mwana wa mtemi
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 374
- 204
Taja Professor aliyeteuliwa Na JK ambaye amefanya kazi NzuriLeo tena Professor mwingine kaula kama CAG mbali na Professor Benno Ndulu na Muhongo
Anawaamini sana ingawa watendaji wadogo chini yao huenda wabovu.
Professor Assaid apewe ushirikiano
Leo tena Professor mwingine kaula kama CAG mbali na Professor Benno Ndulu na Muhongo
Anawaamini sana ingawa watendaji wadogo chini yao huenda wabovu.
Professor Assaid apewe ushirikiano
Tatizo pia ni sisi.Kwa mfano huu mtazamo kuwa kuteuliwa kwake maana yake "Kaula" ni lini utatutoka?
Huyo kaimu alishashindwa kazi.Jamani huyu rais kachemka issue urgent ilikuwa ni kumteua AG,Waziri wa Nishati, Katubu mkuu na Waziri wa ardhi na makazi sasa yeye kaanza na kulipisa kisasi kwa kaimu AG alitoa taarifa ya escrow kwa kumteuwa mwingine jamani sasa hayo ndiyo maazimio ya Bunge? ajabu sana.
Tatizo pia ni sisi.Kwa mfano huu mtazamo kuwa kuteuliwa kwake maana yake "Kaula" ni lini utatutoka?
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
PRESIDENT'S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.
Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.
Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.
Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.
Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Desemba,2014
-----------------------
profesa Sarungi
Pamoja na Maroroso yanayotoka Magogoni...naomba wale wataalam wanaochangia kukua kwa Kiswahili watueleweshe 'mchanyato' huu ni-aje??
" Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991."
Umakini wa hawa wakuu wetu wa Press Release! Mmh!, Naomba kutoa hoja..
Swali: Huyu siye Mwenyekiti wa Bodi ya NBC Bank?? If yes, NBC inaendeleaje!....then fill the blanks!
utawala wa Kikwete umenyofoa Ma-Dr. na Ma-Prof wengi sana kutoka Vyuo Vikuu japo wengi wao wameishia kutenda chini ya kiwango kilichotarajiwa, kuingia kwenye kashfa na wengine kuondolewa kwa aibu.
Nafikiri imani kuwa Dr. au Prof. anafanya kazi nzuri kuliko watendaji wengine haina mashiko sana.