Rais Kikwete amteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi mpya wa mashtaka (DPP)

Rais Kikwete amteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi mpya wa mashtaka (DPP)

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
Rais Kikwete amemteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi Mpya wa Mashtaka nchini (DPP). Kabla ya uteuzi wake, Biswalo alikuwa Mkurugenzi msaidizi katika ofisi hiyo ya mashtaka. Uteuzi umeanza rasmi ijumaa iliyopita.

Dr Eliezer Feleshi ndie alikuwa akishikilia wadhifa wa DPP kabla ya uteuzi huu wa DPP mpya kufanyika.

==============

Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, Dar es Salaam.

6 Oktoba, 2014
 
Kila la kheri mganga,shitaki mafisadi sasa na sio wezi wa kuku kama Eliez
 
Shtaki akina nape wanaotukana watu hovyo hovyo na tumbo lake kubwaaaaaaaaaa
 
Rais Kikwete amemteua Bwi Bw Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi Mpya wa Mashtaka nchini (DPP). Kabla ya uteuzi wake, Biswalo alikuwa Mkurugenzi msaidizi katika ofisi hiyo ya mashtaka. Uteuzi umeanza rasmi ijumaa iliyopita.

Dr Eliezer Feleshi ndie alikuwa akishikilia wadhifa wa DPP kabla ya uteuzi huu wa DPP mpya kufanyika
Tumpe hongera kwa uteuzi wake huo mpya

Hata hivyo itakuwa vyema Mkurugenzi huyo mpya wa mashitaka,kama kazi yake na 1 atakapoingia ofisini,ataamua kuwaburuza mahakamani, vigogo wote waliokwapua zile shilingi bilioni 200 za kwenye akaunti ya Escrow.
 
Hapa ndipo ule utaratibu uliopendekezwa na Tume ya Warioba ulipopaswa kufanya kazi kabla ya kuingia ofisini. Kulitakiwa kuwe na chombo kingine kama Bunge ambalo sasa lingeingia kazini kumfanyia usaili mteule huyu kujua uwezo wake na kama anastahili kweli kushika wadhifa huu au lah. Hii ingeepusha utaratibu wa Rais kuteua washkaji au watu wa kulinda maslahi binafsi. Lakini masikini wabunge wa CCM wameukataa utaratibu huu na kuendelea kumrundikia Rais madaraka mazito!!!!
 
Hao maccm wamepitisha katiba yao ambayo kama siyo kumuachia madaraka makubwa mno Rais ya kuteua watendaji mbalimbali wa serikali, pengine itakuwa imemuengezea zaidi, jambo ambalo linafanya hao wateule wa Rais badala ya kuwajibika kwa wananchi, wateule hao wanakuwa 'loyal' kwa aliyewateua, ambaye ni Rais.

Kwa kuwa wahenga walinena, mtumikie kafiri, upate mradi wako!
 
Kova na macho yale si angekuwa anaandika mashtaka kinyume kama anaandika kiarabu

Nchi hii kwa Udini sasa uarabu umeigiaje,mfumo kristo mbaya sana.nyinyi endeleeni kutubeep beep tu.tusipoangalia Nchi nzuri tutaiharibu hii.
 
Back
Top Bottom