Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukawa ukawa ukawa tuko nyuma yenu tutawa suport mpaka kieleweke
Rais Kikwete akiwa Marekani ameongea na watanzania na kukanusha madai kuwa alimuokoa mwanae Ridhiwani nchimi China baada ya kukutwa na dawa za kulevya.
Rais amesema huo ni upuuzi na hawezi kuongelea upuuzi wa aina hiyo ambao ni uzushi usio na maana.
JK pia amewaambia watanzania waishio marekani kuwa sio kweli kwamba kusainiwa mikataba 12 kati ya Tanzania na China ilikuwa ni sehemu ya masharti yaliyotolewa na China wakati wa kumuachia Ridhiwani.
![]()
=======================================
Na tangu lini 'Upuuzi' ukajibiwa kwa staili ya kukanushwa kwa nguvu nyingi na hasira hivi na Rais mwenyewe pamoja na taasisi yake ya Uraisi tena kwa mabandiko mazito namna ya hii?
Na kama kweli ni upuuzi kwa nini ichukue miaka zaidi ya miwili na kitu baada ya tukio hilo linalosadikika kuwa ni la kipuuzi kuripotiwa? Rais na taasisi ilikuwa wapi siku zote hizo wakati huo 'upuuzi' ulipokuwa unasambaa masikioni mwa wapuuzi?
Naona maswali bado ni mengi kuliko majibu...
Hapana, alitaka kufikisha ujumbe tu kwa mhusika maana ilibaki kama tetesi mda mrefuHivi muuliza swali alitegemea JK angekubali suala hilo!nadhani US watakuwa wanalifanyia kazi suala hilo kwa kuwa waliumia sana kwa kuukosa uwekezaji katika gesi!
Kesi si ipo mahakamani?Huyo aliyetoa tuhuma alipaswa kushitakiwa kwa uchochezi
mimi ningekuwa hakimu atakayeesikiliza kesi hiyo ningemuuliza tu mshtakiwa eti ulitegemea ridhiwani angepata shillingi ngapi(angefaidika kiasi gani) kwa kupeleka unga kiasi gani? halafu ndo tungejua kama akili zetu ziko MAKATONI au la?
Hivi waweza kuuliza Bahressa anauza chapati ili apate shilingi ngapi? Kwako wewe mwenye pesa hafanyi biashara ndogondogo?
Naona Al-Jazeera wanataka kulifufua hili jambo katika meno ya tembo