Rais kuitwa mtukufu na kuabudiwa hadharani bila kukemea inaashiria nini?

Rais kuitwa mtukufu na kuabudiwa hadharani bila kukemea inaashiria nini?

Kwa hili tuwe fair..Marais Nyerere na Mwinyi waliitwa hivi pia bila kuzuia. Ni Rais Mkapa ndiye aliyekuja kukataa kuitwa hivyo. Naandika hivi kwa lengo la kuweka historia sawa tu.
Sasa unaonaje whether Nyerere na Moi waliitwa watukufu,ni sahihi mbele za Mungu?
 
sasa kama viongozi wa dini waliokufunza hizi busara za kimungu wanasujudu unadhani sisi tufanyeje? Nasi tutasujudu mpaka Mungu atuondoe kwenye dhambi
 
Hili jambo limenistua na kunipa hisia hasi. Sikuamini macho na masikio yangu kwa Rais huyu huyu wa wanyonge na mcha Mungu.

Akitoa maelezo ya kutaka Maendeleo jimboni kwake Kibamba, Mbunge Issa Mtemvu alimwita Rais Magufuli MTUKUFU tena akimsujudu hadi ardhini.

Nilijua Rais atakapoamka kutoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Stendi ya mabasi huko Mbezi Louis basi angekemea kuitwa MTUKUFU Rais lakini akapiga kimya!

Nijuavyo mimi hata kama si mjuzi sana wa mambo ya dini lakini mwenye cheo cha utukufu ni Mungu pekee si binadamu mwenye nyama, damu na mifupa. Hii tabia ya kujipendekeza hadi kumwabudu binadamu mwenzio ni kumkufuru Allah.

Au nasema uongo ndugu zangu!
Watu si mpo mpo tu hata hamjui wafalme na viongozi wa watu toka zamani waliitwaje au waliheshimiwa vipi,wala si yeye anayetaka kuitwa hivyo usemavyo

Ukuu haumjii tu mtu hivi hivi,na ukimjia mtu utajua tu kua huyo ndiye mkuu,wewe unaonekana huna hata imani yoyote ya kidini
 
Kwa hili tuwe fair..Marais Nyerere na Mwinyi waliitwa hivi pia bila kuzuia. Ni Rais Mkapa ndiye aliyekuja kukataa kuitwa hivyo. Naandika hivi kwa lengo la kuweka historia sawa tu.
Umesema uwongo. Mwalimu Nyerere alikataa kabisa kuitwa mtukufu au mheshimiwa. Yeye ndiye Rais aliyesababisha viongozi wote waitwe NDUGU.

Mimi niliwahi kusoma risala mbele ya Mwalimu Nyerere nikiwa mwanafunzi darasa 5, kiongozi wa chipukizi, kila aya nilianza na NDUGU RAIS.
 
Kwa taarifa yako zamani ilikuwa inatumika Mtukufu Raisi.... Awamu ya kwanza na ya pili...

Kabla haijaanza kutumika Mheshimiwa Raisi....

Utakuwa mtoto wa juzi wewe....
Wewe ni mwongo au umehadithiwa uwongo. Mwalimu alikataa kabisa kuitwa Mtukufu. Na hakuna kiongozi aliyeitwa Mtukufu au mheshimiwa. Alipoingia Mwinyi, ndipo wabunge walipitisha mwongozo unaosema viongozi wote waliochaguliwa na wananchi Ni waheshimiwa. Na Rais Mwinyi akawa anaitwa Mtukufu Rais.

Mkapa alipochaguliwa, akakataa kuitwa Mtukufu, lakini wabunge wakafurahia kuendelea kuitwa waheshimiwa.

Msimjulishe Mwalimu Nyerere kwenye hizi takataka za kuabudiwa. Mwalimu alitaka aitwe ndugu, na viongozi wote wa wakati huo waliitwa ndugu. Hata spika alikuwa akitajwa NDUGU SPIKA.

Na hiyo iliendana na kanuni ya TANU - WATANZANIA WOTE NI NDUGU, NA AFRIKA NI MOJA. Hivyo hakuna wa kuheshimiwa wala wa kutoa heshima.
 
Hili jambo limenistua na kunipa hisia hasi. Sikuamini macho na masikio yangu kwa Rais huyu huyu wa wanyonge na mcha Mungu.

Akitoa maelezo ya kutaka Maendeleo jimboni kwake Kibamba, Mbunge Issa Mtemvu alimwita Rais Magufuli MTUKUFU tena akimsujudu hadi ardhini.

Nilijua Rais atakapoamka kutoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Stendi ya mabasi huko Mbezi Louis basi angekemea kuitwa MTUKUFU Rais lakini akapiga kimya!

Nijuavyo mimi hata kama si mjuzi sana wa mambo ya dini lakini mwenye cheo cha utukufu ni Mungu pekee si binadamu mwenye nyama, damu na mifupa. Hii tabia ya kujipendekeza hadi kumwabudu binadamu mwenzio ni kumkufuru Allah.

Au nasema uongo ndugu zangu!
Unashangaa kuitwa mtukufu wakati alishaitwa mungu ....... !!
 
Hebu weka video tuone Kama kweli unachosema
Unyenyekevu hutokana na malezi bora, unyenyekevu haushurutishwi. Mbunge wangu amefanya lililo jema
IMG_20210225_093620.jpg
 
Huwezi kuitwa majina usiyotaka, someni ktk biblia kisa cha herode na gharika aliyoshushiwa na Mola na kutafunwa na safura.
 
Inaashiria ndivyo anavyopenda.
Kabisa kampongeza na kudai anapenda wanyenyekevu mpaka akatamani kumpa binti yake , alipata raha sanaa.Gado aliona mbali sana ile katuni watu wakisalisha ubongo wao kwa dust bin mbele ya mtukukufu wao.
 
Mungu uwaacha wanaojikweza wapande wafike juu kabisa ili anguko lao lisibakishe kitu.
 
Back
Top Bottom