Rais kuiagiza TFF kuiongelea vizuri Yanga kuelekea fainali alimaanisha nini?

Pia mama yetu ni mtu wa mitandao.Anaona na kuyasoma yanayoendelea mitandaoni humu...
 
...juzi msanii yule kule kwa madiba alikuwa kanuna muda wote wakati Yanga wanajilia vyao ugenini na watu wote wanafuraha na kushangilia yeye na macho yake kama karunguyeye kasoro yeye white anaangalia anagalia tu huku na huko utadhania kuna jambo limemkuta,alikuwa hajielewi hata kwa nini yupo uwanjani.!mdau mmoja akaniambia huyo ni kolo kindaki ndaki sema bongo dukna kachukua wizara kisela.
 
Pana Fountain Gate Princess ni mabingwa wa CAF tena ni miezi kama miwili tu iliuopita, haiongelewi kabisa.
 
Fainali ni fainali tu ndugu hata pakibadilishwa majina ya mashindano. Pana mjinga mmoja nimemsikia leo BBC akisema eti Yanga haijawahi kuwa na uongozi bora kama huu, nikajiuliza kama historia ya soka ya nchi anaifahamu.
 
Kwenye ubora wao UTO
USM ALGER DAMU
BA NTWA
Tanga mwaka huu unanafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa Afrika wanaoupigania.

1. Imesajri wachezaji wazuri.
2. Wachezaji wake wanajituma sana sana kwa bidii zote kwa hasira ya kuonekana rank ya chini kwa muda mrefu.
3. Wanafadhiriwa na Matajiri wengi Simba wanamtegemea MO peke yake.

4. Wamebahatika kukutana na timu dhaifu huku mwishoni.

Hiyo USM Alger watakayo kutana nayo fainali ni ya 7 nchini kwao.

Mimi ni Simba, ila nimekubali Yanga ina Asilimia 95 kuwa Bingwa wa Shirikisho Afrika Mwaka huu.
Na Uzuri siku ya Fainali ni Mwisho wa Mwezi Bia nitakuwepo.
 
Alimaanisha wachambuzi ucharwa sio karia kwa akili yako fupi unadhani unaweza ukawa raisi wa TFF bila kuwa mwana cccm kindakindaki.
Aliitaja TFF na rais Karia aliinuka kwenye kiti kuashiria amemsikia na kumwelea alichomaanisha Rais. Sasa wewe ndie unaeingiza tafsiri zako zisizo rasmi. Kwani TFF imeshawahi kuwakalipia wachambuzi uchwara wetu wanaocheza nje ya uwanja?
 
Mimi nilikuwa mtu wa kwanza kuitaka TFF walitolee ufafanuzi suala hilo, ni vizuri kama amekuja kuliongelea maana ni wajibu wao pia. Furahieni mafanikio yenu ila acheni upotoshaji na ubishi usio na maana.
Tukishindwa kuelewana tutawauliza caf wenyewe wafafanue kuwa hili kombe wanaloshiri Yanga ndilo hilihili Simba walifika fainali au ni mashindano mengine kabisa yenye sifa tofauti.
 
Pana Fountain Gate Princess ni mabingwa wa CAF tena ni miezi kama miwili tu iliuopita, haiongelewi kabisa.
Hata hujielewi, yaani ukiwa bingwa Afrika kwenye mashindo ya kucheza bao ndio nchi yote ikuongelee wewe!!
 
Fainali ni fainali tu ndugu hata pakibadilishwa majina ya mashindano. Pana mjinga mmoja nimemsikia leo BBC akisema eti Yanga haijawahi kuwa na uongozi bora kama huu, nikajiuliza kama historia ya soka ya nchi anaifahamu.
Yuko sahihi, malengo mama ya timu ya mpira wa miguu ni kutwaa makombe makubwa ya ndani na nje. Yanga ni mara yake ya kwanza kufika fainali CAF. Maana yake Wana uongozi Bora than ever.
 
Tukishindwa kuelewana tutawauliza caf wenyewe wafafanue kuwa hili kombe wanaloshiri Yanga ndilo hilihili Simba walifika fainali au ni mashindano mengine kabisa yenye sifa tofauti.
Ufafanuzi tumeshautoa sana humu ndani na tuliwapa link kabisa za CAF ila kwa kuwa ukweli hauendani na kile mngependa kusikia basi mnaendelea kubisha.

Ni hivi, Kombe la Shirikisho la sasa hivi ni muunganiko wa Kombe la CAF, hilo ambalo Simba walifika fainali, na kombe la Washindi. Kwa hiyo kihadhi Kombe la sasa haliwezi kuwa tofauti sana na yale ya nyuma. Nikikupa mfano, wewe hapo ni zao la muunganiko wa Baba na Mama yako, je wewe uko zaidi yao?
 
Labda baada ya kuona loyo tuwa imebuma.
 
Karia
Babra
Mo
Figisu zao zinajulikana juu ya mafanikio ya yanga CAF.... Karia huyu ndiye aliyeisagia kunguni yanga msimu uliyopita isicheze na mashabiki mechi ya Rivers. Hiyo ni tahadhari kwake mda wowote atarudi Somalia Waheed huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…