Rais kuitwa mtukufu na kuabudiwa hadharani bila kukemea inaashiria nini?

Nyerere alikuwa hapendi kujikweza! Hayo ni mambo ya magufuli!
Mimi nimeweka historia tu kwamba na yeye aliitwa Mtukufu na ilianzia kwake. Binafsi namkubali sana Mwalimu lakini huo ndio ukweli.
 
Mtoa post hujawahi ona MAJALIWA akipita huyu jamaa mbele yake huinua had mikono kuonesha utukufu wa huyu kanjanja yaaan PM huinama kama yupo altare kabsa, inaleta simanzi sana.
hahaahahaaha
 
Tuwaambie vijana historia yenye ukweli tena yenye logic. Inajulikana Mkapa alikataza na wewe unasema Nyerere hakuitwa hivyo, kwahiyo unatuambia aliyeanzisha ni Mwinyi? Bro na mimi nilikuwepo enzi za Mwalimu.
 
Tuwaambie vijana historia yenye ukweli tena yenye logic. Inajulikana Mkapa alikataza na wewe unasema Nyerere hakuitwa hivyo, kwahiyo unatuambia aliyeanzisha ni Mwinyi? Bro na mimi nilikuwepo enzi za Mwalimu.
Nazungumza kwa uhakika, maneno ya Mtukufu na Mheshimiwa yalianza wakati wa utawala wa Mwinyi.

Unajua wakati wa Mwinyi kulikuwepo na jitihada ya kutaka kuongeza hata muda wa uongozi. Kulikuwa na watu waliokuwa wanajipendekeza sana kama kipindi hiki. Wengine walifikia kusema kuwa inakuwaje yeye Mwinyi awe Rais kwa miaka 10 tu wakati Mwalimu alikuwa Rais kwa zaidi ya miaka 20. Kulikuwa na fukuto kubwa kipindi hicho, Ni bahati mbaya tu wakati ule njia za kupata habari hazikuwa rahisi Kama zilivyo sasa. Lakini Mwalimu alisimama imara kweli kuhakikisha hilo halitokei.
 
Labda nimechanganya mambo. Nitafanya utafiti zaidi. Asante.
 
ILALA KUWA JIJI; RAIS AMEVUNJA KATIBA
---------

Mnavunja SHERIA! Rais hana mamlaka chini ya Local Government (urban authorities) act kutengeneza urban authority. Hii ni mamlaka ya WAZIRI wa TAMISEMI.

Kifungu cha 7 cha SHERIA ya Local Government, Waziri anatakiwa kutoa NOTISI ya miezi 2 kwenye GOVERNMENT GAZETTE na gazeti jengine ili kuwapa wananchi muda wa KUPINGA hayo maamuzi.

Mnavunja SHERIA. Mtu asiye na mamlaka anafanya anavyotaka bila ya kufuata UTARATIBU uliyowekwa chini ya SHERIA. Magufuli akiambiwa AFUATE SHERIA na TARATIBU anapandisha HASIRA halafu anataka kuFIX watu! SHERIA ziko ili tusiwe na CHAOS! Anafanya CHAOS kwa maamuzi ya MAJUKWAA!

Wananchi wakipinga maamuzi ya Waziri, ni lazim Waziri asikilize malalamiko ya kupinga na ayachukuwe manani. Halafu anatakiwa kupeleka Maamuzi mbele la Bunge!

Kwa mujib ya SHERIA, WAZIRI ana lazima ya kutumia DISCRETIONARY POWER yake JUDICIOUSLY! Ina maana kungekuwa na PAPER kutoka WATAALAM kueleza kwanini Halmashauri zivunjwe na itengenezwi 1! Mkiitwa STUPID mnahamamki! Kwanini lakini wakati hamuelewi UTAWALA wa SHERIA?

Fatma Karume
 

Maneno na majina hayafanyi mtu kuonekana ndivyo, bali dhamira ya mwitaji na mwiita wameita na kulipokea katika "context" ipi. Kinachokusumbua wewe wenda ni sababu ya elimu yetu duni iliyopo.

Mfano, kuna watu wanaitwa Yesu, yule yesu wa MAN city. Lakini hii haina maana yule jamaa wa MAN city nikimwita Yesu naamanisha YESU mwenyewe ama yeye anajisikia ndo YESU mnazreti.

Mfano mwingine nikisema niletee mbuzi nikune nazi, haina maana uniletee mbuzi mnyama. Ama mfano mabeberu wa ulaya haina maana uniletee mbuzi dume.
Muktadha (context) wa jambo ni mhimu sana. Mfano nikisema yule mjinga amepiga shuti bunduki. Muktadha wa hayo maneno ni tofauti na utakavyochukulia kwa mtizamo hasi ki hasi.

Mungu anajua dhamira ya watu ktk muktadha wake. Wewe huna haja ya kuhangaika sana, usimfanyie kazi Mungu na kumuamlia.

Mtukufu ni neno la kawaida tu kama maneno mengine kwa kiingereza laitwa NOBLE. Hujawahi kusikia watu wakipewa noble prize?
 
Katika kutafsiri maamkizi ya kiitifaki, neno mtukufu linatokana na neno His/ Your excellency.

Kwenye Kiingereza, "Your Excellency" haina tatizo sana, kwa sababu haiunganishwi na habari za dini/Mungu.

Lakini hilo neno excellency likitqfsiriwa Kiswahili kuwa Mtukufu, linaleta utata kidini.

Mkapa alikataa kuitwa mtukufu.

Hizo habari za kusujudiwa mpaka ardhini ni level nyingine.

Kisukuma wanaume wakubwa huwa tunapigiwa magoti na wanawake, hususan tuliiwazidi umri, wakati wa kusalimiwa, lakini hili halipo kwa wanaume wanaposalimiwa na wanaume au wavulana.

Zaidi ya yote, hata habari za utukufu wa Mungu ni idea tu. Mungu hajathibitishwa kuwepo.
 
Mtukufu pia ni noble person.
Kinachowasumbua ni sababu tu ni neno limetumika ktk Bible. Ni neno kama maneno mengine.
 
Mi sina shida sana bali wasiwasi wangu ni kuwa inatoka moyoni au ndio mtumikie kafiri upate ujira wake hizi ni medani za kichawi chawi ndizo zinakupa shida wewe.
 

Pia nafikiri kivumishi tu hakiwezi fanya mtu kuchukua sifa ya mtu mwingine.
Mfano kwenye Bible Mungu anasema mimi ni "Bwana Mungu wako" mbona watu tunaitana tu ma bwana fulani na hatutishani kwamba tumechukua sifa ya Mungu? Kuna wengine hadi wanajiita ma Landlord.

Lazima nafikiri watu tuelewe kuchanganua sentenso na siyo kufanya kuzichanganya changanya ili kuwachanganya hadhira.
ukisema Bwana MkamaP ni tofauti na kusema Bwana Mungu. Watu wanakwama wapi?
 
Hiyo lugha si issue sana, issue ni hiyo image ya rais kusujudiwa mpaka ardhini.
 
Huwezi kuwapingia watu nani wamuite mtukufu na nani wamuabudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…