Rais Kikwete amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais Kikwete amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

BAADA YA FREDRICK WEREMA KUJIUZULU, RAIS ATEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MPYA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.


Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kazi ipo. Je hakuhusika kwa namna moja ama nyingine kwenye sakata la escrow?
 
Simuelewi Mkuu,ni zamu ya vijana sasa,hivi Riz si naye kasoma Bsc in Tundulisu?

Bsc in Tudulissu ndio mini mkuu?? Eh eh eh!! Au ndio LLB Law in Lissu Bachelor
 
Rais Jakaya kikwete amemteua George Masaju kuwa mwanasheria mkuu wa serikali katika uteuzi uliotangazwa punde. Nawawekeeni taarifa nzima ya uteuzi soon
..kama ni kweli basi hamna jipya....maana huyu ndie alikua kaimu mwanasheria mkuu wa serikali chini ya werema....na kwa maana hiyo anajua na kuhusika moja kwa moja kwa makosa ya werema..maana mara nyingi amekua anakaimu nafasi ya werema..huu uteuzi wa JK ni magumashi....ni muendelezo wa kuwalinda waalifu...so sad...
 
Rais jakaya kikwete amemtangaza mh.George Micheche Masaju kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Tafadhali mwenye wasifu wa huyu mtu atuwekee hapa
 
hivi wale mashehee wawili walio teuliwa namkumbua cag mwingine ni nani vile?
 
Back
Top Bottom