano kwa umma. Kama rais hakupaswa kutumia lugha hii. Anaonesha kuwa na hasira na kupanic ambapo kisaikolojia ni njia mojawapo ya kumnasa mhalifu kwani mara nyingi hutumia lugha ya ukali ili kujilinda. Alipaswa kuwa makini katika kujibu hili. Vinginevyo atatufanya tumuone hajui uzito wa nafasi anayoishikilia. Mara nyingi nimemsikiliza tatizo lake ni hilo. hata kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi amejichanganya sana. Anakanusha wakati huo huo anajifunga mwenyewe na kukubali kosa. awaone wataalamu wa lugha ya mawasiliano kwa umma wamsaidieRais Kikwete akiwa Marekani ameongea na watanzania na kukanusha madai kuwa alimuokoa mwanae Ridhiwani nchimi China baada ya kukutwa na dawa za kulevya.
Rais amesema huo ni upuuzi na hawezi kuongelea upuuzi wa aina hiyo ambao ni uzushi usio na maana.
JK pia amewaambia watanzania waishio marekani kuwa sio kweli kwamba kusainiwa mikataba 12 kati ya Tanzania na China ilikuwa ni sehemu ya masharti yaliyotolewa na China wakati wa kumuachia Ridhiwani.
![]()
=======================================
Ukiwa muongo lazima uwe na kumbukumbu sana! Sasa sijui 'rahisi' wetu huwa anapoteza kumbukumbu au hupiga viroba kabla ya kuanza kuongea?
Hivi kwa akili zetu kweli kabisa mtoto wa raisi aende kubeba unga kupeleka China?
Amekosa nini hicho hadi akabebe unga?
Kwani awali alikuwa amekubali na sasa akakataa?
angeachwa tu anyongwe na sio kutoa ges yetu kisa rzone
huyu rais amechafuka kwa kashfa kuliko rais yoyote!kumbe yuko marekani!safari ya ngapi hii wadau?
Habari inaweza kuwa ya kweli au ya uongo vyote vinawezekana.
Unamkumbuka aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na pia aliyeisha wahi kuwa balozi wa TZ nchi za nje "Hassan Diria alikamatwa ujerumani akiwa na mzigo wa madawa ya kulevya?
Hawa jamaa huwa hawasachiwi kisheria, hivyo hutumia nafasi hiyo. Diria siku hiyo walimsachi ingawa ilikuwa ni kinyume cha sheria kumsachi, na wakamkuta na madawa ya kulevya.
Muulize Matonya wa bongo flava anajua kila kitu
Khaa!! Kumbe hata wewe uliamini???!!! Basi kuna kundi kubwa sana la watu hawa
well, hakuwa na diplomatic passport by then... ila alikuwa na nyenzo (fedha) za kuwaajiri vinaja wengi atakavyo kama kweli alikuwa anajihusisha na hayo madawa ya kulevya! BTW Rais huwa anapewa information nyingi za kujua hatari zinazomkabili yeye na familia yake! Msisahau kuwa Mengi aliwahi kupambana na Maharamia waliokuwa wanamtumia mwanae !!! Kwanini tusiamini kuwa ulikuwa ni mtego wa kumuingiza mwanae kwenye kashfa kama kweli ilitokea bali tunaingia kwenye conclusion kuwa Rizwan anahusika na biashara ya Sembe?... Bado sija shawishika kuwa Rizwan ni Duwanzi kiasi cha kushindwa kupima Risk ya yeye kujihusisha na madawa ya kulevya... I stand to be corrected!!!