Ndugu yangu huo ndio ukweli, angalia Airport mpya, Makao makuu ya Dodoma, SGR, Bwawa la Nyerere na miradi mingi tu ni michakato ya muda mrefu huwezi mwezi tu ukasema tunaanza mradi mkubwa kama SGR kesho ni mambo yanapitia process ndefu kuandaa mradi. Hata Kikwete yeye alirithi mambo aliyoanza Mkapa. ILa JPM alikuwa na uthubutu na vilikuwa vipaumbele vyake. Kila Rais anakuja ndio ilani ipo labda ya miaka 5 na akafanya yale anayodhani muhumi kwake na mengine akaacha yaendelee akaja mwingine akaona hili muhimu kwake kuliko lile, ila ni Ilani ya chama tawala.