makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
- Thread starter
- #81
Kwani Jk sio Mtanzania?
Activister,
Ni Mtanzania lakini siyo Mzalendo.
Unaweza kuwa Mtz na usiwe Mzalendo. Tafuta maana ya neno Mzalendo ndipo utagundua kwamba Rais wako Kiwete hana hata chembe moja ya Uzalendo baali amejaa ubinafsi,unafiki,undumila kuwili,ufisadi na udikteta!
Kama kweli Rais Kiwete ni Mzalendo basi angelitanguliza maslahi ya nchi yake Tanzania kama Taifa badala ya kutanguliza maslahi ya Chama chake cha CCM!!! Kwamba Watanzania zaidi ya 60% wanataka Serikali TATU na wachache wanataka Serikali 2.
Kama unataka kujua Mzalendo wa kweli sikiliza na soma vitabu na hotuba za Baba wa Taifa. Kumbuka Nyerere aliunda Tume ya Rais ya kutafuta maoni ya Watanzania kuhusu Tanzania iwe na MFUMO GANI KATI YA CHAMA KIMOJA AU VYAMA VINGI. Taarifa ya Tume ya Rais ilikuja na Majibu ya asilimia 20 walitaka vyama vingi, na asilimia 20 walitaka chama kimoja.
Kwa hikima na busara Mwalimu aliamua kuwasikiliza wachache kwa vile aliona mbele kuwa tulikokuwa tunaelekea siasa za chama kimoja zilikuwa zimepitwa na wakti!! Hicho ni kipawa cha ajabu sana ambacho Mungu huwapa watu wachache hapa duniani!! Nasikitika kusema Kiwete hayuko kwenye kundi hili la wachache waliojaliwa vipawa vya Uongozi na Mwenye enzi Mungu!!