Hili jambo limenistua na kunipa hisia hasi. Sikuamini macho na masikio yangu kwa Rais huyu huyu wa wanyonge na mcha Mungu.
Akitoa maelezo ya kutaka Maendeleo jimboni kwake Kibamba, Mbunge Issa Mtemvu alimwita Rais Magufuli MTUKUFU tena akimsujudu hadi ardhini.
Nilijua Rais atakapoamka kutoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Stendi ya mabasi huko Mbezi Louis basi angekemea kuitwa MTUKUFU Rais lakini akapiga kimya!
Nijuavyo mimi hata kama si mjuzi sana wa mambo ya dini lakini mwenye cheo cha utukufu ni Mungu pekee si binadamu mwenye nyama, damu na mifupa. Hii tabia ya kujipendekeza hadi kumwabudu binadamu mwenzio ni kumkufuru Allah.
Au nasema uongo ndugu zangu!