karim wade
Member
- Apr 2, 2012
- 49
- 10
MkamaP, Salary Slip
..lakini JK alishatangaza hii "nia" in 2011.
..sasa tangu wakati huo serikali imefanya nini?
..kwanini in 2013 anarudia kutangaza "nia" aliyokwisha tangaza hapo awali??
..kwanini hatendi??
..wakati mwingine nalazimika kukubali kwamba kuna justification ktk hizi dharau na kejeli toka kwa majirani zetu wa Afrika Mashariki. Uongozi wetu umekuwa wa maneno-maneno tu kama hizo "nia" zinazotangazwa na viongozi wetu.
..someni hapa:Tanzania, Rwanda, Burundi team up on $5bn rail proposal
cc Geza Ulole, Nguruvi3
..Reli hiyo inajengwa mradi unaanza wakati wowote kuanzia sasa.
Mkuu JokaKuu,[B FaizaFoxy,
..OK, nime-copy taarifa toka link uliyoileta.
..nadhani kichwa cha habari ni kwa ajili ya kuvutia wasomaji.
..JK bado yuko katika hatua ya kutangaza "nia" ya kujenga.
..Wajapani wanadai tubakie na gauge iliyopo mpaka 2030 na wataleta wataalamu wa feasibility study.
..in the middle of the article unayonitaka niisome, mwandishi anadai nchi washirika wa mradi watafute funds ili ujenzi uweze kuanza.
..majuzi napo Rwanda wamechomoka na kuachana na mradi wetu, sasa wanataka kujenga reli kuelekea Uganda na Kenya.
..sasa hebu tueleze tufuate kipi hapa?!!
[/B]
cc FaizaFoxy
Jasusi
Naungana na wewe ni kweli reli ya kati itasaidia sana kukuza uchumi wetu itaunganisha mikoa ya kati mpaka kanda ya ziwa kusafirisha bidhaa.
JokaKuu,NasDaz,
..tatizo la Tanzania ni UZEMBE wa watawala wetu.
..kwamba Kenya alikuwa na miundombinu mizuri in the 90s kuishinda Tanzania, is not a justification kwa sisi kuwa nyuma yao kimiundombinu in 2013.
..Tanzania ina rasilimali nyingi zaidi, na nguvu kazi kubwa zaidi, hatutakiwa kuwa washika mkia ktk eneo hili la Afrika Mashariki.
Rais Kikwete ametangaza nia ya kuanza kwa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa. Rais amesema reli nyembamba inapatikana eneo la Afrika Mashariki tu.
Mh. Rais kayasema hayo mkoani Simuyi wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa barabara itakayounganisha mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani.
CHANZO: ITV
MY TAKE:
Hivi hizi ahadi zinatekelezeka kweli??!!
JokaKuu,
Hapa hakuna suala la ku-justify or anything like that; issue hapa ni kufanya Jambo X at time Y under the available resources!! Issue hapa is all about prioritizing alternatives under available resources; simple like that. Lakini kwa upande mwingine, huwezi ku-ignore ukweli kwamba Kenya tayari walishakuwa na miundombinu msingi kuliko Tanzania kwahiyo hata planning yao itakuwa tofauti tu! Wakati Tanzania sehemu kubwa ya bajeti yake inaenda kwenye barabara, Kenya lazima itaenda kwenye mambo mengine kwavile tayari barabara wanazo; huwezi ku-ignore ukweli huu unless kama unaamini there's somewhere outta there where people can go na kurudi na mifuko ya fedha na kisha kuwekeza kwenye mambo mbalimbali.
Tukija suala la kwamba Tanzania hatutakiwi kushika mkia ukanda huu, nashindwa kukuelewa kwavile Tanzania hatushiki mkia labda kama unamaanisha kitu kingine. Sio siri kwamba Kenya ana-lead lakini Wakenya wenyewe wanafahamu nafasi ya Tanzania...Watanzania tunajidharau wenyewe lakini technically Wakenya wanatuogopa na wanafahamu hawana muda mrefu wa kuwa the leading economy in EA. Angalia data for the past ten years kati ya Kenya na Tanzania ili uone position ya Kenya na TZ.....there's a very wide gap btn two countries lakini gap linapungua mwaka baada ya mwaka; yaani ni kama Kenya anatembea wakati Tanzania inakimbia. Jana nilifuatilia LIVE Coverage ule uzinduzi pale Kenya ambapo Kiongozi mmoja alisema wazi kwamba inabidi ujenzi wa Mombasa uanze mapema coz' wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka TZ ambao nao wapo mbioni kujenga reli of the same quality.
Tukija hilo la uzembe wa watawala wetu, sikatai lakini ni rahisi sana kusema hivyo ukiwa nje (usidhani mimi nipo ndani). Kwenye bajeti ya mwaka huu(2013/2014) nilikuwa na hamu sana ya kuichambua Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwavile wao kama wanasiasa ni rahisi sana kusema "tatizo ni CCM" Nilipoichambua bajeti ile nikakuta ina surplus ya kama shilingi trilioni moja hivi as compared to bajeti ya serikali! Kimsingi nilitarajia iwe ni bajeti iliyoainisha vyanzo vipya vya mapato lakini badala yake nilikuta hiyo additional TZS 1 Trillion wamefanya "ON" and "OFF", yaani walichokuwa wamefanya ni kupunguza kile walichoita posho zisizo za lazima (ingawaje wenyewe hadi leo wanachafuana mitandaoni kwa ajili ya posho) na misamaha ya kodi! Kwangu mimi, bado ongezeko la trillion (tena zisizo na uhakika) ni bado sana. UKiangalia mfano huo, utagundua kwamba tatizo la Tanzania ni zaidi ya watawala na ndio maana mimi nitakuwa mtu wa mwisho nchi hii kuamini eti kuna chama fulani hapa kitakachokuja kuweka mambo sawa wakati watanzania kwa ujumla wetu ni wale wale na viongozi/watawala ni wale wanaotoka kwenye jamii ile ile!!
Tukija upande wa rasilimali, nakubaliana na wewe tunazo za kutosha lakini ukiangalia vizuri, raslimali ya pekee ambayo imekuwa exploited kwa kiasi kikubwa ni dhahabu. Kwa bahati bahati mbaya sana, suala la dhahabu Watanzanai nalo tunaliangalia kwa makengeza; ni ukweli mchungu lakini ndiyo hivyo! Mathalani, hivi sasa ambapo usafirishaji wa dhahabu umepanda, dhahabu inayosafirishwa ni wastani wa tani 40 kwa mwaka....mimi na wewe tufanye ni tani 50. Bei ya dhahabu kwenye soko la dunia haijawahi kufika USD 2000 kwa troy ounce kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita lakini mimi na wewe ngoja tuseme USD 2000 ndiyo bei ya one troy ounce. Pamoja na kwamba tumejipendelea na kusema tunasafirisha tani 50 kwa mwaka, hizo ni sawa na takribani 1.6 troy ounce; kwahiyo ukizidisha kwa USD 2000, ni kama tunaingiza USD 3.2 billion kwa mwaka!! Hiyo ni gross income, less all other costs kisha assume una best mining contracts kisha niambie ungepata Sh. kwa mwaka bila kusahau kwamba figure nilizoweka nimezipandisha.
Hivyo basi, ukiangalia ukweli huo utagundua kwamba raslimali ya madini wala isingeweza kututoa kwenye umasikini. Uchumi wa raslimali za asili is all about what you gonna do with revenues from those resources lakini kwa nchi kama Tanzania ambayo bado haina miundo mbinu ya kutosha, tunalazimika revenues from resources ku-invest kwenye miundombinu badala ya ku-channel kwenye other sectors of economy. Nakubali kabisa kwamba tatizo lingine tulilonalo ni ufisadi na katika hili, hakuna CHADEMA wala CCM, Watanzani walio wengi ni watu wa hovyo hovyo na wezi bila kujali itikadi zao. Atakayekuja kuondoa matatizo makubwa ya nchi hii ni yule anayeamini kwamba Watanzania ni tatizo kuliko nyinyi ambao mnaamini kwamba watawala/CCM ndo tatizo kwavile utawala utakuja kubadilika na watu kudhani kwamba tumepata mwarobaini lakini kinyume chake tukaja kuona yale yale!
Mkuu JokaKuu, nashangaa serikali ya JK kusema tunajipanga kila siku.NasDaz,
..kwanza umeshajifunga mawazo yako kwamba HATUWEZI.
..sasa ongezea hapo na UZEMBE na UFISADI basi ndiyo maana Tanzania ipo hapa ilipo.
..nitakupa mfano mdogo: hivi kuna sababu yoyote ile ya msingi ya kuwa na mgao wa umeme for 20yrs? tatizo hili limekuwepo tangu JK yupo wizara ya madini na nishati na nimeng'ang'ania mpaka sasa hivi anaelekea kustaafu.
..Tanzania haipigi hatua za kimaendeleo zinazoendana na kiwango cha rasilimali tulizo nazo. hicho ndicho kinachonifanya niamini kwamba ktk eneo hili tumeshika mkia. kwa maneno mengine ni kwamba tungekuwa resource constrained kama wenzetu, halafu ukachanganya na uongozi tulio nao, basi tungekuwa tumeshambaratika kama taifa.
..hiyo budget surplus ya wapinzania if it is something that we can have over a number of years inaweza ku-finance miradi mikubwa ya kiuchumi. tatizo letu ni kwamba watawala ni wezi na wajifunga akili zao kwamba haiwezekani.
JokaKuu,NasDaz,
..kwanza umeshajifunga mawazo yako kwamba HATUWEZI.
..sasa ongezea hapo na UZEMBE na UFISADI basi ndiyo maana Tanzania ipo hapa ilipo.
..nitakupa mfano mdogo: hivi kuna sababu yoyote ile ya msingi ya kuwa na mgao wa umeme for 20yrs? tatizo hili limekuwepo tangu JK yupo wizara ya madini na nishati na nimeng'ang'ania mpaka sasa hivi anaelekea kustaafu.
..Tanzania haipigi hatua za kimaendeleo zinazoendana na kiwango cha rasilimali tulizo nazo. hicho ndicho kinachonifanya niamini kwamba ktk eneo hili tumeshika mkia. kwa maneno mengine ni kwamba tungekuwa resource constrained kama wenzetu, halafu ukachanganya na uongozi tulio nao, basi tungekuwa tumeshambaratika kama taifa.
..hiyo budget surplus ya wapinzania if it is something that we can have over a number of years inaweza ku-finance miradi mikubwa ya kiuchumi. tatizo letu ni kwamba watawala ni wezi na wajifunga akili zao kwamba haiwezekani.
Nilikuwa sijafahamu kwamba kumbe nawe ni mtu wa hovyo hovyo sana humu jamvini! Eti nina chuki na CHADEMA, pyuuuu!!! Pole sana, usidhan kwavile wewe unashikiwa akili na wanasiasa basi ndo kila mmoja yupo kama wewe!Umeekeza kwa kirefu kuhusu mtazamo wako kwa watanzania na wanasiasa wa kitanzania bila kuweka wazi itikadi yako ya kisiasa.Lakini kwa mtu makini atagundua wewe ni mwana-CCM tena mwenye chuki dhidi ya CHADEMA.
Nyinyi ndio wale ambao mkiulizwa uko chama gani unajibu "mimi sina chama"!
...lazima tujilinganishe na wengine, kama tusipofanya hivyo, tutapima vipi maendeleo yetu. kuna kitu kinaitwa benchmaking, unakifahamu.Ni bahati mbaya sana katika analysis zetu huwa tunajilinganisha na watu wengine; this's completely wrong!
...reli tunayo! uliza iko wapi! tunakumbuka mambo ya msingi, ndio maana wewe unanun'gunika hapa.Watu wengi tumekuwa hodari wa kuponda linapokuja suala la kutokuwa na reli lakini wakati tunaponda tunaponda tunasahau mambo mengine ya msingi.
...what about the worst one? au hili umelisahau?The best manager ni yule anayefanya rational decision pale anapokabiliwa na multiple objectives...hili wengi wetu tunalisahau!
...hili la kushuka kwa ufaulu kwenye shule, tumetoka nalo enzi za uhuru? na la reli kutofanya kazi je? la umeme kukatika ovyo?Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa budget constraint; hili ndo tatizo la msingi hasa pale manager anapokabiliwa na multiple objectives! Tusijitie upofu, nchi hii ina matatizo lukuki(multiple objectives) na mengi yake kama sio yote tumetoka nayo tangu enzi za uhuru. Mambo ambayo labda yalitakiwa kufanyika in 1960's or 1970 or probably 1980's if not 1990's ndo yanafanyika sasa!
...a rational manager anabaini mahitaji na kufanya lile lenye faida zaidi, politics aside.Sasa basi, a manager anajikuta kati kati ya nchi kutokuwa na barabara na nchi kutokuwa na reli....hakuna ubishi, yote yana umuhimu mkubwa kwa ustawi wa nchi lakini kwavile ana-operate under budget constraint, huyu manager anatakiwa ku-choose among multiple objectives. A rational manager hawezi ku-opt kujenga reli wakati nchi haina barabara kwa sababu maamuzi yake yanatakiwa kuwa na impact in both sides; economically and socially!
...ungekuwa na uchaguzi wa kurahisisha usafiri wa mizigo au abiria ungechagua upi? maana, huo wa mizigo -kwa maana ya reli au barabara- ndio abiria huutumia. au kuna tofauti siioni?Mjerumani wakati anajenga Reli ya Kati hakuangalia social impact kwavile suala la Mnyamwezi kutoka Tabora kuja Dar atumie gari/treni au aje kwa mguu haikuwa juu yake(Mjerumani). Mjerumani huyu alichojali ni kuhakikisha mazao ya aina mbalimbali yanatoka bara hadi Dar es salaam(bandarini); basi! Lakini leo hii kunapokuwa na serikali ya wananchi, decision maker lazima ajiulize; kwamba hata kama tutarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka na kwenda bara; what about usafirishaji wa watu/abiria? And what about sehemu zile ambazo reli haitapita hasa tukizingatia hatuna uwezo wa kutengeneza rail networks?
...nchi za ulaya zisingekuwa na reli, kwa tafsiri hii. reli hazijengwi ili kufurahisha mtu/watu na kupata mtaji wa kisiasa, bali kuleta maendeleo mapana zaidi, kama, kupunguza gharama na muda wa usafirishaji bidhaa, kubeba mizigo mingi na mikubwa kwa pamoja, na hivyo kupunguza gharama za ujenzi na marekebisho ya barabara.Kwa mtu anayezingatia socio-economic impacts lazima ata-opt kujenga barabara kwavile anafahamu akija kupata 900 billion zingine; hatazitumia kumalizia reli ya kwenda Mwanza tena bali atazitumia kwa ajili ya kuboresha route nyingine!
...where do you get your facts from? hebu tueleze, ukitaka kusema Tz imeendelea unailinganisha na nani? US?Kwa bahati mbaya sana tunapenda kujilinganisha na Kenya huku tukisahau kwamba wakati Tanzania tunahangaika na barabara kuu, wenzetu Wakenya barabara hizo tayari wanazo miaka na miaka! Kwa maoni yangu, Wakenya wamechelewa sana kujenga railway ya kisasa kwavile uchumi wao tayari ungewaruhusu kufanya hivyo more than 20 years ago.
...usitumia neno "busara" vibaya.Hivyo basi, mtazamo wangu ni kwamba serikali ilifanya uamuzi wa busara kuanza kuangalia roads network kabla ya kuanza na reli...nazungumza hili kwavile siwezi kujitia upofu na kudhani kwamba kuna billions of dollars outta there lakini zinawasubiria akina Kikwete wakazibebe kwenye mabegi na waje kujengea reli! Njia nyepesi ya kufahamu haya mambo ni kuangalia personal planning/budgeting/financing. Watu tujiangalie wenyewe kuna mambo mangapi tunakusudia kuyafanya na tunafanikiwa mambo mangapi na kwanini tumefanya hili na sio lile! Ukiangalia critically utagundua kwamba mara zote ulikutana na multiple objectives wakati upo constrained na bajeti.
Watu tunajadili mambo ya msingi kishabiki kanakwamba hili taifa linamilikiwa na kikundi flani na wengine ni wakimbizi. Siasa inapelekea watu kuweka akili zao mfukoni na kutoa mawazo ili mradi kuvutia kule mapenzi yake yalikolalia, kwa staili hii hatuwezi kusogea mbele hata kidogo. Mtu mwenye uwezo wa kukosoa tu bila kutoa mapendekezo ya nini kifanyike ni mtu mbaya sana. Nawachukia watu wa aina hii.
Umeekeza kwa kirefu kuhusu mtazamo wako kwa watanzania na wanasiasa wa kitanzania bila kuweka wazi itikadi yako ya kisiasa.Lakini kwa mtu makini atagundua wewe ni mwana-CCM tena mwenye chuki dhidi ya CHADEMA.
Nyinyi ndio wale ambao mkiulizwa uko chama gani unajibu "mimi sina chama"!