Rais kuitwa mtukufu na kuabudiwa hadharani bila kukemea inaashiria nini?

Rais kuitwa mtukufu na kuabudiwa hadharani bila kukemea inaashiria nini?

Upo Sahihi kabisa

Mtukufu ni mwenyezi Mungu pekee kwa upande wa Dini zote.

Ipo siku magufuli ataitwa Jehova na atachekelea tu.
Kwa huyu mkulu wetu anapenda sana sifa hizo.kama sivyo angewakemea mapema wanao msifia kupitiliza.
 
Ni kweli kabisa kuwa waliitwa watukufu!Lakini haikuwa sahihi Kuwaita watukufu hata kidogo na ndiyo maana Mkapa akakataa kuitwa mtukufu na nafikili hata Mzee Kikwete naye hakupenda kuitwa mtukufu kwa maana hawakupenda kujikweza!na hii Inatokana na utashi wa mtu binafsi kama ananendeleaje kuitwa hivyo ama laa!!
 
Wewe ni punguani.
Niambie maana yoyote ya "mtukufu" nnje ya "Utakatifu wa Mungu".
Niambie maana ya kusujudu nnje ya "kumsujudia Mungu Baba,Yehova".

Punguani wewe usiyejua maana lakini unakomaa kutukana, pole sana
Rudi darasani ukajifunze maneno yenye maana zaidi ya moja
Screenshot_20210225-110322.jpg
 
Hili jambo limenistua na kunipa hisia hasi. Sikuamini macho na masikio yangu kwa Rais huyu huyu wa wanyonge na mcha Mungu.

Akitoa maelezo ya kutaka Maendeleo jimboni kwake Kibamba, Mbunge Issa Mtemvu alimwita Rais Magufuli MTUKUFU tena akimsujudu hadi ardhini.

Nilijua Rais atakapoamka kutoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Stendi ya mabasi huko Mbezi Louis basi angekemea kuitwa MTUKUFU Rais lakini akapiga kimya!

Nijuavyo mimi hata kama si mjuzi sana wa mambo ya dini lakini mwenye cheo cha utukufu ni Mungu pekee si binadamu mwenye nyama, damu na mifupa. Hii tabia ya kujipendekeza hadi kumwabudu binadamu mwenzio ni kumkufuru Allah.

Au nasema uongo ndugu zangu!
Vichogo wana asili ya kupenda sifa na kutukuzwa
 
Kwa hili tuwe fair..Marais Nyerere na Mwinyi waliitwa hivi pia bila kuzuia. Ni Rais Mkapa ndiye aliyekuja kukataa kuitwa hivyo. Naandika hivi kwa lengo la kuweka historia sawa tu.
Nyerere alikuwa hapendi kujikweza! Hayo ni mambo ya magufuli!
 
Umesema uwongo. Mwalimu Nyerere alikataa kabisa kuitwa mtukufu au mheshimiwa. Yeye ndiye Rais aliyesababisha viongozi wote waitwe NDUGU.

Mimi niliwahi kusoma risala mbele ya Mwalimu Nyerere nikiwa mwanafunzi darasa 5, kiongozi wa chipukizi, kila aya nilianza na NDUGU RAIS.
Utakuwa rika yangu Mr Hamatan
 
Kitu pekee ambacho mwanadamu ametamani kuwa kwa karne nyingi ni kuwa mungu.

Soma historia ya viongozi wote wa kidunia ukianzia kwa Nimrod kwenye Biblia, kisha nenda kwa watawala wa Misri - Mafarao.

Vuka miaka kadhaa mpaka miaka ya akina Nebukadneza kisha njoo kwa akina Watawala wa dola kuu ya Kirumi akina Kaisari na usogee mpaka miaka ya Alexander Mkuu.

Wanadamu wanataka na kutamani kuwa juu ya ubinadamu.

Na wanadamu wengine wanawafanya binadamu wengine kuwa zaidi ya binadamu.

Note : neno mungu linaonyesha cheo/mamlaka sio jina ndio maana wahindi wana miungu zaidi ya mia nne.

Usiogope unapoona neno mungu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hili jambo limenistua na kunipa hisia hasi. Sikuamini macho na masikio yangu kwa Rais huyu huyu wa wanyonge na mcha Mungu.

Akitoa maelezo ya kutaka Maendeleo jimboni kwake Kibamba, Mbunge Issa Mtemvu alimwita Rais Magufuli MTUKUFU tena akimsujudu hadi ardhini.

Nilijua Rais atakapoamka kutoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Stendi ya mabasi huko Mbezi Louis basi angekemea kuitwa MTUKUFU Rais lakini akapiga kimya!

Nijuavyo mimi hata kama si mjuzi sana wa mambo ya dini lakini mwenye cheo cha utukufu ni Mungu pekee si binadamu mwenye nyama, damu na mifupa. Hii tabia ya kujipendekeza hadi kumwabudu binadamu mwenzio ni kumkufuru Allah.

Au nasema uongo ndugu zangu!
Kumuita MTUKUFU linaweza kuonekana kama jambo la kawaida, ila hadi kumsujudia, ni LAANA! Ni dhahiri huyo bwana ni muoga wa maisha, kwa upeo wake wa kutojiamini anahisi kujipendekeza kwa mwadamu ambae hawezi kuongeza hata nukta 1 ya maisha yake, dhahiri ana upungufu kwenye fikra zake.
 
Hili jambo limenistua na kunipa hisia hasi. Sikuamini macho na masikio yangu kwa Rais huyu huyu wa wanyonge na mcha Mungu.

Akitoa maelezo ya kutaka Maendeleo jimboni kwake Kibamba, Mbunge Issa Mtemvu alimwita Rais Magufuli MTUKUFU tena akimsujudu hadi ardhini.

Nilijua Rais atakapoamka kutoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Stendi ya mabasi huko Mbezi Louis basi angekemea kuitwa MTUKUFU Rais lakini akapiga kimya!

Nijuavyo mimi hata kama si mjuzi sana wa mambo ya dini lakini mwenye cheo cha utukufu ni Mungu pekee si binadamu mwenye nyama, damu na mifupa. Hii tabia ya kujipendekeza hadi kumwabudu binadamu mwenzio ni kumkufuru Allah.

Au nasema uongo ndugu zangu!
Binafsi nakushangaa wewe unayetegemea Magu akatae utukufu. Hata hivyo huyo Mtemvu hakufika 100% ya akitakacho Magu kuhusu kuabudiwa. Yeye anataka kila mtu nchi hii amwimbe yeye, amwabudu yeye, amsikilize yeye, kila kitu ni yeye!

Anasema "Mimi najua mengi ndugu zangu"
 
Hujwahi kuwa na hisia chanya kwake hata siku moja. Majaji wanaitwa 'Your Lordship' hujawahi kulalamika. Malkia wa Uingereza anaitwa 'Her Majesty', 'Her Royal Highness', 'Your Royal Highness' hujawahi kuhoji. Kusujudu hiyo ni tafsiri yako yenye fikra hasi siku zote.

Hata huyo aliyemwita mtukufu analikuwa na lake jambo namna bora ya kuliwasilisha ijapokuwa hadhi yake aliikweza sana hata hivyo haikuwa lazima amkemee mbunge kwa kuwa ni mwakilishi wa wananchi hata huyo aliyeitwa mtukufu hivyo isikuume kiasi cha kukukosesha hata usingizi ewe mwanasiasa wa kudandia unayeandika ukiwa nje ya mipaka ya nchi.
Kwa hiyo na yeye ni Beberu? Maana naona unamfananisha na heshima wanayopewa mabeberu.
 
Ndugu yangu duniani napo kuna watukufu. Hilo lisikuumize kichwa.

Walikuwepo watukufu hapo kale kidogo japo kwa sasa hawaitwi tena watukufu. Mfano Mtukufu Ali Hassani Mwinyi, Mtukufu Daniel Arap Moi....n.k

Bb johnthebaptist
Mtukufu Iddi Amini, Mtukufu Hitler, Mtukufu Mobutu, N.K. Nashukuru sasa tunaye rafiki wa hao niliowataja.
 
Back
Top Bottom